rosita
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 510
- 471
Kuna watu wamezaliwa na tabia ambazo kwa ulimwengu wa leo watapata shida sana
Hapa nawazungumzia wale ambao wamezaliwa huku wakiwa hawawezi kabisa ku-cheat lakini wakati huohuo hawawezi kuhimili mwenza wao kuwasaliti
Hili ni suala gumu sana
Binafsi nilishawahi kujaribu kulifikiria hili nikajikuta nashindwa kabisa,siwezi kutofautisha kumdharau mpenzi wangu na kum-cheat
Yaani siwezi kum-cheat halafu niendelee kujidai eti nampenda
Ni ngumu
Nahisi kujidhalilisha na zaidi sana namdhalilisha mwenza wangu
Nahisi maisha yatakuwa magumu sana kwenye dunia hii ya "cheating is inevitable"
Nawaona wake za watu mitaani wanavypishana kwenye nyumba za wenyeji[sio wageni]
Najaribu kuvivaa viatu vya waume zao nahisi uchungu sana
Na hata wale wenzangu wenye mtazamo huu nawaambieni tutaipata tu kwenye maisha haya
Au tuamue kuachana kabisa na hii kitu?
Tutaoa kweli?
Mimi nimeamua tu kubaki naangalia kwanza!
Maisha ya kuigiza ni magumu sana!
Wanaume wasiopenda kucheat kumbe bado mpo....dah atajayekupata atakuwa na bahati sana.