Tuwafahamu wajumbe wa Task Force ya Msajili

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,227
35,151
Itakuwa ni kujidanganya mchana kweupe, kudhani kuwa hali ya kisiasa nchini ni shwari na kuwa kazi inaendelea.

Taarifa rasmi kutokea katika mkutano huo wa kusaka tahfifu katika siasa kwa wadau ni kama ilivyo hapa chini:

IMG_20211226_051830_336.jpg

IMG_20211226_051406_601.jpg

IMG_20211226_051343_468.jpg


Hiyo ndiyo habari yenyewe.

Kama vipi kuwafahamu wajumbe hawa zaidi majina ikiwamo wasifu, mafungamano yao kisiasa, kuaminika katika jamii, vigezo vya kuwamo, nk ingependeza zaidi.

Tukawe na Christmas njema yenye tafakari ya yaliyo mema kwa taifa letu.
 
Itakuwa ni kujidanganya mchana kweupe kuwa hali ya kisiasa nchini ni shwari na kuwa kazi inaendelea.

Kufuatia mkutano wa Msajili na wadau wa Siasa kuna habari ya timu (Task Force) ya watu 10 kufanikisha kufikiwa kwa maazimio takriban 80 yaliyoafikiwa kama ilivyoripotiwa.

Fahari ya macho haifilisi duka. Si haba kuwafahamu wajumbe wa tume hii ili kuendelea kufahamiana zaidi katikati ya sintofahamu zilizopo.

Kama vipi kuwafahamu wajumbe majina, wasifu, mafungamano yao kisiasa, nk, ingependeza zaidi.

Inasemekana kuwa katika timu hii, waheshimiwa hawa wamo:

(a) Profesa Rwekaza Mukandara (REDET)
(b) Dean Fupe (KKKT)
(c) Sheikh Alhad Mussa (BAKWATA)
(d) Dr. Edward Hosea (TLS)

"Lisemwalo lipo kama halipo waungwana wanasema linakuja nyuma."

Kongole kwao.

Kwamba watu hao 10 ni kutokea kwenye mchanganuo huu:

1. Mwandishi wa habari........Pascal Mayala
2. Jaji mstaafu..........
3. Mwanaharakati nguli.......Cyprian Musiba
4. Kiongozi wa dini (Mkristo).........Gwajima
5. Kiongozi wa dini (Muislam) ....Sheikh wa dar
6. Kiongozi mstaafu (chama cha upinzani)....Dk Slaa
7. Kiongozi mstaafu (chama tawala)....Wasira
8. Mhadhiri vyuo kikuu...Bana
9. Mkulima.....Aliyegombea urais CCM 2015
10. Mjasiriamali.......Mange

Timu haitakuwa tofauti sana na hiyo, Majina yanaweza badilika lakini tabia za wajumbe zitafanana na za hap.

NADHANI KUNA NAMNA CCM WANATUONA WABONGO MISUKULE.
 
Tungekuwa na umoja wakujadiliana vipaumbele vya Nchi na siyo vipaumbele vya kila anaeingia kukalia kiti kubwa nakuvishwa mamlaka
 
Tungekuwa na umoja wakujadiliana vipaumbele vya Nchi na siyo vipaumbele vya kila anaeingia kukalia kiti kubwa nakuvishwa mamlaka

Vikwazo ni viroboto, wahuni na matapeli waliojaa upande wa pili
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya.

Hiki kinachoitwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.

Kwa kweli wanatuona mazuzu kweri kweri:

".. ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!"

Tume huru na katiba mpya ni kwa mujibu wa matakwa ya wananchi wanaoathirika na utawala madarakani.

Utawala uliopo hauwezi kutoa suluhu ya uozo huu yenyewe.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom