Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, nikitayarisha vipindi vyangu vya TV na Redio na kuvitangaza kupitia vituo mbalimbali vya Televisheni, Redio na kusambaza habari kwenye Magazeti.
Kama una kipaji cha utangazaji, au hata bila kuwa na kipaji wewe lakini unataka kuanzisha production studio yako ya kuandaa vipindi vya Redio na TV, kuna fursa ya kutengeneza pesa, hivyo karibu nitakushauri humu jf bure.
Nakiri kupandisha uzi huu, kufuatia ombi la mwana jf huyu.
Kuanzisha Kipindi Binafsi cha TV.
1.0 Kwanza uwe na wazo. Program Idea
Wazo au Program Idea ndio ndio utajiri mkubwa kuliko kitu chochote. Wazo ni kipindi kuhusu nini, maudhui ya kipindi, lenoo la kipindi ni nini?. Unataka kuonyesha nini, au watu waone nini?, jee hao watu wakiishaona hicho unachotaka kuonyesha, watapata nini?, habari, elimu, burudani, ushawishi, etc. Jee ni kipindi cha aina gani na kitaendeshwaje?.
2.0 Aina za Vipindi vya TV. Type of TV Program
Kuna aina nyingi za vipindi vya TV.
Kuna TV Documentary, TV Talk Show, TV Reality Show, TV VOX Pop, TV feature, TV Descriptive, TV Exhibition show, Live TV Broadcasting, Special TV Prog, TV Interview Prog. etc.
3.0 Mwendeshaji wa Kipindi/Mtangazaji. TV Presenter, Host, Anchor
Nani atakiendesha kipindi, Mtangazaji, kama ni wewe mwenyewe, jee una kipaji?, una uwezo?, una sauti?, unatazamika? (photogenic)
4.0 Mtayarishaji wa Kipindi /Producer
Nani atakitayarisha kipindi?, nani atakitengeneza kipindi?, yaani producers. Wako watayarishaji wa aina tatu.
4.1 TV Stations-
Vituo vya TV ndio wenye vifaa vyote vya production. Ukipeleka wazo lako kwenye TV yoyote wakiridhia TV hiyo wanaweza kukubali kuwa the producers wa kipindi chako na mkakubaliana kugawana mapato, wao watakitengeneza bure na kukirusha bure, kisha hiyo TV wakulipe wewe, au mgawane mapato.
Advantage: The easiest and the cheapest, unachohitaji wewe ni kuwa tuu na wazo la kipindi hata kama huwezi kutangaza, hiyo TV watakutafutia mtangazaji.
Disadvantage: Wazo linaweza kuibiwa, ama wanaweza kukulalia kwa kulipwa kiduchu, kisha wao ndio wakatengeneza faida.
Copyright ya Kipindi i ya TV Station, hicho lazima kirushwe na TV hiyo tuu wanayokutengenezea.
4.2 Production House/Studio.
Hizi ni makampuni ya production ambayo unapeleka wazo lako, wanakupa gharama za kukutengenezea kipindi chako, unawalipa, yaani unapewa production cost, unalipa wanakutengenezea kipindi chako. Bongo makampuni ya kutengeneza vipindi yako zaidi ya 100.
Advantage: Mkiisha kubaliana bei, kipindi kinakuwa ni mali yako na uko free kukirusha TV yoyote.
Disadvantage: Its an expensive exercise kwa sababu lazima kwanza uwe na fedha za kulipia hiyo production.
4.3 Own Production.
Hii ni baada ya kuwa na wazo, una invest kwenye vifaa, unakuwa una own a production yako mwenyewe kama mimi nilivyo na PPR.
Hivyo unatengeneza vipindi mwenyewe na kuamua utavirusha wapi. this is what I do.
Advantage: This is the best option, vipindi unatengeneza mwenyewe kwanza kwa kutafuta sponsor wa kugharimia production cost, na kuvilipia airtime cost, anakulipa wewe, kisha mwenyewe, una produce, unalipia airtime halafu pesa yote inayobakia inakuwa ni pesa yako.
Disadvantage: Its an expensive undertaking, lazima uwe na mtaji wa kununua vifaa na viko expensive, na lazima uwalipe watendakazi, ila sio lazima kuanza na kila kitu, unaweza kuanza na baadhi tuu ya vifaa vya muhimu, halafu vifaa vingine vyote ukakodisha, kila kifaa kinakodishika na gharama ni cheap kukodi kuliko kutumia pruduction house.
5.0 Vifaa vya Production.
Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo as Basic Equipments za Own Production
5.1 Professional Camera angalau 1 kwa kuanzia ila standard good production ni kamera 3 na kuendelea. Simple good camera ni Milioni 2, expensive ni hadi milioni 100
Kadri unavyotumia kamera nzuri, ndivyo kipindi kinakuwa kizuri zaidi. Kamera nzuri kwa Broadcast ya Tanzania ni Sony HDV ila hata SLR (hizi za still kama Canon na Nikon zina video na zinaweza), wenzetu sasa wako kwenye 4K quality, sisi bado tuko kwenye HD.
5.2 Uwe na Mic nzuri 500,000 - 2,000,000 (wireless)
5.3 Taa angalau 2, 100,000-500,000 (kwa kuanzia sio lazima sana mfano mimi vipindi vyangu vingi, navifanya nje kutumia natural light, mwanga wa jua ambao ni bure.
5.4 Editing bench ni computer ya kueditia hata any good laptop can do. Computer zinazoongoza kwa kupiga kazi ya production ni Mac (apple) ila hata Windows za kawaida zinaweza, kinachohitajika ni high specs tuu kwa upande wa graphic card
Apple Macbook Pro ya bei poa used ni 1.5 mkononi
Vifaa vyote vipya na used vinapatikana. Vyote vina faida zake na hasara zake.
