Tusubiri singo ya muasi Kubenea kesho

ndutu

Member
Mar 22, 2011
90
15
Ni masaa machache tu yamebaki kabla ya singo nyingine ya Saed Kubenea na Mwanahalisi kuingia mtaani, kama kawaida singo hiyo itasheheni maneno ya kashfa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na familia yake. Wakati singo hiyo ikitoka, kwa maelekezo ya waajiri wake wapya aliopingana nao sana kabla ya kusalimu amri, inatarajiwa pia kwamba atakuwa anaendelea na majukumu yake mapya ya kumtakasa Edward Lowassa na wafuasi wake wa ufisadi.

Kwa hakika sasa hivi ile jumatano ambayo ilikuwa iisubiriwa na watanzania wengi kwa hamasa na kiu kubwa kulisubiri gazeti hilo sasa wamehamisha imani yao kwa Raia Mwema.

Karibu kwa mara nyingine bwana Kubenea, utakase unaowatumikia na 'kumuua' mkuu wa nchi na familia yake.
 
Nashukuru kwa kuokoa jero langu kukuchangia wewe, huku mifuko yako ikicheua fedha haramu za mafisadi. Aibu tupu!
 
Huu ni unafiki wa kundi la Sitta kulishambulia mwanahalisi. Kundi hili sasa linatumia Raia mwema kujisafishia njia na hapo hapo kuichafua Chadema.
 
hata mimi slowly naanza kuegemea Raia Mwema kuliko hii kitu ya huyu jamaa Kubenea. Ni kama naelekea shimoni vile, lakini pengine ni kwa sababu amepewa mshiko mrefu na mafisadi. Ila ni suala la muda tu atajua alikosea au la! Tusubiri tuone.
 
Watanzania wanapenda hadithi za uasi ila waliowengi hawajui wala hawezi kuasi. Hivyo MwanaHALISI litaendelea kuuza ilimradi tu waendelee kuandika hadithi za kuchochea uasi, kudhalilisha mamlaka n.k.
 
Umejaliwa upuuzi wa aina yake. Kwa nini usimpigie simu kumueleza haya?
 
2015 linaweza kujiunga na Rai kama gazeti zilipenda lililobaki kuuzwa kwa kugawiwa bure.
 
Hili gazeti nilikua nalifagilia sana hapo nyuma lakini naona sasa hivi Said Kubenea anaanza kupoteza mvuto! Muda si mrefu nitayarudia magazeti ya Shigongo bora nipate habari za akina Lulu/Wema Sepetu na mzee wa Mbagala! Nimechoka na umbea wa siasa.
 
Mbona hamtaji Tazama,Jambo leo,Uhuru,Mzalendo na Hoja kwamba nayo yamenunuliwa na Mafisadi? Kwa vile mwanahalisi halishabikii sera ya kujivua magamba basi lionekane limenunuliwa na mafisadi? Mtapiga propaganda sana lakini zitashindwa.
 
Huwa nafurahi na kuchekelea sana ninaposikia kumbe magamba hawalali usingizi usiku wa Jumanne kuamkia jumatano! Hongera Kubenea kwa tabia yako ya kuwasha moto ndani ya chupi za hawa mafisadi wa CCM!
 
...unamtofautishaje unayemtetea hapo juu na Lowassa au Mafisadi kama unavyotaka kutuaminisha.

Acha mbwembwe zako wewe, Kama unayosema unayaamini, basi pia sioni tofauti yako kwa upande moja na ya Kubenea kwa upande mwingine ("Action and Reaction are equal but opposite in reaction ").

Kaka au whatever they call, tunatumia vichwa kufikiri na sio uti wa mgongo na/au masaburi. Hiyo kambi nyingine inayomwona Lowassa mwovu yenyewe ni safi kwa kiwango kipi ndani ya CCCCCM? au basi R1 na Lowassa tofauti yao ni ipi hasa......?

Sawa tuchukulie ww na wenzio nyuma ya pazia mmefanikiwa kutuaminisha ubaya wa Lowassa, sawa nani Mzuri? Migiro yule Rozi? (teh teh teh), Membe?, Mwinyi (Dk) ? Mwandosya? Mwakyembe? Sitta? Pinda? (eee, yeye atalia na wananchi watalia, sijui nani atambembeleza mwenzake)
 
Umejaliwa upuuzi wa aina yake. Kwa nini usimpigie simu kumueleza haya?

Nawewe kwanini unataka ampigie simu?!!!kuna kitu gani ulitaka tusikijue hapa jukwaani?hakuna kupigiana simu kila kitu kiletwe hapa then anaeguswa na kutaka maoni ya mhusika bwana said ampigie yeye,lakini hapa mambo hadharani
 
Watanzania wanapenda hadithi za uasi ila waliowengi hawajui wala hawezi kuasi. Hivyo MwanaHALISI litaendelea kuuza ilimradi tu waendelee kuandika hadithi za kuchochea uasi, kudhalilisha mamlaka n.k.
hivi ni kudhalilishwa au kujidhalilisha?
 
Huwa nafurahi na kuchekelea sana ninaposikia kumbe magamba hawalali usingizi usiku wa Jumanne kuamkia jumatano! Hongera Kubenea kwa tabia yako ya kuwasha moto ndani ya chupi za hawa mafisadi wa CCM!

There you are sir! Salute!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom