Tutazunguka sana, ila ukweli umefichwa hapa

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Sijui nisalimie vipi! Anyway niende madani.

Tutazunguka sana, sana, sana, sana, sana! Ila huwezi kujenga ghorofa kwa kutegemea kuuza karanga kwa faida ya 500 kwa siku. Huwezi, huwezi, huwezi. Kuna siri!

Kwanza kabisa jua kuwa ni nani mmiliki wa mali na utajiri vya dunia hii? Ni watu wachache.
Na si hivyo tu, vizuri karibu vyote vipo miongoni mwa wachache.

Ukweli mchungu ni kuwa, malalamiko ya raia kuwa maisha ni magumu yapo toka enzi na enzi na hayatokwisha. Kila siku watu wanalalamika maisha ni magumu, hakuna siku wakasema ni rahisi.

Baada ya tafakari nzito nimebaini kuwa, huwezi kuubadilisha mfumo. Huwezi kuutikisa mbuyu, utaishia kutikisa makalio yako.

Wachache wajanja ndiyo wanaofaidi maisha popote, siku zote. Masikini hawatokuja kwisha, ugumu wa maisha na malalamiko hayatokuja kwisha.

Usiwe miongoni mwa wengi, pambana uwe mmoja wa wachache niliowataja hapo juu. Mfumo ndiyo unataka hivyo.

Dawa na mzizi wa kuua yote ni kuwa mmoja wao, yaani miongoni mwa wachache wanaofaidi raha. Mfumo ndiyo upo hivyo tangu enzi za Yesu.

Cha kwanza kabla hujaanza mapambano yoyote maishani, pambana KWANZA uijue siri ya ULIMWENGU.

Lazima uifahamu siri ili usiwe mtumwa TENA, na uujue na kuuishi uhalisia uliokuwa huufahamu kwa miaka mingi.

Usipambane kuuza mkaa wala karanga wala chochote kile ili uwe tajiri, pambana UIJUE SIRI kwanza.

Ukitaka karanga zikupe ghorofa basi usikazane kuuza karanga, pambana UIJUE SIRI.

NB: Na ukiijua kaa kimya, usiropoke.

Haya, wa kung'amua ang'amue!.
 
Siri ni kufanya yasiyompendeza Mungu ndiyo yatakufanya uwe tajiri! Unashindwa kumsoma jamaa anakupa siri ya mchezo wa matajiri wengi hapa Duniani!!
Mkuu kwa nini umekwenda direct sana? Kwa nini kila kitu kizuri kinapatikana kwa kutompendeza Mungu at large %? Kwa nini kila kitu kizuri kiko very limited kwa wachache na si wengi?
 
Back
Top Bottom