Tusiwalaumu Waingereza kwa Ubaguzi hata Bill Clinton alivyokuja Tanzania alitumia Toyota Hiace kama usafiri wake

Nature

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
761
2,033
Nimeona mitandaoni hapa nchini kwetu, baadhi ya watu wakitoa maoni yao kuhusu viongozi wa Afrika na usafiri walioutumia walipokuwa wanaelekea eneo la msiba wa Malkia Elizabeth.

Mwanzoni nilifikiri ni Tanzania pekee lakini nimeona hata Kenya nao baadhi ya watu wanasema kwamba viongozi wa Africa wamedharauliwa akiwemo wa Rais William Ruto.

Lakini jambo ambalo watu wengi hawajui ni kwamba kuna viongozi mbalimbali wa zaidi ya mataifa mia moja Duniani na kila kiongozi akiwa na msafara ni gharama kubwa sana. Pia ingelazimu Askari wengi zaidi kuhudumia misafara ya viongozi hao...

Pia viongozi kutoka Asia nao waliwekwa gari la pamoja.

Viongozi kutoka South America nao walikaa gari la pamoja.

Baadhi ya viongozi wa Ulaya pia waliwekwa gari la pamoja

Suala la kila kiongozi kuwa na msafara wake binafsi ni iitu ambacho Serikali ya Uingereza ingekuwa vigumu kulitekeleza ndani ya Muda mfupi. Yangetakiwa yafanyike maandalizi ya miezi mitatu kabla.

Huyu ni Bill Clinton alivyokuja Tanzania akiwa tayari ni Rais mstaafu wa Marekani, alitumia Hiace kama usafiri wake na akaenda nayo mpaka Ikulu na kukutana na Rais Kikwete wakati huo.

Kuna msemo Unasema Maskini akila Dagaa anaambiwa ni kwa sababu hana kitu lakini Tajiri akila Dagaa anaambiwa anaimarisha Afya.
C%201.jpg
View attachment 2361547
View attachment 2361551
 
Umeshasema mwenyewe akiwa ni Rais Mstaafu! Na usikute huo msafara wake uliandaliwa na Ubalozi wake wa Marekani!

Au ulitaka na yeye azungushwe na yale Ma V 8 yetu meusi? Wewe kubali tu kilichotokea kwa viongozi wetu ni fedheha! Bora hata wangebaki tu. Iweje akina Biden wapokelewe kwa magari yao maalum!! Ni kwa sababu wao ni wakubwa bila shaka.
 
Umeshasema mwwnyewe akiwa ni Rais Mstaafu! Na usikute huo msafara wake uliandaliwa na Ubalozi wake wa Marekani!

Hakunaga usawa wa kila kitu uweZi mfananisha biden na ruto au Samia yule kiongozi mzito sna super power kwa hyo Ana adhi yake popote pale kuliko na miuzanyiko wa marasi wengine

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Umeshasema mwwnyewe akiwa ni Rais Mstaafu! Na usikute huo msafara wake uliandaliwa na Ubalozi wake wa Marekani!

Au ulitaka na yeye azungushwe na yale Ma V 8 yetu meusi? Wewe kubali tu kilichotokea kwa viongozi wetu ni fedheha! Bora hata wangebaki tu. Iweje akina Biden wapokelewe kwa magari yao maalum!! Ni kwa sababu wao ni wakubwa bila shaka.
Waafrika tunadeka sana wakati mwingine na kila Jambo tunaona kama vile tunabaguliwa...

Hata viongozi wa Asia nao walipakia basi la pamoja...

Halafu kumbuka wameenda msibali na sio kwenye maonyesho ya Misafara.

Viongozi kutoka Asia
JamiiForums-1387784414.jpg
 
Nimeona Mitandaoni hapa nchini kwetu, baadhi ya watu wakitoa maoni yao kuhusu viongozi wa Africa na usafiri walioutumia walipokuwa wanaelekea eneo la msiba wa Malkia Elizabeth.

Mwanzoni nilifikiri ni Tanzania pekee lakini nimeona hata Kenya nao baadhi ya watu wanasema kwamba viongozi wa Africa wamedharauliwa akiwemo wa Rais wao William Ruto

Lakini Jambo ambalo watu wengi hawajui ni kwamba Kuna viongozi mbalimbali wa zaidi ya mataifa mia moja 100 duniani na kila kiongozi akiwa na msafara ni gharama kubwa sana. Pia ingelazimu Askari wengi zaidi kuhudumia misafara ya viongozi hao...

Pia viongozi kutoka Asia nao waliwekwa Gari la Pamoja.

