Tuwe creative kutengeneza story fupi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe creative kutengeneza story fupi.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Viol, Sep 28, 2012.

 1. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Tujaribu ku-create story fupi,unaendeleza kutunga story fupi kwa kureply pale mwenzako alipoishia,na umwachie mwingine aendelee (kupokezana),unaweza kuandika mstari mmoja,miwili au hata tatu.
  Usiweke hitimisho halafu wengine wakakosa pakuanzia.
  Mfano mi naanza
  .. Katavi alichoka na maisha magumu pale kijijini kwao,kila siku aliwaza na kuwazua jinsi ya kuanzisha maisha mapya
  yenye matumaini na raha mustarehe,wazo pekee lililomjia akilini ni kutafuta nauli ili apande basi ya kuelekea jiji la Dar es salaam ili kuanzisha maisha mapya kwa kufanya vibarua.Jumapili asubuhi akiwa stendi ya mabasi wilayani mpanda aliamua kukata tiketi,akapangiwa siti ya dirishani,mda ulipofika abiria wote walipanda ndani ya basi,mara msichana mmoja mrembo aitwaye Preta
  akaenda kusimama karibu na Katavi kisha akachukua kitambaa kwenye mkoba wake akaifuta kiti kisha akakaa na kumwonyeshea Katavi tabasamu,dereva akawasha gari na safari ya kuelekea dar ikaanza.............(endelea)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakiwa njiani kuelekea dar Katavi alikuwa akiangalia nje masaa yote..Kwa kuwa hakuzoea kusafiri mwendo mrefu,walipoenda Kama km 20 hivi Katavi alianza kutapika.
  Hali ile ilimchefua sana Preta aliyekuwa pembeni yake ila alimuhurumia sana.
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Endeleeni.....!!
   
 4. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Baada ya Preta kuona hivi alimhurumia Katavi, hivyo alifungua pochi lake na kutoa kimfuko cha rambo na kumpa abiria mwenzake huyo. Jirani yao i mean kwenye siti ya pembeni alikaa kijana mchanashati aitwaye Excellent ....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Preta akaanza kumwita kondakta....."konda konda mwambie dereva asimamishe gari kuna mtu ametapika",mara konda akaanza kufoka kwa sauti ya juu "We bhana unatapikaje ndani ya gari angalia sasa umechafua kila sehemu"konda akampa Katavi kitambaa iliyochafuka oil chafu ili asafishe kiti.
   
 6. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  eheee....endelea.....
   
 7. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
   
 8. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwakweli Preta alikua akimwonea sana huruma abiria mwenzake ndugu Katavi kwakua alikua amechoka sana na alikua ameishiwa nguvu kabisa.
  Hivyo walipo fika kijiji cha NTENDO kilometer chache kufika mjini Sumbawanga katika safari yao ya kuelekea Dar-es-salaam. Preta alimuomba bwana Excellent abilia aliyekua amekaa karibu na konda wa Basi hilo amuite tena konda huyo aliye fahamika kwa jina la SnowBall kutokana na machachari yake.
  SnowBall" alisikika Excellent akimwita konda.
  Konda aliitikia wito na kwenda pale walipokua Preta na Katavi.
  "Mbona mnanisumbua sumbua" alisema manenohayo konda wa basi kwa ukali sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Konda wa basi kwa kujua matatizo aliyokuwa nayo Katavi na kwa kuzingatia huduma ambayo Preta alikuwa ameitoa kwa mgonjwa aliamua kujisogeza eneo la tukio. Excellent aliyekuwa amekaa jirani nao alimnong'oneza kitu konda na konda kama mtu aliyekanyaga kaa la moto kwa haraka alimuita dereva wa basi aliyejulikana kwa jina moja la Autorun ...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,668
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi Bw. Autorun alikua ni dereva wa muda mrefu, alikua ni mtu makini katika kazi yake. Mara zote wananchi wa Mpanda akiwemo Preta, walipenda sana kuutumia usafiri wa basi la Bw. Autorun pindi wapatapo safari za ama kwenda mjini Sumbawanga au kwingineko.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Oya, hii Stori mwishoni inatakiwa iishe kwa kusema wakaishi kwa raha mustarehe (Happy ending)..... Haya endeleeni
   
