kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,006
Napendekeza Serikali ianze kuangalia suala la kodi kwenye harusi.
Binafsi kwa mwaka nachangia karibu laki sita kwenye shughuli za sherehe za harusi. Huko nakunywa soda zisizozidi 6 na maji madogo 6 pamoja na chakula ambacho nikiagiza hotelini hakizidi sh.elfu 60 yaani milo sita.
Sasa ukiangalia pesa nyingi inaenda wapi?
Kuna wanaokunywa bia hao ndio wanakunywa angalau vinywaji vingi.Pia gharama za kumbi,keki na mapambo kwa ujumla.
Hivi vyote ni anasa tu ni tofauti sana na suala kama kutuma pesa.Unaweza kuwa unamtumia mtu mwenye shida sana mfano ugonjwa n.k.
Serikali ingeweka kikokotoo kama cha kununua gari kwenye hizi arusi. Maana watu huchanga kama wana wazimu na hawaoni uchungu kutoa pesa hizo.
Watu wenye kumbi nao kutokana na uchache wa kumbi wanatoza gharama kubwa sana kwa sherehe ya siku moja.
Serikali ingeweka utaratibu kuwe na risiti za efd kwa anayechanga ili iambatanishwe na kadi yake ya arusi.Na waweke mtu wao pale mlangoni wanapoingia ili akague kila mtu awe na risiti.
Ni mawazo yangu tu