Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Hajajibu hata moja wao hadi leo,hawa yawezekana ni marobot au Zombies.Tumeshuhudia mengi waliyoyanena na leo wanayapinga.Jambo moja la dhahiri hilo ni kundi ndani ya idara za CCM.

Wajibu wapi ndugu yangu?

Kuna na huyu ndugu yetu hapa KeyserSoze asipoangalia atajikuta nao baba mmoja baba mmoja.

Pathetic:

Kuachiwa Mbowe Mbowe na Wenzake, Tanzania imeshinda

Walikuwapo mapandikizi kina Katambi, Slaa, Waitara, Mollel, Silinde, Mashinji nk sembuse nani au KeyserSoze na fake ID?
 
Mkuu hivi unayajua kuwa:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Bado unadhani hayo ni ya bavicha tu na kuwa wao hata hawayajui hayo?

Bado hudhani kuwa yote ya namna hiyo yanapaswa kupatiwa ufumbuzi pasipo na kuchelewa sasa, kwa kuyashughulikia ipasavyo kwenye katiba mpya?
Hata ya chadema iko hivohivo. Karekebisheni kwanza ya chadema halafu mje sasa turekebishe ya taifa.
 
Hata ya chadema iko hivohivo. Karekebisheni kwanza ya chadema halafu mje sasa turekebishe ya taifa.

Hii ndiyo ya msingi zaidi.

Kumwua nyoka si unapiga kichwa, si mkia?

Kukata mti si unakomaa na shina, si matawi?

Kwanini kutuchagulia pa kuanzia? Hii si sawa na mhalifu kujichagulia hukumu?
 
@brazaj Mkuu kuniweka kwenye huo mlengo ulinionea sana Mkuu, yawezekana nikawa na mawazo tofauti lakini si kutaka jambo baya lolote limkute mtu.

Kubadilisha mawazo tunaposafiri inaruhusiwa mkuu.

Si unajua hakuna rafiki wa kudumu wala adui ila agenda?

Tuungane kukataa wahuni.

Katiba mpya ni sasa.
 
Hii ndiyo ya msingi zaidi.

Kumwua nyoka si unapiga kichwa, si mkia?

Kukata mtu si unakomaa na shina, si matawi?

Kwanini kutuchagulia pa kuanzia? Hii si sawa na mhalifu kujichagulia hukumu?
Dah!! Nimemchomoa nyoka pangoni.
 
Dah!! Nimemchomoa nyoka pangoni.

Una maana huyu nyoka anaye haha kutusambaratisha kama taifa hata ikibidi kwa kumkana Nyerere na kuji ndugunize na Iddi Amini?

IMG_20220411_085136_045.jpg


Kwa hakika huyo nyoka ni wewe na nduguzo akiwamo huyu Otterhound.
 
Namna pekee ya kupony majeraha tuliyo nayo ni serikali kuchukua hatua za kuchunguza na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wote waliohusika na matendo ya mauaji na uvunjaji wa haki za binaadamu kipindi cha magufuri.

CHADEMA wasije kubali maneno yasiyo na nyama mpaka hatua hizo zimechukuliwa na wale waliohusika kupewa adhabu stahiki.
Point 📌🔨
 
Namna pekee ya kupony majeraha tuliyo nayo ni serikali kuchukua hatua za kuchunguza na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wote waliohusika na matendo ya mauaji na uvunjaji wa haki za binaadamu kipindi cha magufuri.

CHADEMA wasije kubali maneno yasiyo na nyama mpaka hatua hizo zimechukuliwa na wale waliohusika kupewa adhabu stahiki.

Mdogo mdogo tutafika tu.

Habari hii iwafikie Zitto na nduguze ACT Wazalendo.
 
Hii ndiyo ya msingi zaidi.

Kumwua nyoka si unapiga kichwa, si mkia?

Kukata mtu si unakomaa na shina, si matawi?

Kwanini kutuchagulia pa kuanzia? Hii si sawa na mhalifu kujichagulia hukumu?

Chadema mkipewa nchi watu watakufa njaa,, moshi tu imewashinda, hata kahama imewapita mbali sana kimaendeleo, yumkini hata majengo. Hampaswi kushika dola.

Olenimala faza?
 
Kutofautiana kimawazo katika nchi ni jambo la afya. Haiwezekani sote tukawa na mtizamo mmoja. Hata watoto mapacha hutokea wakati wakatofautiana.

Kwa bahati mbaya kuna zama zimepita kwa kutofautiana tu pana watu wamekufa, wamepotezwa, wamejeruhiwa, wamedhulumiwa, na mengi ya namna hiyo.

Yaliyopita si ndwele bali kiungwana hayawezi kuachwa kuwa ndiyo ilikuwa malipo stahiki kwa wahanga wale.

Mungu bariki tumepata rubani mpya mwenye kuthamimi maridhiano kwa maneno na kwa vitendo. Rubani aliyedhamiria kutuleta pamoja. Makundi yote kwa ujumla yanamkubali na sasa taifa linakuja pamoja.

Hata hivyo kuna wanaoonekana kutopendezwa na hali hii yenye matumaini mapya. Wao wamedhamiria kwa hali na mali kutusambaratisha.

Hawalali. Kila uchao wanakuja na kila aina ya chokochoko, uzandiki, fitna, uongo, uzushi, na vya namna hiyo. Alimradi tu kututatiza sisi kama wananchi na pia kumtatiza mama.

Wanahangaika mno kuzitatiza agenda zake ikiwamo hata kujaribu kumfarakanisha tu kwa lolote na kwa yeyote.

Haieleweki hasa wanataka nini au hawataki nini. Haijulikani pia kuwa, hii ni kwa maslahi gani hasa.

Watu hawa wapo pia humu JF. Mada zao na mabandiko yao mbalimbali yakiwatambulisha hivyo.

Hii nchi ni ya watanzania wote, ambamo kuna wanachama wa vyama vyote wakiwamo pia wasiokuwa na vyama.

"Hivi wandugu, mkiwamo nyie akina Elitwege, Wakudadavuwa, Nigrastratatract, johnthebaptist, Idugunde, Mulokozijr12 na wenzenu wengine ambao kila uchao ni kutafuta fursa za kupalilia utengano tu, mna madhumuni au maslahi gani hasa?"

Hivi wandugu, "Kwa nini mmedhamiria yasiwepo maridhiano kabisa? Kwa nini ni nia yenu kuona watanzania hawa wakiwamo wa CCM na wa CHADEMA haitokei kabisa nafasi ya kukaribiana? Madhumuni yenu ni nini hasa?"

Hatuwezi sote kupigia chapuo kuwa na taifa lenye ustawi, haki na usawa kwa maslahi yetu, wanetu na hata kwa watoto wa watoto wetu?

Tuwakaribishe ndugu hawa kutusaidia kuwaelewa. Labda wakijieleza wenyewe tutawaelewa. Isije kuwa kila mtu labda ana mshangaa mwenziwe.
Porojo za mitandaoni ni tofauti na uhalisia mitaani,watu tunaishi kitaa ambako mambo ni shwari.
 
Back
Top Bottom