Tutafakari juu ya gharama hizi za Harusi

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Ndungu wana jamvi habari za asubuhi, ni matumaini yangu kuwa mmeamka salama na mnendelea na shughuli zenu za kulijenga taifa.

Hebu tutafakari juu gharama tunazochangia katika sherehe za harusi ambazo zimekuwa zikipanda kila siku.

Tunachangia gharama hizi kubwa sana ambazo mwisho wake wanaonufaika ni wamiliki wa kumbi. Wanaoweka mapambo wapishi ma MC na usafiri n.k.

Huku walengwa yaani bibi na bwana harusi hubaki hawa na zawadi yeyote au watapewa zawadi ya kamati kiasi kidogo sana.

Tubadilikeni tuache tabia hii ambayo kwa sasa imekuwa ndiyo utamaduni wetu kama hujamfanyia kijana wako sherehe hizi basi kwa sasa utaonekana huna maana.
Kwa fano mkichanga sh.million 20 basi gharama ukumbi million 3 chakula million 12 mapambo million 2 na kadhalika.

Pesa hizi zikichangwa wapewe bwana na bibi harusi ili wakaanze maisha.

Ndoa kamili hufanyika kanisani au msikitini haya mambo ya kwenye kumbi ni kupoteza pesa muda na kujifakhirisha.

Tubadilikine najua watakuja hapa watu wanaonufaika na biashara hizi kupinga lakini ukweli unabaki palepale.
 
Kuna ka ukweli kidogo, maana wengine wanakopa ili wafunge ndoa huku wakiwa wamepanga kama ni hivyo bora gharama iwe ndogo ili kuwasaidia maarusi.
Kama vipi waache waoane, na,kupanga ni kuchagua
 
Kuna ka ukweli kidogo, maana wengine wanakopa ili wafunge ndoa huku wakiwa wamepanga kama ni hivyo bora gharama iwe ndogo ili kuwasaidia maarusi.
Kama vipi waache waoane, na,kupanga ni kuchagua
Maana hizi gharama wananufaika wengine badala ya wahusika
 
Ndo maana wale wengine wamefanya rambirambi mradi.Sijui kwa nini hawaoni hili wamkamate mwenyekiti wamkamate mwenyekiti wa kamati ya harusi halafu hela ziende kwenye miradi
 
siku hizi tumestukaaa...michango yote tunashikilia walengwa wa sherehe..mfano harusi ndugu na jamaa marafiki watachngia but michango anaeka bwana hausi bank..mnampa mahitaji ye anawasilisha pesa
me wakitaka kunifanyia send off ntashikilia mwenyewe hela
 
wanawake ndio wanasababisha huu ujinga usiishe... kuanzia mama, dada, shangazi, mke mtarajiwa wote wanataka kuserebuka
 
siku hizi tumestukaaa...michango yote tunashikilia walengwa wa sherehe..mfano harusi ndugu na jamaa marafiki watachngia but michango anaeka bwana hausi bank..mnampa mahitaji ye anawasilisha pesa
me wakitaka kunifanyia send off ntashikilia mwenyewe hela
Duh
 
Kuna bwana harusi alitokomea na pesa za michango pamoja na mchumba wake,

Baadae akatuma taarifa wapo Kenya, ndoa wameshafunga.

Kamati ikabaki mikono kichwani.
 
Nyie mtakuwa merongwa. Huu uzi unaonekana km kituko tu. Nyie ndiyo wala rambi rambi
Comment zenu zinaonesha mnaupungufu wa akili. Km meweza kuongea kuwa harusi ziwe zinakatwa kodi ni sawa na rambi rambi kwenda kukarabati hospital.
Ujinga sana huu. Haujalazimishwa kufunga ndoa. Wenye vipesa vya mawazo ndiyo huwa wanaropoka ropoka.
 
Hayo ya gharama mnayataka wenyewe,kwa waislamu hakuna hiyo,barazani tu harusi inafanyika,ikianza saa saba mpaka saa tisa,kama hakijatokea kitu,kila mtu kwake, na maharusi kwao.
Nani kakudanganya mkuu?labda hao ni waislamu wa huku kwetu Rufiji,lkn waislamu wa mjini wote wameshabadilishwa mindset na wakristu,hii ni aibu,waislamu nao siku hizi wanaenda na mtindo huohuo wa kuchangishana then baadae ukumbini kama kawa!Utamaduni mbaya kabisa huu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom