Tutazikumbuka tozo, ni suala la muda

Tutazikumbuka tozo, ni suala la muda

Sio kweli.. Tozo zinaua uchumi…
Usiwadanganye watu
Tozo ni wizi period
Kodi tunalipa why tulipe mara kumi?
Yes tozo zinaua uchumi, kila tozo zinapokatwa ninapunguza mzunguko wa pesa mtaani.
Hizo zinarudi hazina kwa njia ya tozo zinaliwa na watu wachache na wengine kuzipeleka nje kwa mabenk au kuzurura kama wanavyozurura
 
Tanzania hapa 65-70% ya wakaazi wanaishi Vijijini..

Huko Mjini kama Dar kuna bandari na airport ndio zinaingiza Pesa zaidi Wala sio maskini wa Dar..

Jasho la wanavijiji linajenga Mjini.
Haijalishi asilimia ngapi wanaishi wapi, mjini ndio sehemu kwenye mapato makubwa duniani hili hali hitaji shule mkuu
 
Sio kweli kwamba tozo hazikuwa na faida kwa maendeleo ya Mwananchi wa chini.

Na sio kweli nchi yetu inajitosheleza kimapato kiasi cha kuona tozo haina msaada wowote kwenye maendeleo.

Navyofahamu tozo ilikuwa inatoa nafasi kwa watanzania wengi kuchangia maendeleo yao.

Sasa wameondoa tozo, naamini mzigo tuliokuwa tunauona kwenye tozo kuna sehemu tutaenda kuulipa kwa gharama.

Ni suala la muda tu.........

Sent using Jamii Forums mobile app
Hazijaondolewa
 
Tungeweka nguvu kupinga hizi hanasa lakini sio kuondoa tozo
Kwanini wasingeanza kwanza na kuondoa hizo anasa na kupunguza ufisadi kisha ndio wakaleta hizo tozo? Yani katikati ya sifa mbaya ya ufisadi uliyokithiri pamoja na matumizi mabaya halafu hapo hapo serikali inaleta kodi na kutaka wananchi kuwa wazalendo?

Bila hizo tozo tu watu walikuwa wanalalamika hali kuwa ngumu bidhaa zimepanda bei,cha ajabu kipindi hicho hicho ndio serikali imeona ndio muda sahihi wa kuleta tozo huku ikiwa wao wenyewe wameshindwa kuonesha matumizi sahihi ya kodi za wananchi.
 
Nilichokigundua Watanzania wengi hatupendi kuchangia maendeleo yetu, tunaona ni jukumu la serikali kutufanyia kila kitu. Hata ukiundwa mfumo shirikishi mwingine wa wananchi kuchangia maendeleo mbali na tozo kwa misukumo yetu ya kisiasa tutaita ni unyonyaji.

Tusiishi kwa kusema kuwa nchi yetu ina rasilimali nyingi bila kujata rasilmali muhimu pia ni mwananchi. Sasa rasilimali isiyochangia kitu na ya kwanza kulalamika inapokutana na huduma mbovu ni hasara mara mbili kwa taifa.
 
Kabla ya hizo tozo hicho kilichokuwa kinapatikana ni hicho hicho kilitumika kufanya maendeleo, wajanja kukwapua, pamoja na kugharamia maisha ya kifahari ya viongozi.
 
Hebu Watanzania tuanze kupanga mambo yetu kwa ajili ya wakati ujao ( Let's live for the future and not for the current).

Hivi mnavyokomalia ishu za tozo, ndiyo kusema kweli hii nchi haina rasilimali zingine zozote zinazoweza kuendesha serikali na wananchi wake? Kweli?

Huwa tunaambiwa na kuona kwamba, hii nchi ni tajiri wa rasilimali mfano mbuga za wanyama, ardhi ya kilimo, madini, nk. Kwanini tozo tu kwenye mitandao ya simu na benki? Kwa nini siyo kilimo cha mbegu za mafuta ya kupikia na pamba kwa ajili ya nguo?

Binafsi naona, ni muda umefika CCM waachie hii nchi mana mbinu zao zote zimefeli, wamebaki kumkandamiza mwananchi wa chini.
 
Tozo ni daylight robbery.

Hakuna mwananchi asiyechangia maendeleo ya nchi.

Kuna Direct tax na Indirect Tax.

Matumizi mabaya ya serikali ndiyo maana wanaona kodi haiwatoshi.

Haiwezekani ununue vx(v8 ,v12) za milioni 400 kwa RC,DC,DED,RAC,DAS,RAS,W,NW,KM ,K,DED(wa kila Taasisi)(Hapo unapata V8 ngapi kwa nchi nzima?) ,Bado warsha,semina,makongamano,per diem,maintance ya maV8 yote nchi nzima ,wese ,Vitafunio,chai etc

Mishahara mikubwa sana kwa wabunge,wakurugenzi wa taasis,posho,safari etc

Hayo ni matumizi mabaya ya fedha.

1.9T had 2.x T zinatosha sana kufanya mambo makubwa tukiacha matumizi ya anasa.
 
Sio kweli kwamba tozo hazikuwa na faida kwa maendeleo ya Mwananchi wa chini.

Na sio kweli nchi yetu inajitosheleza kimapato kiasi cha kuona tozo haina msaada wowote kwenye maendeleo.

Navyofahamu tozo ilikuwa inatoa nafasi kwa watanzania wengi kuchangia maendeleo yao.

Sasa wameondoa tozo, naamini mzigo tuliokuwa tunauona kwenye tozo kuna sehemu tutaenda kuulipa kwa gharama.

Ni suala la muda tu.........

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni Mwigulu? Kwa nn utumie hela za tozo kujinunulia Gari la milioni 500?
 
Sio kweli kwamba tozo hazikuwa na faida kwa maendeleo ya Mwananchi wa chini.

Na sio kweli nchi yetu inajitosheleza kimapato kiasi cha kuona tozo haina msaada wowote kwenye maendeleo.

Navyofahamu tozo ilikuwa inatoa nafasi kwa watanzania wengi kuchangia maendeleo yao.

Sasa wameondoa tozo, naamini mzigo tuliokuwa tunauona kwenye tozo kuna sehemu tutaenda kuulipa kwa gharama.

Ni suala la muda tu.........

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamelilia kuondolewa kwa tozo, tujiandae kisaikolojia kwa kinachofuata ITV......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom