Tutoe ushauri kulingana na mada husika

Tunakukomaza kwa namna mbalimbali ili uwe makini, mstahimilivu na jasiri katikati kupambana na hali zote.

Yes humu kuna wataalamu wa kila aina bana kila ubandikacho humu hiyo comment unayoiona ni ya mtaalamu wa eneo husika, iwe tusi,kejeli n.k

vumilia kupitia comment zote hadi ukutane na ya mtaalamu wa shida yako, wenzio wametusua kupitia humu shauri yako.....
 
1. Ukishatoa Jambo lako Mbele ya jamii huku mitandaoni ambapo hakuna Ndugu zako, hawakufahamu, moja ya vitu unavyotakiwa kuvitarajia ni pamoja na hayo uliyoeleza.

2. Kama hautaki, ni Bora ukauliza Mzazi wako, wenyeviti wa ukoo wenu, Mzee wa kanisa au sheikhe wa msikiti, Mjumbe au mwenyekiwa mtaa wako. Au Rafiki zako. Kama hao wameshindwa basi huku mtandaoni sio sehemu ya kuitegemea Sana kukupa Maoni ya kukudekeza dekeza.

3. Alafu Kwa mwanaume Kupata changamoto kama hizo ni ishu ndogo Mno ambayo haipaswi kumuumiza, angalau Mwanamke akilalamika kwani Wana mioyo laini.

Hii ni jamiii, wapo wenye busara na wasio na busara.
Wapo wenye matatizo makubwa na wenye matatizo madogo.
 
Ni kweli kuna baadhi ya wajumbe badala ya kutoa ushauri watatoa kejeli kwa sababu ni sehemu ambayo wengine wanatoa machungu waliyobeba. Lkn wale wanaotoa ushauri kwa kupitia mifano yao,,huwa inatoa nafasi kwa kujifunza na kujua kumbe inawezekana maana watu wanapitia experience mbalimbalia hata kama wewe hautapitia lakin ni sehemu mojawapo ya kujifunza.

Kuna kipindi nilikuwa nafanya mafunzo kwa vitendo ktk ofisi moja ya ushauri nasaha. Sasa kila siku alipokuja cliet yule mkuu wa pale akawa anatoa historia tofauti. Zilipopita siku chache nikajiuliza mbona kila siku anahistoria mpya ina maana maisha yote haya magumu kayapitia? Ikabidi nimuulize alichojibu ni sehemu ya kumfanya mtu ajisikie vizuri,,,na kubadili mtazamo kwa kile anachoamini.

Kikubwa ni kubeba yale watu wanayokushauri wenye kukejeli unaacha na kejeli,,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama mbinguni tu shetani alileta mambo yake ambayo n nje ya mada, itakuwa humu JF ambako kuna wal3 ambao mungu aliwataja kwamba n dhaifu??

Anyway, ushauri wa watu mbalimbali sometimes huwa kama mchanga, maji na cement kwenye mahitaji ya TOFALI. Yote huwa yana umuhimu wake ila hujaamua kuuona.

Tambua kwamba PUMBA kwa mwanadamu ni uchafu, ila pumba hizo hizo kwa bata na kuku ni PILAU. Hivyo ukishauriwa pumba wew jaribu kuwa kuku, na ukishauriwa mahindi rudi kuwa binadamu that simple.

Watu dhaifu siku zote hupanic kwenye mambo madogo madogo, be strong.

Alamsiki[emoji3578][emoji3578]
 
huo ndio ubinadamu,hayakwepeki hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…