Tutashinda Corona kwa Maombi? Hatua za kufuata...

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Modes naomba miufute huu uzi wala kuunganisha kama itawapendeza

Imani zetu zinamtaja MUNGU kama wa pekee, asiyebadilika wala kufafanishwa. Mungu alivyotuumba alitupa utashi ambao ndio kitu pengine cha kipekee kinachotutofautisha na wanyama na viumbe wengine.

Ukisoma Biblia Takatifu, 2 Wafalme 7:3-20 kile kisa maarufu sana cha Watu wanne wenye Ukoma ambao waliamua kwenda kwenye kambi ya adui maana walijua wazi, hawa watu ni adui zetu siku zote, twendeni tukaombe chakula, walijisemea wenyewe kwa wenyewe kuwa TUKIBAKI HAPA TUTAKUFA, na tukienda tutakufa tu! Kwakua waliamua kuchukua HATUA ndipo Mwenyezi MUNGU akatenda Muujiza, kwenye kambi ya adui walivyosikia vishindo wakajua Wana wa Israel wanakuja kuwamaliza, wakaacha kila kitu wakakimbia, jamaa wakaingia kambini wakala wakashiba na wakaenda kuwaita na Utawala wao unaweza kuendelea kusoma.

Nashauri, kwakuwa hawa Wazungu ( Mabeberu ni maadui zetu siku zote) twendeni tu tukapate chanjo, tukibaki tutakufa na tukienda tutakufa tu! Acha twende huenda MUNGU atabariki hatua tunazochukua kuliko kukaa na kuzika kimyakimya, tumepewa akili tuzitumie.

Vivyo hivyo, MUSA kama anavyotajwa kwenye vitabu vya dini alifika mahali akaona hakuna njia ya kwenda, alipoona mbele kuna maji na nyuma kuna jeshi la Farao, hakumuomba MUNGU ashuke pale awabebe, bali alimjulisha MUNGU na MUNGU akamuuliza Musa una nini mkononi? Pengine swali hili leo tungeweza kusema Una wataalam wangapi na wa nini? Watumie hao. Musa alitumia fimbo sio maombi ya kufunga tatu kavu, akayapiga maji yakatawanyika, alitumia akili na maarifa na akachukua hatua! Hakubweteka kwakua ameshamlilia MUNGU.

Visa vingine vinavyothibitisha haya ni pamoja na hivi hapa Mungu hakumjengea Nuhu safina bali Nuhu alitumia akili akiongozwa na nguvu za kiungu katika ujenzi wa Safina, Samson hakumuomba MUNGU ashuke aonekane pale ili alipe kisasi, bali alimuomba MUNGU amlipie kisasi kwa kumrudishia Samson nguvu zake kwa wakati ule ili aweze kulipa kisasi kwa ajili ya macho yake mawili.

Ndugu zangu, ningeweza kuendelea na mifano kedekede ya namna na jinisi MUNGU anavyotenda kazi na miujiza kwa namna yake, kwa bahati mbaya sana sana MUNGU hashurutishwi na wala hapangiwi deadline, na huwa anabaki kuwa MUNGU hata pale asipojibu kwa style ile tunayotaka. Miujiza yote na matendo yote makuu kwenye vitabu vya dni iliyotokea, inayofahamia sana na isiyofahamika au isiyo na umaarufu LAZIMA kulikua na vitu viwili Kulikua na Kusikiliza sauti ya MUNGU (sauti ya wengi na sauti ya MUNGU) na kulikua na kuchukua HATUA.

Wafalme wa kwenye vitabu vya dini, walitumia njia hii sana, waliwaita Makuhani wao, pengine kwa Nyakati hizi tungeweza kusema (Wana sayansi wetu) na kuwauliza jambo kisha Wafalme hawa wangetekeleza sio kwa matakwa yao ila kwa muongozo wa Makuhani hao. Haijawahi kutokea Mfalme akaota maono yeye mwenyewe, akajiuliza yeye mwenyewe, akajipa majibu yeye mwenyewe na akatekeleza yeye mwenyewe.

Kama Tanzania tumeamua kumgeukia MUNGU katika hili la Corona basi tukumbuke kuna Principles zake. Tuzitumie hizo na sio kutafuta upenhyo wa kukwepa wajibu wetu kwa MUNGU, Tutakufa kama Wajinga.
 
Back
Top Bottom