Kwanini hatuna somo la "Siasa ni Wizi" kwenye mitaala yetu?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,181
5,317
Tumekuwa na kasumba ya kuongelea ubovu wa mitaala yetu lakini kuna kitu nahisi huwa tunakisahau.

Leo nipo kijiweni kwangu waliponitimua na nimerudi tena nikimsubiria mkuu wa eneo lake aje tena na vyombo vya habari kusafisha safisha, ghafla namwona mwanangu anarudi toka shuleni kama kawaida amebebelea madaftari yake mkononi.

Kama ilivyo ada ya kizazi cha nyoka, tai shingoni kalegeza suruali kaifungia makalioni anadunda nafikiri ndiye chekibobu wa darasa, nikamwita dogo ebu njoo hapa, leo huko shuleni kulikoni mbona mapema hivi wakati tumezoea siku hizi mnatoka nyumbani usiku nakurudi ni usiku na bado hamjui lolote zaidi ya kufahulishwa.

Dogo ananiambia kuwa huko shuleni kwao kawa suspended kwa wiki mbili na atakaporudi arudi na mzazi sasa sijuhi ni mzazi gani yaani mimi huyu huyu au?

Eti kisa wakati mwalimu alipotaka wanafunzi wampe mifano hai ya viongozi waadilifu na wazalendo wa taifa hili, dogo alisimama na kujibu kuwa taifa hili halijawahi kuwa na viongozi waadilifu na wazalendo wanaostahili heshima yeyote zaidi ya WEZI wanaopaswa kuwa mahakamani kujibu mashtaka ya hasara na umasikini waliolisababishia taifa na watanzania kwa ujumla.

Licha ya usela nondo wa huyu mwanangu (hapa niliona katema point) ambaye shule ataki daily ananisisitiza baba nataka kujiajiri, shuleni sitoambulia chochote maana kazi ni mchongo na haki ya hoe hae ni job applications nakuchangia nauli na accommodations kwa wamiliki wa malazi na usafiri wakiwahi kufanya usahili wa kazi za wengine.

Sasa huwa najiuliza tu hivi huyu anaujua mtaa lakini? Si kheri apoteze sehemu ya maisha yake tu huko shuleni ambako nako atanipotezea rasilimali na muda kuliko huku mtaani ambako atakuja kutundika mimba bila huduma, huo mtaji atautoa wapi ikiwa hata mkopo wenyewe ni mchongo.

Ikiwa watu waliosomeshwa kwa pesa la jasho la wananchi wakufikirika kuwaongoza wengine kupitia migongo ya bloodline za familia zao waliobahatika kuwa viongozi wakubwa wa kufikirika ndo hao hao wanaokesha ughaibuni daily kufukuzia madeni kwa taifa na mikataba isiyo na tija itakuwa mimi pangu pakavu ndo niangaike na kujua namna ya kutumia vyema rasilimali za nchi na kupunguza utegemezi?

Mzazi kwa kuvurugwa nikafunga genge langu la mapera mapema nkarudi home kutafakari kuwa sasa imefikia muda mashuleni mitaala iruhusu somo la SIASA NI WIZI lifundishwe mashuleni na madudu yaliyofanywa na viongozi husika yaanikwe hili wale wanaotarajia kuwa viongozi wa hapo baadae waepuke kurudia kufanya utumbo kama watangulizi wao kwa kujua historia ya kweli na siyo ya ukoloni yakuzugazuga kwenye kimvuli cha akina Mkwawa itawahukumu na siyo kuwatunza kama ilivyo sasa.

Mfano mdogo wa mambo yanayotia hasira kama mzalendo wa taifa la kufikirika na katu uwezi yakuta darasani yakifundishwa ni kama haya:-

Kiongozi awamu ya 2 aliuza lolitondo akisaidiwa na mkewe fisadi na kinara wa utoroshaji madini ya almasi kinyemela kwa kutumia marubani wa shirika la ndege la taifa.

Baadae jamaa mmoja toka hunjoo huko waziri wa mambo ya ndani kipindi hicho machachari akamtia adabu kwa kumkamata uwanja wa ndege red handed huyo mwanamke mwizi ila kwa kuwa bwana mdogo huyu hakujua uwanja anaopaswa kucheza kibarua kiliota majani siku chache baadae.

Akawa rhuksa mno akavuruga uchumi mpaka ikafikia wakati akawa amedondoka wino Lake Vicky na Kilima njeree vipokwe sijuhi aliwaza nini na kama siyo kiongozi wa awamu ya 1 kuzuia sijuhi ingekuwaje. Jamaa nae eti kaacha kizazi chake kinaendeleza alipoishia nacho kinarendemka rendemka ama hakika tutafika mifupa.

Awamu ya 3 nayo ilikuwa funga kazi ikaanzisha WIZI wakutisha kwa jina la ubinafsishaji, akajimilikisha migodi kwa bei ya kutupa(kashfa za merymeita) na mali zingine za umma, mkewe akimiliki zaidi ya tax 5000 katika jiji la sokomoko na wakijimilikisha nyumba za umma za shirika la nyumba la taifa hili viongozi waserikali wakapangishe mtaani, viwanda vikauzwa kwa bei yakutupwa hata vile ambavyo vilikuwa vikijiendesha kwa faida kama breweries.

