Mi nashindwa kuwaelewa wasomi wa kitanzania. Watu walikuwa wanasoma wakijiaminisha 100% kwamba wataajiriwa na serikali. Hili ndo linaleta matatizo kea watu wengi kiasi kwamba watu wanashindwa kuona njia nyingine ya kimaisha.
Kuna shule binafsi bado zinahitaji watu waliosoma lakini competent. Tatizo kama mtu ulitegemea uajiriwe na serikali ambayo mara nyingi cheti kinatosha we kuwa compentent, hapo tatizo ndo linapoaanzia.
Pili, Kuna uhaba wa walimu kweye vyuo vikuu hata kwa masomi hayo ya arts. Tatizo wengi hawalioni hili, kwamba wanaweza kusoma masters na hadi PHD kwasababu watu hawa hawapo wa kutosha. Watu wanafikria kurudi nyuma walikotoka kwenda kulima.
Tatu, ukishasoma mpaka level za masters bado unaweza ukatafuta kazi nchi nyingine. We hukusoma uajiriwe Tanzania tu. Kama Rwanda wameanzisha courses za Kiswahili na wanahitaji walimu wa lugha nyingine kama kiingereza. Hizi fursa zipo hata nchi kama za Burundi na nyinginezo.
Mi nashauri wasomi wa Tanzania mpanuue wigo wa kufikiri kiweza kuona hata mambo mengine. Siamini kwamba kazi zimeisha ila watu waliobobea (specialize) kwenye masomo fulani bado wanahitajika. Tujikite kujiendeleza kuliko kukakaa tunalalamika.