Uadililifu wa Kamati ya Maadili na usalama ya CCM ni upi kwa siasa za Tanzania?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kamati ya Maadili na usalama ya CCM imepokea na kujadili wana ccm 38 waliotia nia na kupeleka majina matano (5) Kamati kuu badala ya kupeleka majina yote na mapendekezo kama Katiba ya CCM inavyoagiza. Je huo ndio uadilifu wao? Pia kuna tetesi kuwa mchujo ulifanyika nje ya Kamati ya maadili na hivyo kukabidhiwa majina matano tu kufuata utaratibu. Je huo nao kama ni kweli ni uadilifu? Kama haya yalifanyika ni kweli kwa chama kongwe kama ccm je vyama vichanga viige nini kwake na ccm itabaki salama kwa dosari hizi katika karne hii ya siasa za vyama vingi? Nawasilisha kwa mjadala wanajamvi.
 
Tuwekee hivyo vipengele vya katiba unavyosema vilivyokiukwa tuvisome, la sivyo, zitabaki kuwa ni porojo tu.

Halafu mwenyewe unaandika mwenyewe hauna uhakaika unauliza "Kama haya yalifanyika ni kweli...".

Wewe ulete hii habari halafu wewe utuuluize sisi kama "ni kweli"!

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Punguani wahed.
 
Fox acha ghadhabu. Yote yaliyotokea Dodoma tunayajua sote na mtoa mada ameomba tujadili mimi sijaona upunguani wake ila naona mihemko yako ukijaribu kuweka mazingira ya kutaka kukwamisha mjadala huu kwa maslahi unayoyafahamu wewe binafsi.
 
"Punguani wahed" hili neno kalitumia Faiza Foxy kwenye huu uzi....nini maana yake nami nianze kulitumia,maana namuamini saana huyu kwenye Imani.Siku zote nimemuona Faiza muadilifu na ni mkweli.
 
Back
Top Bottom