frema120
JF-Expert Member
- Jan 1, 2012
- 5,098
- 1,341
Mkuu mbwa ukishamjua jina hasumbui.
Duh! hii ni tamasali ya neno, nahau au tasititi mkuu.
Mkuu mbwa ukishamjua jina hasumbui.
Mkuu, Nduka, ulikuwa mtu sahihi kuweka taarifa ya akaunti za baadhi ya wajumbe kucheka, lakini ghafla umekuwa mtu asiye sahihi kuweka copy ya transaction licha ya kuahidiwa ushirikiano na mwenye hayo malipo! Naanza kupata smell fulani hapa!
Asante Nduka kwa kutujuza.Wanademokrasia na wananchi kwa ujumla!
Kuna mipango miovu inayopangwa na wahafidhina na wasioitakia mema nchi yetu kuwazuia wajumbe halali wa baraza kuu CHADEMA kuhudhuria mkutano wa baraza kuu hapo Julai 18. Mipango hii inahusisha kuweka vikwazo vya fedha kwa wajumbe hasa masharti ya kuwarejeshea wajumbe posho ya usafiri na kujikimu kipindi chote mkutano. Hii inatishia afya ya demokrasia kwani wajumbe waliopangwa tayari akaunti zimecheka na wengine wameanza kujisogeza eneo la tukio.
Hivyo basi mnaombwa kuwasaidia wajumbe kwenye maeneo yenu kwa michango ili waweze kuhudhuria mkutano huu muhimu unaokwenda kuibadilisha historia ya nchi hii. Kwa wajumbe wa baraza kuu walioathirika na unyanyasaji huu mnaombwa kutoa taarifa zenu hapa ili wana JF wawasaidie.
Nduka,
Kwanza,hicho kikao/mkutano wa Baraza Kuu Tarehe 18 July umetangazwa na nani na wapi?
-Ajenda ni zipi?
Hakuna malipo yoyote ambayo yamefanyika kwa mujibu wa maelezo ya idara ya Fedha ya chama.
Sasa ili uaminike,na pia katika kulinda hadhi na heshima ya JF na wasomaji wake naomba
1:Utuletee vocha za malipo hayo hapa.
2:Orodhesha majina ya hao wajumbe waliolipwa na ambao hawajalipwa
Vinginevyo itabidi upuuzwe kwa kiwango kinachostahili na pia JF ifuate sheria na kanuni zake
CHADEMA kinafanya kazi zake kwa uwazi katika kukuza demokrasia na kupigania uhuru wa kweli.
Kamwe kelele na hila za maadui wa mabadiliko hazitatutoa nje ya mstari.Mapambano yanaendelea.
Hatutegemei mfurahi mkiumbuliwa kwa mipango miovu sasa unataka kujifanya unajua kila linalo endelea chadema! Chadema wenyewe hawawezi kukuamini kukwambia kila jambo! Acheni kulilia na mods!POMPO,
Tuebdelee kupambana makamanda hakuna jambo jema walilofanya JF kama hili la kuacha uzi huu wa uzushi,uongo na unaovunja kanuni zao walizojiwekea.Wamejianika wazi wazi..!Kumbe humu habari zozote za uongo zinaruhusiwa. Motto wetu umebadilika na kuwa "Where we dare to lie Openly"?
Mkuu Nduka endelea kutujuza huyu Ben hajuI kuwa wezi kushirikishwa kwenye kila kitu maana anaonekana Kama msaliti na haaminiki kabisa.Mkuu reaction yako kwenye juu UONGO ndio hasa punchline ya stori yenyewe. Endelea kutest my patient ili nifanye nisichotaka kufanya. Be warned tunataarifa za kutosha kuhusu mpango huu. Najua hujui kwanini siku hizi umekuwa sidelined kwenye hii mipango nitakufahamisha pia.
Hahahaha naona una lialia tuu!Hawa wachumia tumbo ni wanafiki sana .Leo tumeaaibisha sana na imesaidia pia kujua JF ilivyo na hila.Siku hizi hatutakiwi kuwa wastaarabu tena na kufuata kanuni humu mana kila tukifuata kanuni wao wanaziacha zivunjwe.Hatutavumilia tena .Tutashinda hata iweje.Hakuna kurudi nyuma
Matokeo ya kukariri kila jambo bila kushirikisha akili.Mkuu Nduka endelea kutujuza huyu Ben hajuI kuwa wezi kushirikishwa kwenye kila kitu maana anaonekana Kama msaliti na haaminiki kabisa.
Acha umbea kijana unapaswa kujitambua na ujue katika maisha yako unasimamia nini,Sio kuendeshwa na mihemko ya Lumumba,Huna namba ya Mnyika nikupe umuulize?
Mkuu wana taka wakimjua wampige tofali Kama Mwigamba.acha kulialia kwa mods wewe. Una wasiwasi gani kama unasema kuwa taarifa hii si ya kweli? Halafu, una dhamira gani ya kutaka jina na namba ya uanachama ya mwanachama aliyefichua uozo huu? Ben, si kila kitu ni cha kupinga. Mengine unapaswa kutazama kwa jicho la kiuchunguzi zaidi
Mkuu wana taka wakimjua wampige tofali Kama Mwigamba.
Nduka ni mzalendo amefichua maovu.
hakika Mkuu. Mbowe anadhani kuwa atatawala milele
Nduka,
Umeleta tuhuma hapa JF na ukaomba wanaJF wasaidie.Ukarusha tuhuma za uongo.
Sasa uliposema yupo tayari kutoa ushirikiano halafu unasema atapeleka kwenye vikao vya chama una maana gani?Kwanini ulileta huku at first place kama ulijua kuna taratibu za vikao?
Mnatunga uongo kwa kushirikiana na wasaliti wa mabadiliko halafu mnaweka huku.JF inakaa kimya.
Nawashauri wasomaji wa Jukwaa hili wakupuuze sasa na JF ikuchukulie hatua kama nao hawanufaiki na uongo wako huu ili kulinda hadhi yetu sisi wasomaji na wachangiaji wa jukwaa hili na JF kwa ujumla.
Hatutegemei mfurahi mkiumbuliwa kwa mipango miovu sasa unataka kujifanya unajua kila linalo endelea chadema! Chadema wenyewe hawawezi kukuamini kukwambia kila jambo! Acheni kulilia na mods!