Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Bavicha hao wanaotaka katiba mpya ikiwa ya zamani hawaijui
Agano jipya lilikuja baada ya watu wote kulielewa agano la kale?

Ccm wanajua katiba mpya ni kama VAR ya uchaguzi, hivyo wanapata hofu ya ajabu wakisikia katiba maana wanajua mifumo ikiimarishwa ya mapungufu ya Katiba ya sasa, huo utakuwa mwisho wao. Hawapimi ukweli/ubora wa kitakacholetwa na katiba hiyo, wanaangalia ni kwa jinsi gani itakuwa ngumu kwao kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Namna nyingine ya pekee ya kuponya majeraha ni kufanya uchunguzi wa ninj kilipelekea kifo cha JPM, hasa kuangazia ni nani hasa wa walitumika kama link ili kumfikia na kumsababishia madhara.

Ushahidi wa kimazingira wa sera za mama za hivi karibuni (kuhusu Corona, kuhusu mradi wa Bagamoyo, kauli zake tata kuhusu uchimbaji wa madini, n.k) unatia shaka sana.

Hatuna sababu zozote za chuki. Haipo dhana bora kuliko maridhiano katika mambo yote. Haki sawa kwa wote ndiyo ulio msingi mzima.

Kama JPM alikufa kwa Corona ukweli na ukawekwe wazi ili kutokuaminiana kuishe. Vivyo hivyo kama ni mchezo mchafu.

Maridhiano ni pamoja na ukweli na uwazi katika mambo yote.

IMG_20210627_154154_315.jpg


Msingi wa mada ni umoja wetu kuhusiana na hawa magwiji wa mifarakano.
 
Namna nyingine ya pekee ya kuponya majeraha ni kufanya uchunguzi wa ninj kilipelekea kifo cha JPM, hasa kuangazia ni nani hasa wa walitumika kama link ili kumfikia na kumsababishia madhara.

Ushahidi wa kimazingira wa sera za mama za hivi karibuni (kuhusu Corona, kuhusu mradi wa Bagamoyo, kauli zake tata kuhusu uchimbaji wa madini, n.k) unatia shaka sana.
Magufuri si waliishasema alifariki kwa matatizo ya moyo ambayo alikuwa nayo muda mrefu?
 
Pana agenda za fitna kupalilia mifarakano. Dhidi ya watu na hata dhidi ya mama:

View attachment 1832223e
Nyie nao acheni tabia za ma concubines wa magufuri, walianza hivi hivi tukawachekea chekea mpaka wakaaribu kabisa akili za magufuri.
Huyo mama aache kupapasa papasa mambo.

Mpaka sasa sijaona jambo lolote alilofanya zaidi ya kuongea ongea tena kwa kujicontradict kwa viwango vya magufuri pia.
 
Sorry mkuu, nje ya mada kidogo: vipi kuhusu Corona. Unazungumziaje kuhusu Corona Tanzania!

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app

Karibu, jisikie uko nyumbani na hasa ukitujuza nia hasa ya wenzetu hawa kuhaha namna hii kutusambaratisha kama taifa, itapendeza zaidi.

Ukinihitaji kwenye mambo mengine nyeti yenye kutishia uhai wetu kama taifa, kama ilivyo kwa Corona, karibia huku:

Rais Samia, hatua zaidi zinahitajika kukabiliana na COVID-19

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Kutofautiana kimawazo katika nchi ni jambo la afya. Haiwezekani sote tukawa na mtizamo mmoja. Hata watoto mapacha hutokea wakati wakatofautiana.

Kwa bahati mbaya kuna zama zimepita kwa kutofautiana tu pana watu wamekufa, wamepotezwa, wamejeruhiwa, wamedhulumiwa, na mengi ya namna hiyo.

Yaliyopita si ndwele bali kiungwana hayawezi kuachwa kuwa ndiyo ilikuwa malipo stahiki kwa wahanga wale.

Mungu bariki tumepata rubani mpya mwenye kuthamimi maridhiano kwa maneno na kwa vitendo. Rubani aliyedhamiria kutuleta pamoja. Makundi yote kwa ujumla yanamkubali na sasa taifa linakuja pamoja.

Hata hivyo kuna wanaoonekana kutopendezwa na hali hii yenye matumaini mapya. Wao wamedhamiria kwa hali na mali kutusambaratisha.

Hawalali. Kila uchao wanakuja na kila aina ya chokochoko, uzandiki, fitna, uongo, uzushi, na vya namna hiyo. Alimradi tu kututatiza sisi kama wananchi na pia kumtatiza mama.

Wanahangaika mno kuzitatiza agenda zake ikiwamo hata kujaribu kumfarakanisha tu kwa lolote na kwa yeyote.

Haieleweki hasa wanataka nini au hawataki nini. Haijulikani pia kuwa, hii ni kwa maslahi gani hasa.

Watu hawa wapo pia humu JF. Mada zao na mabandiko yao mbalimbali yakiwatambulisha hivyo.

Hii nchi ni ya watanzania wote, ambamo kuna wanachama wa vyama vyote wakiwamo pia wasiokuwa na vyama.

"Hivi wandugu, mkiwamo nyie akina Elitwege, Wakudadavuwa, Nigrastratatract, johnthebaptist, Idugunde na wenzenu wengine ambao kila uchao ni kutafuta fursa za kupalilia utengano tu, mna madhumuni au maslahi gani hasa?"

Hivi wandugu, "Kwa nini mmedhamiria yasiwepo maridhiano kabisa? Kwa nini ni nia yenu kuona watanzania hawa wakiwamo wa CCM na wa CHADEMA haitokei kabisa nafasi ya kukaribiana? Madhumuni yenu ni nini hasa?"

Hatuwezi sote kupigia chapuo kuwa na taifa lenye ustawi, haki na usawa kwa maslahi yetu sote, wanetu na hata kwa watoto wa watoto wetu?

Tuwakaribishe ndugu hawa kutusaidia kuwaelewa. Labda wakijieleza wenyewe tutawaelewa. Isije kuwa kila mtu labda ana mshangaa mwenziwe.

1624824402182.png
 

Sijatambua picha hizi zinahusika vipi na mada iliyopo mezani yenye kuhitaji ufafanuzi tu kwenye maswali yaliyo wazi:

IMG_20210627_231833_595.jpg


Waona je kama tukijikita kwenye mada?

Kama vipi ukafunguliwa uzi mwingine kuhusiana na haya yako yaliyo nje mno ya mada?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Watu wenyewe ndiyo kama hawa:

IMG_20220216_212136_442.jpg


IMG_20220216_214602_969.jpg


Usoni kama watu!
 
Back
Top Bottom