Tv shows binafsi zinawalipaje wahusika?

Tv shows binafsi zinawalipaje wahusika?

Ford Range

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2016
Posts
351
Reaction score
537
Wadau naomba mwenye uelewa kuhusu namna gani vipindi vya televishen vinavyoendeshwa na kumilikiwa na watu binafsi vinawafaidisha? Vipindi kama mkasi, Rita Paulsen show,Sporah show, Mboni talk show , Wanawake live n.k ni kwajinsi gani vinawalipa? Je kwa kipindi cha nusu saa mpaka saa nzima bei ya kulipia airtime ni kiasi gani?
Karibuni!
 
Sina uhakika mkuu ila nafkiri sponsors ndio wanawalipa pamoja na matangazo mbali mbali ya biashara yanayolipiwa. Ngoja waje wajuzi watakuelewesha zaidi
 
Wadau naomba mwenye uelewa kuhusu namna gani vipindi vya televishen vinavyoendeshwa na kumilikiwa na watu binafsi vinawafaidisha? Vipindi kama mkasi, Rita Paulsen show,Sporah show, Mboni talk show , Wanawake live n.k ni kwajinsi gani vinawalipa? Je kwa kipindi cha nusu saa mpaka saa nzima bei ya kulipia airtime ni kiasi gani?
Karibuni!
Cc Pasco
 
Mfano kama kipindi cha wanawake show yale matangazo uyaonayo ndo wadhamini wao wanaolipia air time,na pia wanapokosekana wadhamini mwenye kipindi itakubidi ulipie airtime
 
Mfano kama kipindi cha wanawake show yale matangazo uyaonayo ndo wadhamini wao wanaolipia air time,na pia wanapokosekana wadhamini mwenye kipindi itakubidi ulipie airtime
Kwa maana hyo, wamiliki wa kipindi wanajilipa kutoka ktk kile kinachobaki baada ya gharama za uendeshaji. Sijui kama nipo sahaihi
 
Wadau naomba mwenye uelewa kuhusu namna gani vipindi vya televishen vinavyoendeshwa na kumilikiwa na watu binafsi vinawafaidisha? Vipindi kama mkasi, Rita Paulsen show,Sporah show, Mboni talk show , Wanawake live n.k ni kwajinsi gani vinawalipa? Je kwa kipindi cha nusu saa mpaka saa nzima bei ya kulipia airtime ni kiasi gani?
Karibuni!
Wakuu Nguvu na Joseverest, asanteni kunitonya.
Mkuu Fodi Renja, vipindi vyote binafsi kwenye TV, vinalipiwa na wadhamini katika taratibu za aina, tatu.
1. TV inakufanyia productions wewe unakuwa presenter, TV inakulipa wewe gharama zako za presentation halafu fedha za wadhamini ni mali ya TV. Aina hii ni kama Talk Shows za Jenerali on Monday, The Hamza Kasongo Hour, Jee Tutafikac, na This Week in Perspective.
2. Co Proranduction ni pale ambapo wewe mwenye kipindi utafanya production, halafu TV Station atatoa airtime, kisha fedha za udhamini, mnagawana na TV Stations. Hivi ndivyo zilivyo talk shows nyingi, na hurushwa na kituo kimoja cha TV .
3. Private Programme ni wewe mwenye kipindi, unagharimia production, kisha unalipia airtime halafu fedha zote za udhamini zinakuwa zako. Hivyo kipindi unaweza kukirusha popote hata Vituo 10.

Kwa national wide stations, rate za 30min airtime, TBC ndio the cheapest, TZS. 2,000,000/=, Star TV 2,400,000, Channel Ten 2,500,000 na ITV ni 5,000,000.

Kwa ufafanuzi zaidi tembelea
[URL="https://www.jamiiforums.com/threads/jee-una-kipaji-cha-utangazaji-jinsi-ya-kujiajiri-utayarishaji-na-utangazaji-vipindi-vyako-vya-tv.1206955/page-4"]Jee Una Kipaji cha Utangazaji?. Jinsi ya Kujiajiri Utayarishaji na Utangazaji Vipindi Vyako vya TV.[/URL]

Paskali
 
Mkuu Paskali Mayala, Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako ambao umejibu kila kitu ktk uzi, asante sana kwa Joseverest pamoja Nguvu kwa kumuita Paskali kutoka huko alikokuwa.
 
Mi nataka kujua kumiliki team ligi kuu unawezaje pata faida au ni kujitolea na wadhamini uwa wanapataje faida kutokana na udhamin wao
 
Wadau naomba mwenye uelewa kuhusu namna gani vipindi vya televishen vinavyoendeshwa na kumilikiwa na watu binafsi vinawafaidisha? Vipindi kama mkasi, Rita Paulsen show,Sporah show, Mboni talk show , Wanawake live n.k ni kwajinsi gani vinawalipa? Je kwa kipindi cha nusu saa mpaka saa nzima bei ya kulipia airtime ni kiasi gani?
Karibuni!
MATANGAZO YA BIASHARA,WALE GUEST WENGINE HUWA WANAOMBA WATOKEE WANALIPIA HULINGANA NA MAKUBALIANO,SOME MESSAGES DELIVERED ZINAKUA ZINATOKA MAHUSUSI BAADA YA MTU FULANI NJE KUTOA PESA ILI KULETA USHAWISHI FULANI,
 
Back
Top Bottom