DOKEZO DAWASA inatesa Wafanyakazi wa mikataba, haifuati sheria wala taratibu za Utumishi katika stahiki zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TOG

New Member
Nov 24, 2022
4
4
Habari za mda huu,

Tunapenda kutoa Malalamiko yetu sisi wafanyakazi na viongozi wa wafanyakazi, (sababu hatuna sehemu ya kwenda kusemea, kwani kila sehemu DAWASA imeweka mkono wake na kuzuia sauti zetu).

DAWASA, shirika la Maji Dar es Salaam na Pwani. Ni shirika lililo chini ya Serikali kupitia Wizara ya Maji, ikiongozwa na Jumaa H. Aweso. Ni shirika ambalo linatakiwa kufuata taratibu za KIUTUMISHI wa SERIKALI.

Hivyo, Shirika hili kama mashirika Mengine, DAWASA imekuwa ikiajili Wafanyakazi wa Mikataba kwa kuwapatia Mikataba ya muda mrefu kama Mwaka mmoja au Miaka miwili, kisha kuwaajiri kabisa wafanyakazi kwa Kuwapa Permanent Employment kama taratibu za kitumishi zinavyosema.

Lakini shirika hili, limekuwa likiwatumikisha na kuwatesa Wafanyakazi hao wa Mikataba, kwa mateso makubwa, huku wakitishiwa kuwa watafukuzwa kazi pindi watakapo lalamika, au kusikika wakilalamika.

Wafanyakazi hao wa Mikataba sasa hivi wanakaribia elfu moja, huku wengi wao wamekuwa wakifanya kazi ya mkataba kwa zaidi ya miaka minne, huku wengine wakifanya hadi zaidi ya Miaka Mitano, yaaani five Years.

DAWASA imekuwa ikiongozwa na aliyekuwa CEO, Eng. CYPRIAN LUHEMEJA, ambaye kwa sasa hivi ni NAIBU KATIBU MKUU Wizara ya Maji.

Ni CEO aliyekua akiendesha Shirika kwa Mabavu saana, akitesa wafanyakazi, huku akijihusisha na kutafuta sifa saana kwa wanasiasa wakiwemo Wabunge...bila kujali maslahi ya wafanyakazii wa shirika la DAWASA. Hadi ikapelekea kuvunja taratibu za Utumishi, na kuzorota kwa Maslahi ya wafanyakazi wa DAWASA wakiwemo wa Mikataba.

Eng. CYPRIAN Luhemeja, amewatesa saana Wafanyakazi wa Dawasa, huku akitumia Vyombo vya Habari kujisifia, kujisafisha na kuwafanya wananchi waone kama Dawasa ni shirika Kuubwa sana na, lenye Viwango, na lenye Uwezo mzuri kuliko mashirika Mengine. Kitu ambacho SIO KWELI.

Dawasa Imekua ikiwafanyisha kazi wafanyakazi wa Mikataba kwa zaidi ya Miaka MITANO, huku wakiwaahidi (Eng. Cyprian Luhemeja) kuwa atakuja kuwaajiri pale Mwaka wa Fedha utakapoanza, lakini hafanyi hivyo, na kuwatishia kuwa akisikia wanalalamika, basi kibarua chao kitaota nyasi.

Wafanyakazi hawa wa Mikataba wengi wameshafanyishwa INTERVIEW, tangu mwaka Jana May 2022. Lakini mpaka Leo July 2023, hamna maendeleo yoyote ya kuwaajiri Permanently na kuwapa Stahiki zao kama Sheria na Taratibu za Utumishi zinavyolezea.

Eng. Cypriam Luhemeja, alisema na kuwaahidi kuwa Kibali cha kuwaajiri kipo katika Ofisi ya Rais (Kwa Katibu Mkuu Kiongozi), alisema hivyo tangu January 2023 katika Mkutano wetu wa Viongozi wa Wafanyakazi.

Lakini kiuhalisia, jambo hilo lilikuwa ni UWONGO MTUPU, na ilikuwa anawahadaa Viongozi hao kwa kusema Uwongo. Hasa kusingizia ishu Serious kama hiyo kwa Rais wa Tanzania.

Vile vile, katika kikao chetu kingine pamoja na wafanyakazi kazi Woote mwezi April 2023.

Eng. Cyprian Luhemeja na CEO wa Dawasa wa Sasa alihaidi kuwa Kibali hicho cha Ajira kitatoka katika Ofisi ya Rais hadi ifikapo mwezi June 2023.

Lakini Hadi leo Hiii, jambo hilo halijatekelezwa. Na tukifuatilia sisi viongozi wa wafanyakazi tunaambiwa kuwa, Kibali hicho hakipo katika Ofisi ya Raisi, wala hakipo Utumishi, wala hakipo kwa Katibu Mkuu Kiongozi...!! NI UWONGO, UWONGO, UWONGO MTUPU. Na NI UONEVU MKUBWA SAANA KWA VIJANA HAO WA MIKATABA.

Swari la Msingi Ni, Je Kibali hicho cha Ajira kipo wapi? NA KIPO KWA NANI HASWAA!!?

Kwanini BOARD YA WAKURUGENZI WA DAWASA wapo KIMYA?

Je, Board hiyo nayo Imenyamazishwa? Je, haina Nguvu tena?

Je, inajali Maslahi ya Wafanyakazii wake? Haswa wa Mikataba?

TAFADHALI, TUNAOMBA MSAADA MATHIBUTI na WA DHARURA KUHUSIANA JAMBO HILI KWA HAWA VIJANA WETU WA MIKATABA.

KWANI VIJANA HAWA NDIO DRIVING WORKFORCE, kwa kuwa wanafanyakazi saana kwa kujitolea, kwa manyanyaso, kwa Pressure. Bila kupata STAHIKI ZAO HALALI kama WAAJIRIWA WA SERIKALI.

SISI VIONGOZI WA WAFANYAKAZI TUMEKUWA TUKISEMELEA JAMBO HILI, BILA KUPATA SULUHU YOYOTE. kwani TUMEKUWA TUKIDANGANYWA NA SISI PIA.

DAWASA INAHITAJI MSAADA WA DHARURA KWA KWERI. MAMLAKA HUSIKA ILIANGARIE HILI KWA JICHO LA UMAKINI.
 
Bora ulalamike na kufukuzwa kazi utakuwa sadaka Kwa wengine kuliko kukaa kimya unagunia gumia
 
Nyie wa mikataba ndio mnaokujaga kukata maji bila huruma. Kitu kidogo tunawaambia tunalipia bill nyie hamsikii. Ila kwakua mkikata kurudisha kuna pesa mnapata hamtaki kusikia. Endeleeni kuteseka.

Pili, kwanini kama umamblame Eng. C. L wakati ameshahama, si mnaongozwa na K. Kingu?
 
Pole sio DAWASA Pekee hii Hali ipo sehemu nyingi Tu,

Aisee ukiwa kibarua kweny mashirika ya serikali hamna rangi utaacha kuona,

Kikubwa ni uvumilivu na kuona namna gani ya kujinasua maana mbaya zaidi maslahi ni madogo.
 
Back
Top Bottom