Tuwe Wakweli... Isingekuwa JF Muda Huu Ungekuwa Unfanya Nini

Ningekuwa nimepumzika kitandani natafuta usingizi baada ya mihangaiko ya kutwa nzima.
 
Ingekuwa hivyo ambavyo ingekuwa,.ila sio siri halipiti lisaa bila kuchungulia jf labda nikiwa nimelala tuu otherwise ndio kijiwe changu nambari one...huko kwingine wiki inaweza isha sijagusa.....

Viva JF Viva.
 
Wakuu Tuwe Wa kweli.

JF Toka Imeanzishwa imekuwa na Mchango Mkubwa sana kwa Jamii kwa Ujumla hasa wale wanaoitumia JF kwa Manufaa .

Wengi tumefanikiwa na wengine Wametulia mahala walipo wakiendelea kujifunza mambo mengi kupitia JF.

Ukiangalia kwa Undani japo JF wanaijumuisha kuwa sehemu ya Mitandao ya Kijamii lakini Majukwaa mengi sana yamejikita katika kuelimisha zaidi.. Kuna Kila aina ya Jukwaa kulinga na Mahitaji ya Kila Member.

Kama isingiekuwa JF Muda huu ningekuwa nasinzia Hapa kazini tu Maake siyo kila Muda unakuwa na Mood ya Kazi.

Hongera Mkuu Max Melo kwa kazi Nzuri Ningependekeza Tuangalia cha Kumfanyia huyu Founder wa JF Mwisho mwa Mwaka Huu...

Nawasilisha

Mkishamaliza kupanga cha kumfanyia JF Founder Maxence Melo na Mimi mniambie ili nimpelekee Zawadi yake ya Mbuzi ' Beberu ' aliyenona kabisa ili akamchinje ale pamoja na Wanafamilia wake wote kwani nadhani bila uwepo wa JamiiForums pengina na Mimi sasa hivi ningekuwa nacheza tu Karata na akina Harbinder Seth na James Rugemalira Gerezani Segerea.
 
Back
Top Bottom