Tuwe makini sana na mikopo hii ya kutoka Bretton Woods Institutions (IMF & World Bank)

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Leo nchi yetu tumepata mkopo wa 1.3 trilioni kutoka IMF (International Monetary Fund) tumefurahia sana watanzania na kupongeza sana kwa hatua hii

Lakini ukifuatilia sana mikopo hii, ambayo mabeberu wanasema eti ni mikopo ya masharti nafuu (concession loan) kutoka kwenye hizo taasisi za kifedha za kibeberu (Bretton woods institutions) haina historia nzuri sana kwa nchi zetu zinazoendelea (Developing countries)

Watatatukopesha sana kuwekeza kwenye miradi ya kuhdumia jamii, kama mashule, hospital, lakini baadaye mikopo hiyo huwa mikubwa sana na mzigo mkubwa kwa nchi zetu zinazoendelea

Mikopo ikiwa mikubwa sana na mzigo kwa nchi zetu, watatuambia tukae chini na kuandaa mipango ya kutupunguzia mzigo wa madeni (Debt relief)

Mpango huo wa kutupunguzia madeni, kwa kawaida huwa inaambatana na masharti magumu, ambayo kumsingi sio rafiki sana kwa maendeleo ya kiuchumi kwa nchi zetu, bali masharti hayo yatakuwa rafiki zaidi wa maendeleo ya kiuchumi ya nchi zao (mabeberu)

Kwa mfano kwenye miaka ya 1990, hizo taasisi za kibeberu (Bretton woods institutions) kama IMF, WORLD BANK, IDA nk, walikuja na mpango wa Structure Adjustments programs (SAP) ambapo moja ya masharti, walitutaka tuachie uchumi wetu (soko huria) ulioambatana na ubinafsishaji kwa mashirika na viwanda vyetu muhimu vya Kimkakati (Strategic companies& industries) ikiwa eti ni kupunguzia mzigo wa gharama za uendeshaji kwa serikali

Mabeberu walituambia eti hatuwezi kutumia fedha za walipa kodi wetu, kuyapa ruzuku (subsides) baadhi ya mashirika/ viwanda vyetu muhimu vya Kimkakati kwa uchumi na maendeleo ya nchi yetu

Nini kilitokea?

Baada ya masharti yao hayo, hatimaye mashirika/ viwanda vyetu vilishindwa kujiendesha kutokana na ushindani
na hatimaye viwanda/mashirika vyetu kufa

Nini kilitokea?

Baada ya mashirika/ viwanda hivyo kushindwa kujiendesha kwa kibiashara, walitokea wawekezaji wenye lengo la kunujua viwanda/ mashirika hayo kwa lengo la kuviendeleza

Lakini kwa bahati mbaya au kwa makusudi, viwanda na mashirika hayo muhimu kwa uchumi wa yetu yalikufa na ndio ukawa mwanzo wa nchi yetu kuwa soko la bidhaa zao kutoka kwenye viwanda vya nchi zao na washirika wao kitu ambacho kwa kiwango kikubwa sana kimechangia kuua ajira kwa nchi yetu

Lakiii very unfortunately, kwenye miaka ya 2000, uchumi wa nchi za kibeberu ulipata mtikisiko mkubwa (Economic recession)

Mfano mashirika na makampuni makubwa ya nchi ya Marekani tena makampuni binafsi (Public liabilities company) kama JP Morgan, Ford, Lehman Brothers, Godman and Sachs nk yalipata mtikisiko mkubwa wa kiuchumi

Lakini cha ajabu, serikali ya Marekani kwa kutumia fedha za wzlipa kodi, walitoa ruzuku kwa mashirika hayo binafsi ili kuyanusuru yasife, wakasema eti ts too big to fall

Kitu walichotukataza sisi kudanya, ndio exactly wao wanafanya kunusuru mashirika yao binafsi na uchumi wa nchi zao kwa ujumla, kwa sababu mashirika hayo yalikuwa ni msingi mkubwa wa ajira ndani ya nchi yao

Sasa leo tutakuwa ni watu wa ajabu sana na kushangaza, eti tukiamini kuwa taasisi hizo za kibeberu wanaweza kutupa msaada wa kuokoa uchumi wa nchi zetu, ambao umeathirika vibaya kutokana na janga hili la COVID-19

Mimi naamini, kama kweli walikuwa na lengo la kunusuru uchumi wa nchi zetu za Kiafrika, basi walipaswa kutusamee madeni yetu ya nyuma na si kutukopesha, kwa sababu nchi zetu hizi za kiafrika tunatumia peaa nyingi sana kila mwezi kuservice madeni yetu (Debt expenses) ambayo kimsingi kwa kiasi kikubwa madeni yetu hayo ni kutoka kwenye hizo Multilateral institutions

Waafrika tunapaswa kuwa pamoja, kushirikiana pamoja na kutafuta suluhisho la matatizo yetu bila kuwashirikisha mabeberu

Mungu ibariki Afrika
 
Haya lete suluhisho basi tulione. Kumbuka pia madeni yetu yaliwahi kusamehewa miaka ile ya 2000's. Tulifika wapi? Tumerudi tena kukopa. Jiulize kwa nini? Sera mbovu bado tunazo, viongozi wabovu bado wapo, taasisi dhaifu bado tunazo. Lawama usiwatupie mabeberu tuu, tujitupie wenyewe ambao tumeshindwa kujiongoza miaka 60 baada ya uhuru.