Advantage and Disadvantage of New Equipments
Advantage: Vifaa vipya vina faida moja, vina good quality, vina uhakika na vina guarantee, vitadumu kwa muda mrefu kabla ya kuchoka.
Disadvantage: Vifaa vipya ni kwanza ni ghali, they are expensive lakini pia getting the genuine ones ni changamoto!, vingi ya vifaa vya producton ni famba za kutoka China na Dubai hivyo havidumu.
Advantage and Disadvantage of Used Equipments
Advantage: Vifaa used, vina faida mbili, kwanza bei yake ni cheap, pili ni vifaa genuine vya ukweli
Disadvantage: Havina guarantee na vingine vimetumika sana hadi kuchoka, hivyo unakaa navyo kidogo tuu vinachoka. technology yake imepitwa na wakati.
Yapo maduka ya vifaa vyote full iliwemo
1-Sony pale Samora.
2. Duka la Deo Filikunjombe pale NSSF Benjamin Mkapa Towers
3. AL Muntazil Mtaa wa Jamhuri.
4. Kuna duka Shoppers
5. Kuna duka Mlimani City
6. Kuna duka Quality Plaza
7. Arusha -Benson
8. Moshi-Bahsgwan
9. Mwanza-Barmedas
10. Dodoma kuna duka la Mchaga fulani Uhindini.
6.0 Gharama za Airtime, Airtime Cost
Ukifanikiwa kuanzisha studio yako na kutengeneza kipindi, ili kirushwe lazima kufanyike mambo matatu yafuatayo
6.1 Kipindi Kinunuliwe na TV Station.
Ukiishatengeneza kipindi chako, unawauzia TV Station, wao wanakupipa kiasi unachotaka na kukirusha kipindi, mapato yote ya kipindi chako ni mali ya TV Station.
Advantage: Kazi yako ni kuzalisha tuum yaani unauza kipaji, unakama fungu lako kwa ulaini.
Disadvantage: TV zetu zinatubania sana, watakulipa pesa mbuzi kisha wao ndio watazimake, ila TV za hapa wako radhi kulipia mamilioni kununua vipindi vya nje kuliko vya ndani.
6.2 Kipindi kirushwe bure na TV Stations Mgawane Mapato Co-production
Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakipeleka TV Station kuomba kirushwe bure, kikipata wadhamini, mnagawana 50/50 na TV Stations
Advantage: Wewe unaingia ghara za kutayarisha tuu, halafu unaingiza fedha za udhamini.
Disadvantage: Ukitokea udhamini mnene, unawafaidisha TV Stations bure.
6.3 Ukirushe kwa Gharama zako.
Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakilipia fully kukirusha kwenye TV Station
Advantage: Ukilipia kipindi, unaamua kitoke TV ngapi, unawalipa TV airtime yao wanakurushia, fedha zote ulizopata zinakuwa zako.
Disadvantage:You have to be good kupata mdhamini mzuri atakayelipa pesa za production, airtime na faida ukabaki.
Rates za Kurusha kipindi cha 30 min.
The cheapest ni TBC -TZS 2,000,000
The highest ni ITV -TZS 5,000,000
TV nyingine zote zina range hapo katikati
Ushauri kama huu niliwahi kuutoa kwa JF
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
Thanks.
Pascal
Update
Paskali

Mkuu Mkaruka, ni kweli swali nililiona nikawa nakusubiria uulize, na hapa nimeliona tena, ila hujauliza, lakini kwa faida ya wengi, haya sasa naumwaga tuu huu mtama hapa jf.Pascal Mayalla Nimekuomba angalau unipe a, b, c za namna ya kuanzisha Kipindi binafsi cha TV Kama NgazkwaNgaz, hususani taratibu na gharama zake, lakini umenitosa mkuu - Najua wewe ni mzoefu wa media

Wanabodi huu ni msimu wa Saba Saba. Nimejitolea kutangaza fursa za utangazaji kwa Watanzania wenye vipaji vya Utangazaji. Kama unajihisi una kipaji cha Utangazaji wa Redio na TV, mimi nimejitolea kufanya screening bure kule kwenye viwanja vya Saba Saba. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na Kiingilio chako kwenye Saba Saba. Zoezi la Screening litafanyika Siku ya Jumamosi Tarehe 8/7/2017 kuanzia saa 8:00 mchana ndani ya ofisi za PPR ambazo ziko ndani ya viwanja vya Maonyesho.Mkuu Abtali Mwerevu, kitu muhimu kuliko vyote kama nilivyoeleza ni kuwa na idea, wazo, that is where money lies!.
Baada ya wazo, ndipo kinakuja kipaji, ukiwa na wazo, hata kama huna kipaji, unaliuza wazo lako, kwenye TV Stations, then wao ndio watatafuta hao wenye vipaji kuendesha kipindi chako.
Baada ya kutambua kipaji, ndipo sasa unakitafutia elimu ya utangazaji. Elimu ni kitu kinachofundishika, ila kipaji ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho, kikiendelezwa kwenye the right direction ndipo kinatengeneza pesa.
Vyuo vya uandishi wa habari, kila siku vinawapika mamia ya waandishi na watangazi, ila only wenye vipaji, ndio they make it kwenye fani, wakati mitaani kuna wenye vipaji kibao, ambao hawakubahatika kupata elimu ya utangazaji, mwisho wa siku vipaji vyao vinaishia kujifia bure!.
Paskali
Paskali