Tv ya asili inamtesa mke wangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tv ya asili inamtesa mke wangu.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Kiranja Mkuu, Apr 6, 2011.

 1. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jirani aliibiwa simu miezi miwili nyuma nikiwa kazini, akasema wote waliokuwepo muda huo waende kwa mganga wa kienyeji mwenye Tv asilia ili wamuone mwizi wa simu. Huko walinyweshwa maji ya dawa yaliyochanganywa na damu mbichi. Tangu wakati huo afya yake imedorora sana, ameota vinyweleo vingi mwilini. Ana ndevu za sharafa na mustach, garden lavu pia limeshamiri kifuani. Kuweweseka hakumuishi usiku, raha hana. Je nimsaidiaje? Mimi ni mtafiti wa gas hivyo muda mwingi nakuwa site.
   
 2. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaka mmm!!!!!! hivi mpaka ukamluhusu mkeo aende kwa mganga wa kienyeji kwani yeye ndiye aliyeiba simu? Kama ww ni mtafiti wa gesi bila shaka umeenda shule. Na hilo lingekuwezesha kuachana na kasumba za ramli. Mwizi wa simu toka lini akaonekana kwenye luninga?? Kwa namna moja ama nyingine umechangia kwa mkeo kushiriki katika mambo hayo. Hata kama hakukuaga, ingekuwa unapinga hayo mambo pengine angeogopa kwenda huko. Sasa la maana hapa ni kumpeleka kanisani akaombewe na hayo mapepo/majini aliyopewa huko alikokwenda yamwishe. Na mwisho nakupa pole sana kwa yaliyokukuta. Mwizi huwa anatafutwa na Polisi, japo hawaaminiki siku hizi lakini ni bora kuliko mganga wa kienyeji.
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,049
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka, waganga wajadi ni kifo
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,759
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Pole sna kaka jaribu kumshitaki huyo aliempeleka mkeo kwa waganga!
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,901
  Likes Received: 19,473
  Trophy Points: 280
  Hao wengine waliokwenda na wao wanazo hizo "symptoms"?

  Hizo "symptoms" ni za madawa ya vidonge ya kujichubuwa mwili uonekana mweupe, chunguza mkeo, kama anaanza kuwa muhindi, muarabu au mzungu ghafla, basi si ramli hiyo, ni hayo madawa ya kujichubuwa.
   
 6. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mpwa, sikumruhusu aende kwa waganga, ameenda kwa shinikizo la majirani. Mimi ningekuwepo yote yasingetokea.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Chukua GAS na Mbabuebabue mwilini.

  Nywele zote zitafilia mbali. Ila fungua dirisha maana harufu ya nywele zinapoungua, mhhhhh.........
   
 8. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hao wengine hawana dalili zozote kama za mke wangu, ila mmoja alitoka mapunye mwili mziuma
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 56,901
  Likes Received: 19,473
  Trophy Points: 280
  Jee, na hilo la weupe, umechunguza?
   
 10. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,049
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  kwanini msiende taasisi ya kansa?
   
 11. BCR

  BCR Senior Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole kaka, usikate tamaa,
  mgeukie YESU atawafungua,
  nakushauri uende kwenye kanisa la kiroho aombewe maana atakuwa amewekewa mapepo,
  uko mkoa gani
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,774
  Likes Received: 504
  Trophy Points: 280
  ushauri mwingine kama kuna sumu karibu unaweza ukanywa bila kupenda.
  Khaa!
   
 13. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,049
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Husninyo JF ina mambo mengi kana unga wa ngano
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,489
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Kwani hii habari ni KWELI au ni mambo ya JF? Mie niliona kuwa jamaa anafurahisha JF na mie nikaona NIUNGE mstari......

  Kama ni kweli basi nashauri waende kitengo cha kuchunguza Sumu mwilini.......

  Au urudi kwa mganga huyohuyo na kumpa WARNING kuwa kama My Wife wako asipopona ndani ya wiki moja, basi utamshaki mahakamani ili aubebe msalaba wake kama Mkulo alivyoagiza............
   
 15. NOT FOUND

  NOT FOUND Senior Member

  #15
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MZEE ATAKUWA KATUMIA VIPODOZI VYA KICHINA HUYO,
  NA BADO!! ATAKUJA KUWA KAMA HUYU HAPA, NA MIDEVU KULIKO WEWE.  [​IMG]
   
 16. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ntapeleka ushahidi gani mahakamani. Uchawi upo ila ni ngumu kuthibitisha.
   
 17. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ushauri mwingine hauna tofauti na nguvu za giza!!!!!!!!!!!!!!!!
  By the way nakushauri umpeleke mkeo hospitali fasta kabla hali haijawa mbaya zaidi.Maana inaonyesha kabisa kuwa moja ya athari za hiyo dawa aliyokunywa ni kuongezeka zaidi kwa homoni za kiume na ndio maana ameota vinyweleo miwli mzima.Hilo tatizo linatibika hivyo wahi mapema.
   
 18. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nimemfuata mganga, anasema mke wangu hakuwa mteja wake, ila alipelekwa tu kwa huyo mganga kama shahidi, hivyo basi hana uwezo wa kumtibu hayo madhara aliyoyapata.
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,616
  Likes Received: 21,237
  Trophy Points: 280
  ukiishi uswazi bana

  kuibiwa vitu vidogo tu kwa waganga..
  hiyo pesa ya waganga si ungeweka grills........
   
 20. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  asante sana kwa ushauri
   
Loading...