Haya mashindano ya Tusker project fame tangu nimeanza kuyafuatilia Watanzania tunafanya vibaya na ni Msechu tuu alijaribu kudogo kutufurahisha Watanzania na sana sana sii kwa kiwango kikubwa saana cha kuimba lakini ni ujanja ,uchangamfu na ucheshi pale anapoona range ya sauti yake haifiki na kufukia mabode either kwa kucheza au kuongea maneno ya vichekesho ambavyo viliweza mpaka kumdatisha Muamuzi nguli na mkorofi Judge Ian
Tatizo la Tanzania ni lipi? Ni vipaji vya kuimba hatuna? Hapana bongo tuna vipaji kibaao, Je ni Lugha ya kiibereza inatubabaisha? Hapana hata kiswahili kule kinakubalika wanachoangalia ni kipaji na ufundi wa kuimba nyimbo za melodia Tofauti.
Nimeshuhudia mashindano ya mwaka huu Uganda wamepeleka vijana wakali woote na ilibidi mpaka waamuzi walipiga kura kuangalia atarudi nani.Ni kitu gani kimesababisha Uganda kuonekana wamepeleka vijana waliojiandaa kiwango kile? Mimi ninadhani yawezekana Juliana anatumia ujuzi wake wa kuwa judge muda mrefu kuangalia ni sifa gani zinahitajika pamoja na kuwanowa ili waendane na viwango.
Lakini Tanzania si alikuwepo mtu anaitwa Holmes ambaye mwaka huu amerithiwa na Mzee Zoro? Yeye alikuwa akirudi nyumbani baada ya mashindano alikuwa anafanya nini ili kuepuka aibu ya wewe mwenyewe kumchagua mtu na kwenye mashindano anaonekana anapwaya?
Nadhani ipo sababu ya msingi ya mashindano haya kuandaliwa vyema kinchi na kutangazwa sio kushtukiza tuu interview Dar es salaam na kudhani kuwa Tanzania ni Dar Peke yake. Experience ya Bongo star search inanionyesha kuwa waimbaji wazuri hutoka nje ya Dar. Mfano mashindano yaliyopita kuna binti mmoja kutoka Zanzibar ana viwango vya kimataifa vya kuimba,wengine ni ndugu mabinti wa pwani wana majina magumu magumu lakini kama hao wakienga wanaweza kuiwakilisha vyema nchi.
Mashindano ya mwaka huu tuwasindikize tuu waganda waliojiandaa vyema nakwa mbali wakenya wachache kwangu binafsi kwa wawakilishi niliowaona wa bongo siwakatishi tamaa ila kwa changamoto iliyopo raud mbili zijazo watakuwa wamerejea nyumbani woote.Tujiande kwa mwakani kwa kutoa matangazo ya kutosha na wadau mbalimbali wanaojua vipaji vya kweli wasaidie kwa hili ili nchi iweze kupata vipaji vya ukweli vya kuwakilisha