 
Nchi za Asia zilizofuata ushauri WA IMF na world Bank mapema nyingi zimeendelea kuwa masikini lakini Japan, China, Taiwan na South Korea, Malaysia walikataa kufuata approach za IMF na WB na Leo ni mataifa yaliyopiga hatua.

Kwa nchi changa free market sio Jambo linalofaa.
 
Pride Rock inaongozwa na uncle SCAR kwa sasa akishirikiana na wenzake Shenzi, Banzai na Ed.

Mpaka Simba aliyefukuziwa huko mbali gerezani atakaporudi ndipo nchi itapata uhuru wake kutoka kwenye midomo na makucha ya majitu malafi.
1636679675064.png



Shenzi, Banzai, and Ed are the secondary antagonists of Disney's 1994 animated feature film The Lion King. They are a trio of spotted hyenas who were loyal followers and henchmen of Scar. Known for their sadism and haunting laughter, the hyenas dwell in the Elephant Graveyard.
 
Huo ushauri mngempa kipindi kile magufuli asikope kwa hao aliowahaminisha miaka yote kuwa Ni mabeberu!

Nyie Ni wanafiki na ni wajinga wakubwa,kutwa mnamtukana Rais halafu mnajifanya mnampa ushauri wa kumpotosha
 
Ni mada fikirishi, lakini sina uhakika kama itapata michango stahiki.

Mkuu, tuachane kabisa na hizi lawama, nchi zetu hizi siyo changa tena. Tuna umri wa miaka 60 sasa, kwa nini tuendelee kuwa tunalialia na kutaka kubebwa kila mara?

Siku za nyuma kidogo, nami nilikuwa na mawazo kama haya yako hapa; lakini sijui nilivyogeuka digrii 360 kamili!

Ni hivi mku wangu. kwa maoni yangu hakuna tena mikopo mitamu kuliko ya hawa washenzi tunaowaita mabeberu, akina IMF na WB. Hii ndiyo mikopo hasa ya kuchukua bila jasho, mradi tu ujue unafanya nini na mikopo hiyo na kufanya kweli ulichonuia kukifanya.

Kama ni elimu, fanya kweli, usitumie kimchezo mchezo haya mahela. Inua elimu ya nchi iwe bora kabisa.

Kama ni kilimo, umekopa kuinua hali za wakulima, fanya kweli, mbegu, mbolea, wataalam,n.k., ili kilimo kiwe chenye tija hasa.
Hivyo hivyo na huko kwenye sehemu nyingine kama umekopa kwa kupata umeme, barabara, reli n.k.

Baada ya kuyafanya yote haya kwa uhakika, sasa subiri waje kukudai.

Hebu nikuulize swali mkuu: ungependa nani akukopeshe kati ya hawa, mashirika ya mabeberu au serikali za mabeberu wenyewe, au wachina?

Chukulia mfano wa wachina, mnakubaliana ukishindwa kulipa dhamana mliyokubaliana iwe halali yao! Kwa mfano: tukubaliane watujengee SGR hadi Kigoma, lakini tukubaliane tukishindwa kulipa deni wachukue/waendeshe bandari yetu ya Dar es Salaam ili pesa ya kulipa deni ipatikane, kwa muda gani? Mpaka deni lote lilipwe!

Yale masharti ya hawa Breton woods institutions, haya ya structural adjustment, kwani tukitaka kuyafanya tuonavyo sisi inafaa watatunyonga? Tukikataa kufanya wanavyotaka wao kama tunaona hayana manufaa kwetu, watafanyaje? Hebu nieleze hapa, kwa maana sijui 'punitive actions' zao wanazitekeleza vipi.

Kwa hiyo, binafsi ningehimiza sana haya mahela yao ndiyo tuyachukue sana, ila tuwe na lengo la kutimiza yale tunayochukulia mahela hayo.

Hayo masharti, kama hawana uwezo wa kutuweka jela au kutunyonga tukishindwa/tukikataa kuyatekeleza kwa sababu zetu halali kuhusu maslahi ya nchi yetu, tutawapoza kwa kiswahili chetu kireeefu, huku tukiangalia maslahi yetu.
 
Back
Top Bottom