Tuwalipe vizuri Wafanyakazi wa majumbani mwetu

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Wana jamvi habari za usiku huu,

Leo nimeona nilete hii habari kwenu, najua fika kwa wengi wenu sio habari mpya na kwa wengine na habari mpya kabisa.

Na kuna wengine habari hii sio mpya ila wamejisahau kiasi kwamba wanabana na kuvunja sheria na taratibu zilizowekwa na serikali kuhusu kima cha chini cha mshahara cha wafanyakazi sekta binafsi.

Msisitizo wangu mkubwa upo kwa wafanyakazi wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa sana kwetu katika kuangalia familia zetu, mali zetu na vingine vya thamani.

Hivyo basi ni muhimu kuwalipa vizuri ili wafanye kazi zao kwa uaminifu mkubwa na kuendelea kutuhudumia vizuri.

Tusiwadhulumu kwakua wengi wanafanya kazi hizi kwasababu mbalimbali za kimasha.

Naomba kuwasilisha.🙏

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…