Viongozi kutoka South America nao walikaa gari la pamoja

Baadhi ya viongozi wa Ulaya pia waliwekwa Gari la pamoja

Suala la kila Kiongozi kuwa na msafara wake binafsi ni
Kitu ambacho Serikali ya Uingereza ingekuwa vigumu kulitekeleza ndani ya Muda mfupi. Yangetakiwa yafanyike maandalizi ya miezi mitatu kabla.

Huyu ni Bill clinton Alivyokuja Tanzania akiwa tayari ni rais msataafu wa Marekani, alitumia Hiace kama usafiri wake na akaenda nayo mpaka ikulu na kukutana na Rais Kikwete wakati huo.

Kuna msemo Unasema Maskini akila Dagaa anaambiwa ni kwa sababu hana kitu lakini Tajiri akila Dagaa anaambiwa anaimarisha Afya.View attachment 2361548View attachment 2361547
View attachment 2361551
Futa huu upuuusi acha kutetea ujinga na dharau walizooneshwa viongozi wa nchi maskini
 
Waafrika tunadeka sana wakati mwingine na kila Jambo tunaona kama vile tunabaguliwa...

Hata viongozi wa Asia nao walipakia basi la pamoja...

Halafu kumbuka wameenda msibali na sio kwenye maonyesho ya Misafara.

Viongozi kutoka AsiaView attachment 2361591
Nani kasema wanabaguliwa! Mimi nimeongelea mbwembwe zao wanazo onesha, wawapo katika nchi zao!
 
Umeshasema mwenyewe akiwa ni Rais Mstaafu! Na usikute huo msafara wake uliandaliwa na Ubalozi wake wa Marekani!

Au ulitaka na yeye azungushwe na yale Ma V 8 yetu meusi? Wewe kubali tu kilichotokea kwa viongozi wetu ni fedheha! Bora hata wangebaki tu. Iweje akina Biden wapokelewe kwa magari yao maalum!! Ni kwa sababu wao ni wakubwa bila shaka.
Mi nisingekubali kupanda hayo mabasi
 
Lakini Jambo ambalo watu wengi hawajui ni kwamba Kuna viongozi mbalimbali wa zaidi ya mataifa mia moja 100 duniani na kila kiongozi akiwa na msafara ni gharama kubwa sana. Pia ingelazimu Askari wengi zaidi kuhudumia misafara ya viongozi hao...

Pia viongozi kutoka Asia nao waliwekwa Gari la Pamoja.

Viongozi kutoka South America nao walikaa gari la pamoja

Baadhi ya viongozi wa Ulaya pia waliwekwa Gari la pamoja

Suala la kila Kiongozi kuwa na msafara wake binafsi ni
Kitu ambacho Serikali ya Uingereza ingekuwa vigumu kulitekeleza ndani ya Muda mfupi. Yangetakiwa yafanyike maandalizi ya miezi mitatu kabla.
Mbona hata hapa kwetu kwenye matukio ya kitaifa marais huwa wanapakiwa kwenye coaster zile zinakaa pale makumbusho kwa jamaa wa usalama binafsi sioni tatizo
 
Ukisoma comment ndo utajua akili ya mtu mweusi imeishia wapi.

* Karibu 95% ya viongozi wote duniani hawajaruhusiwa kuwa na convoy, kwa nn minon'gono iwe kwa maraisi wa Africa tu? It's pointless.

*Mawaziri wa kizungu wengi wanapanda economy class kwenye ndege, lakini waafrica wanaosaidiwa mikopo wanapanda business class.

*Viongozi wa kizungu wanaendesha magari ya kawaida sana, ila kiongozi wa kiafrica anayeenda kuomba mkopo wa kujenga matundu ya choo anaenda na gari ya 400M.

*Kwa mlipa kodi wa ulaya, kumwona kiongozi anapanda business class au gari la kifahari la ofisi ni fedheha kubwa sana, lakini mlipa kodi wa kiafrica ambaye ni tegemezi na hana uhakika wa hata mlo mmoja, kumwona kiongozi wake kapandishwa kwenye basi kama viongozi wengine anaona fedheha.

*Waziri au Rais ulaya au marekani utamkuta anaendesha baiskeli na walipakodi hawana issue sababu anaepusha matumizi mabaya, ila Africa viongozi wakiendesha hata bodaboda ni skendo.

*Who will save Africa?
 
Akili za KiAfrica ni za kipumbav na kipuuz + inferiority complex , hao vibwengo na ngozi zao nyeusi kama wamepakwa masizi wanauthamani gani tofauti na wale WA Asia ,South America na Europe ambao kila continent walikuwa grouped kwenye gari moja moja ?
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom