Nature
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 758
- 2,027
Nimeona mitandaoni hapa nchini kwetu, baadhi ya watu wakitoa maoni yao kuhusu viongozi wa Afrika na usafiri walioutumia walipokuwa wanaelekea eneo la msiba wa Malkia Elizabeth.
Mwanzoni nilifikiri ni Tanzania pekee lakini nimeona hata Kenya nao baadhi ya watu wanasema kwamba viongozi wa Africa wamedharauliwa akiwemo wa Rais William Ruto.
Lakini jambo ambalo watu wengi hawajui ni kwamba kuna viongozi mbalimbali wa zaidi ya mataifa mia moja Duniani na kila kiongozi akiwa na msafara ni gharama kubwa sana. Pia ingelazimu Askari wengi zaidi kuhudumia misafara ya viongozi hao...
Pia viongozi kutoka Asia nao waliwekwa gari la pamoja.
Viongozi kutoka South America nao walikaa gari la pamoja.
Baadhi ya viongozi wa Ulaya pia waliwekwa gari la pamoja
Suala la kila kiongozi kuwa na msafara wake binafsi ni iitu ambacho Serikali ya Uingereza ingekuwa vigumu kulitekeleza ndani ya Muda mfupi. Yangetakiwa yafanyike maandalizi ya miezi mitatu kabla.
Huyu ni Bill Clinton alivyokuja Tanzania akiwa tayari ni Rais mstaafu wa Marekani, alitumia Hiace kama usafiri wake na akaenda nayo mpaka Ikulu na kukutana na Rais Kikwete wakati huo.
Kuna msemo Unasema Maskini akila Dagaa anaambiwa ni kwa sababu hana kitu lakini Tajiri akila Dagaa anaambiwa anaimarisha Afya.
View attachment 2361547
View attachment 2361551