Kaisari
JF-Expert Member
- Nov 13, 2012
- 3,636
- 3,046
Wanajamvi,
Ninaomba wahusika wauchukue ushauri wangu juu ya hawa wanaoitwa "wauwaji wa Kibiti" Imekuwa sasa kawaida kupata taarifa kwamba hawa waliouawa ni miongoni mwa genge lile.
Mie naomba kuwapa ushauri kwamba wasiwaue ila wawakamate wakiwa hai kwa faida hizi. Kwanza wakiwakamata watapata nafasi ya kuwauliza na kujua wako wangapi, nia yao ni nini, wamepata wapi ujuzi huo, "mafunzo" hii itakuwa faida sana kuwafahamu hawa na kumaliza kabisa tatizo hili.
Pili kuwauwa hawa jamaa kuna punguza idadi ya watu, hivyo kufanya kupungua nguvukazi ya taifa. Bora hata wakienda magereza watafanya kazi za kuzalisha itakuwa faida kwa taifa.
Mtu akiua na wewe ukamuua basi tunakuwa tumepoteza watu wawili hasara bora yule mmoja aliepotea huyu wapili tumtumie kuzalisha na kule "chuo cha mafunzo" anaweza akajutia kosa lake akawa raia mwema sana akawa balozi mzuri kwa mambo mema.
Tatu tunamnyima haki ya msingi ya kujitetea mahakamani, haki ya kikatiba.
Siku zote mnahubiri tusichukue sheria mkononi kwa maana wafikishwa mahakamani fanyeni basi hili kwa vitendo.
Nawasilisha.