Akabinafsisha migodi kwa wazungu holela huku yeye akitunukiwa zawadi ya vipande vya tofali,makoleo na vigoda vya dhahabu kila alipotembelea migodi husika. Wakazi wa maeneo husika wakiambulia umasikini wa kutisha nakunywa maji machafu yenye mercury (kashfa ya kule Kaskazini dhidi ya mgodi wa nyamoongoka kuchafua mto maira na wakazi wake kudhurika wakibabuka ngozi ambapo wakili msomi wetu wa ubeligiji ndipo alipopatia umaarufu wake huko)

Wakati huo kiongozi akishauriwa alikuwa mkaidi kama moto, wanakufikirika waliuawa hovyo katika migodi kule marekani ya mkoani manhara na (bulkhanihulu katika awamu ya 4) na serikali ya viongozi hawa ilitetea wazungu badala ya wananchi.

Kuna kisa kimoja cha mkuu wa wilaya mmoja machachari ambaye mwanae aliyerithi mahali pa babaye sasa yupo gerezani huko kufikirika aliuwa wakina mama wajawazito na wanakijiji akiwachomea nyumba na kuwapiga risasi bila huruma mchana kweupe huko nyamumumma na kesi akashinda.

Waziri mkuu wa awamu hiyo aliwahi miliki Hoteli Aracheda halafu akaikana kwa sababu ya mazingira ya rushwa ikafikia akajibinafshia uwanja mdogo wa ndege wa Aracheda kama haitoshi akamiliki akaunti ya trilioni 11 huko nchi za ughaibuni, mkuu wa polisi enzi hizo akawa anamiliki hela chafu mpaka askari polisi asiye na "V" hata moja alikutwa nyakati hizo akiwa na milioni 200 kwenye akaunti yake.

Awamu ya 4 kiongozi akawa kinara wa ujangili akiruhusu tembo wetu wauawe karibia waishe akitunza mashwaiba wake kina yule katibu wa chama chake, waziri mkuu mstaafu awamu ya 3 na wazandiki wenzie, katika nyakati hizi tulishuhudia mengi ikiwemo na yale ya licha ya urefu wa twiga bado alitoroshwa airport na hakuonekana, mbwa mwitu na wanyama wengine waliohatarini kutoweka wakazidi kutoweshwa.

Kiongozi akawa meneja wa hoteli za utalii za kiongozi wa nchi nyingine, bandari ikapigwa vilivyo na kiongozi pamoja na kiongozi mwenzie aliye-finance kwenye uchaguzi, biashara zikamea watu wakajimilikisha miradi ya umeme hewa, biashara ya mafuta,vinara wa biashara haramu za madawa ya kulevya mpaka watoto wao wakadakwa huko uchina wakaishia kuiuza nchi sawa na bure wakisaini mikataba ya ovyo kama ile ya gesi na bandari kama vile wamelala kisa kunusuru uhai wa familia zao na maslahi yao ya 10 percent na siyo taifa.

Kiongozi akakesha sana angani kuliko anavyokaa ikulu, mikataba na viongozi wa serikali yake ikawa inasainiwa hotelini pembeni wakiwa na warembo wao wakishuhudia utiaji saini huo kama yule waziri wa utalii na demu wake miss waliousishwa na kashfa za uporojaji wa mamilioni ya fedha na benki moja ya kigeni nchini, ikaja skendo ya EIPHA, RICHADIMOND,DOAWANSI n.k Kesi zote zikatiwa kapuni au kutafutiwa ufumbuzi mwepesi na hakuna pesa iliyorudi, list is endless.

Sasa Watanzania wenzangu kwa muktadha huu na nyie mwadhani ni busara kama mzazi nirudi kumwombea mwanangu msamaha kwa makosa aliyoyafanya yakuwakosea heshima viongozi wa nchi ya kufikirika kwa kuwaita WEZI hili wamruhusu aendelee na masomo yake?
 
Lipo kwenye uchaguzi mkuu

Mrusi mweusi
Hahahaaa! Mbona hicho kinyago cha uchaguzi siku hizi akiwatishi wachongaji wake cha zaidi wanawatishia watendaji wao kuwanyima ugali na wanapita bila kupingwa kama wananawa vile.
 
Nikiingia kwenye system lazima na mimi niwe mpigaji tu yaani kuangaika kote na cv wanao wanawaingiza kirahisi tu haiwezekani aisee hiyo keki tule wote
 
Nikiingia kwenye system lazima na mimi niwe mpigaji tu yaani kuangaika kote na cv wanao wanawaingiza kirahisi tu haiwezekani aisee hiyo keki tule wote
Pengine huko sahihi kwa maana ya kama mbwai na iwe mbwai ila kwa namna nyingine utokuwa umesolve chochote zaidi ya kufanya ushetani wa maCCM hao nakufanya watu wengi walio masikini zaidi waendelee kuishi kwa shida kisa kukidhi haja za moyo wako.
 
Back
Top Bottom