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,668
  Trophy Points: 280
  Punde Bw. Autorun akaitikia wito na kujisogeza walipokuwepo Preta, Katavi, Excellent na Snowball. Uso wa Katavi ulikua umejaa makunyanzi na wasiwasi tele labda pengine ni kutokana na hali ya ugonjwa uliompata ghafla, alikua ameshakata tamaa ya kuendelea na safari. Wakati huo wote alikua kajilaza kwa kichwa chake kuegemea kiti kilichokuwa mbele yake. Preta na Excellent walikuwa wametulia tuli kama maji kisimani yanayosubiri mtekaji. Snowball alikua akijishughulisha kumpepea Katavi ili walau apate nafuu ya hali mbaya aliyokuwa nayo.
   
 14. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  dereva Autorun alipofika na kushuhudia hali aliyokuwa nayo Katavi, alimhurumia sana. Wakati huo Preta alikuwa busy kumpa huduma ya kwanza bwn. Katavi. Dereva Autorun alimwambia bw.Katavi ateremke kituo kinachofuata kwani alikuwa ameishiwa nguvu kutokana na kutapika sana, cha ajabu Preta alikataa bw.Katavi asiteremke bali yeye atateremka na kumchukulia maji pamoja na glucose. walipofika kituoni hapo Preta alifanya kama alivyohaidi. hali ya bw.Katavi iliimarika na safari ya kuelekea dar iliendelea. . .
  https://www.jamiiforums.com
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Baada ya safari ndefu hatimaye siku iliyofuata kijana Katavi akaingia jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza, kwakuwa hakupajua kwa mwenyeji wake yule dada waliyekaa naye siti moja akankaribisha kwao Gongo la Mboto ili ajisitiri huku akimtafuta binamu yake (mtoto wa mama yake mdogo) Boflo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  heshima yako babangu watu8, story imefikia Katavi kafika dar tayari. hebu liunge. . .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Boflo alikuwa mjanja wa town si akampitisha katavi kwenye uchochoro, waka muibia kila alicho kuwa nacho, cha kushangaza Boflo yeye hakuuibiwa chocho kila mtu alijiuliza je Boflo ndio alihusika na wizi ule na ilikuwaje yeye hakuguswa?
   
 18. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa hakujua aanze vipi kumtafuta ndugu yake,
  Katavi alikubali kwenda nyumbani kwao Preta.
  Preta alikuwa akiishi na mdogo wake wa kiume aliyeitwa Filipo..
  Preta alimkaribisha Katavi kwa ukarimu sana Kama ndugu yake,Katavi alifurahi sana, maana alioga,alikula na kuangalia tv..
  Alipoanza kusinzia Preta alimwambia mdogo wake Filipo ampeleke Katavi chumbani akalale.
  Filipo alichukia maana alikuwa na ratiba ya kumvusha charming lady usiku huo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Thread ikikamilika story inaunganishwa pamoja ili iwe mtiririko mzuri
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Ilipo fika mishale ya saa4 usiku charmglady alijiweka tayari kumsubili filipo lakini mida ili zidi kusonga bila Filipo kutokea, ndipo charmglady alipo shika simu ili kumtafuta Filipo ili kujua kulikoni. Alipo piga simu tu charmglady alianza kwa kuongea...........ooooooh baby wangu mbona kimya? kumbe simu ilipokelewa na mdogo wake wa kiume Filipo aliye julikana kwa jina la St.paka mweusi lakini chamglady hakujua kama alikuwa akiongea na mtu mwingine tofauti lakini kwa upande wa St paka mweusi(mdogo wa filipo) alijua alikuwa ana ongea na shemeji yake ndipo St.paka mweusi alipo mjibu charm glady kuwa kuanzia leo mimi nawewe basi, wala sikutaki nenda hukohuko kwa Arusha one, charmglady aliendelea kulalamika ooooh nimefanya nini baby wangu, baby ni samehe
   
Loading...