Bima ya Afya kwa wafanyakazi wa viwandani iwe lazima kisheria

NEWSINKP

Member
Sep 26, 2016
77
92
Habari wana JF!

Ndugu zangu nimefanya kazi katika baadhi ya viwanda mkoa wa Pwani nimegundua wapo Watanzania wanafanyakazi maeneo hatarishi sana.

Ndugu zangu kama mnavyojua viwandani kuna kemikali na emissions nyingi mno. Ingawa kwenye sheria zetu kuna taratibu nyingi zimewekwa kwa ajili ya kuwalinda wafanyakazi ila hizi taratibu hazifuatwi na wamiliki hatimae kila siku watu wanapata majeraha na kuugua vifua.

Ndugu zangu wapo watu nimafanya nao kazi mpaka wamepata vilema makazini ila matibabu ni juu yao, unachopewa ni sick sheet ila garama ni juu yako.

Nimeshuhudia watu wa serikali ambao ndio walipaswa kutembelea na kukagua hata kwa kushtukiza ila wanapiga simu na kuwapa taarifa wamiliki ili hiyo siku wakifika kila kitu wakute sawa ila ni uozo mtupu.

Na cha kushangaza hivi viwanda havitoi Bima ya afya kwa wafanyakazi wake! Sote tunatambua unapozungumzia kiwanda kuna mitambo, kuna kila aina ya emissions na ndio maana haviwagi karibu na maeneo ya makazi ya watu. Wafanyakazi wanapata hadi ukiziwi viwandani.

Bima ya afya iwe ya lazima kwa wafanyakazi wa viwandani. Najua humu kuna hadi wabunge, please pelekeni kawekeni hii kitu kwenye sheria za kazi kabsaa. Watanzania wanateseka mnoo, mi nimeshuhudia kila siku kwenye kiwanda chenye wafanyakazi 150, kila siku wafanyakazi zaidi ya 20 wanaenda hospitali tena kwa garama zao na mishahara ni laki moja na 70 kwa mwezi.

Kuna jamaa alikatwa kidole akajitibu mwenyewe na kwakua waliona aibu wakampa cheo cha usimamizi ila hela ya kujitibu alitafuta kwa kuomba omba mitaani.

Tafadhali mawaziri wa afya na wa kazi wasaidieni hawa watanzania wanateseka sana huko viwandani.
 
Back
Top Bottom