Tusitishane: Hakuna maisha baada ya kifo!

Tusitishane: Hakuna maisha baada ya kifo!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
35,752
Reaction score
86,393
Nijuavyo wapo binadamu baadhi wameyajua matamanio ya binadamu kiujumla!,namaanisha wanajua ubongo wa binadamu unataka kusikia nini..? Unafikiria nini juu ya mambo mtambuka na binadamu anahisia zipi juu ya maisha yake!.

Hilo sijasoma mahali wala mada hii sijasoma mahali bali ni fikra zangu!,na moja ya kumfaulu mwanadamu ni kupitia matamanio yake iwe kihisia au kimwili.(fikiri)
Hayo ni mambo yanayoweza hata kupindisha fikra sahihi na kuleta fikra potofu pandikizi isiyosahihi!.

Sijaona sababu haswa inayowafanya watu wakubaliane kuwa kuna maisha baada ya kifo!!!! Labda ni upofu wangu na ujinga nilionao!

Kwangu kifo na uhai ni kama hali mbili zinazokinzana na Wala sio mabadiliko ya daraja la kutoka uhai huu na kuingia uhai mwengine!. Kama uhai unasifa za kuwa na utendaji kwa maana ya kupumua,kula,kunywa, kutembea n.k Basi kifo ni kinyume chake ambapo kuwa kinyume kunamaana ya kinyume haswa! Kilichokufa hakina fikra,hakili,hakitendi n.k

Kufa ni sawa na kuwa kabla haujazaliwa!.. kabla haujazaliwa hukuwa na fikra,hukuwa chochote hukua wewe unaejihisi hivi sasa,wewe na utambuzi huo ulionao. Baada ya kuzaliwa (kuwa hai) basi umekuwa wewe na kuwa na fikra na utambuzi huo ulionao na wewe kujihisi hivyo unavyojihisi!.. kifo ni hali inayokuja kuharibu hali hiyo,itakuwa hainamaana ya kifo Kama kinachokufa Kama bado kutakuwa na sifa za uhai Kama kufikiri,kutenda n.k

Ulimwengu tuliopo unasifa ya kuharibu na kutengeneza,tupo katika sifa ya vinavyoharibika na pia tupo ktk ulimwengu wa sifa ya vinavyojiripea ktk uharibikaji huo!.. namaanisha ipo namna ya uhai wetu umejitengenezea namna ya kusurvive ktk ulimwengu huu wa kuharibika! Na namna hiyo ni "kuzaliana" hii ndio dhana pekee nayoilewa kama uendelezaji wa uhai ktk ulimwengu!. Nafasi iliyopo ya sisi kuendelea kuishi ni ktk kuzaliana. Kifo ni kama gari la taka linalokuja kukusanya taka zilizopoteza sifa ya kuwa hai!.. ukifa ndio mwisho wa kila kitu kuhusu wewe Ila kuzaa ndio muendelezo wa uhai uliokuwanao wewe.

Niwape hongera kwa wanaojua kucheza na akili ya mwanadamu ili kufanikisha malengo yao ya kuishi vizuri na kuongoza!.

Kila kitu ambacho kinakuja kwenye maisha yako kitakuathiri kutokana na vile unavyokichukulia!. Kila hisia iliyopo mwilini mwako inakazi yake lkn akili ndio inakazi ya kuongoza hisia hizo, so nishauri lako uchague uongozwe na mitikisiko ya hisia au utumie hiyo mitikisiko ya hisia Kama njia ya kubiidisha ubongo wako ufikiri zaidi!.. it's your choice.
 
Umesahau kutupa ushahidi wa haya unayoyasema.
 
Mkuu siujiue uthibitishe andiko lako kama kuna next episode baada ya kufa ama laa mbona jambo jepesi tu hakuna kitu kisicho na mwenyewe katika hii dunia.

Alafu nyinyi ndio mnao tuharibia watoto wetu mnawapa sumu hakuna maisha baada ya kifo hatimae wanaponda raha kupindukia mwisho zinawaua.
 
Mkuu unajifunga sana kwa kutumia akili tu umesema kufa ni kama vile bado hujazaliwa yaani hujui chochote dunia lakini uko tumboni kwa nchi za wenzetu wanakuwa wshatambua kuwa ni mtoto wa kike au kiume then ukazaliwa ukaishi ndo uhai sasa ukafa tena duniani kwa nn usiwe tena mzima na kuishi maisha mengine kama continuation of trend

Yaani tulianza kuwa wafu tukiwa tumboni tukaishi tukafa duniani kwa hyo tunaweza kuwa hai katika maisha mengine full stop epuka kula viporo asubuhi unaleta mawazo mgando hapo nimekujibu kwa fikra kama wewe sio vitabu
 
Nasubiri jibu lake hapa
 
Ukifa na madhambi unatupwa motoni, ushike adabu!! Tuliambiwa na wamisionari! Mtoa mada hebu fikiria kwa makini "Mungu atawatupa watoto wake motoni kweli? " Ni mbinu ili ushike imani yao! Nakuunga mkono, tunapotea na kufutika katika uso wa dunia kama wanyama na mimea. Tafuna mifupa bado meno ipo - aliimba mwanamziki
 
Bandiko lako linaonyesha kuwa wewe sio muumini wa dini yeyote.

Sasa sijui unajihangaisha nini kuanza kuleta mjadala juu ya maisha baada ya kifo.

Suala la maisha baada ya kifo limefungamana na imani (kuamini), kwa sababu ni jambo usiloweza kulitambua kwa kutumia milango ya fahamu.

Na hakuna mafundisho ya dini yaliyoanza kuwaambia watu waamini eti kwa sababu kuna maisha baada ya kifo, bali watu walitakiwa waanze kwa kumuamini mungu halafu katika kumuamini mungu ndio kuna kuamini uwepo wa maisha baada ya kufa, kwa sababu hilo ni katika mafundisho yanayotokana na mungu.

Sasa wewe huamini kama kuna mungu, unadhani utaamini/ kusadikisha khabari zake?

Yaani umeiacha moja halafu unarukia saba, lazma usielewe.

Binafsi huwa nawashangaa watu kama wewe wanapoleta mada za namna hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha baada ya kifo ni hadithi zakufikirika tu

Mara sijui kuna adhabu ya kaburi kuudanganya umma kua malaika anakuja kaburini na mijoka kukupa adhabu eti na watu kweli wanaamini......ni ujinga tu
 
Nijuavyo wapo binadamu baadhi wameyajua matamanio ya binadamu kiujumla!,namaanisha wanajua ubongo wa binadamu unataka kusikia nini..? Unafikiria nini juu ya mambo mtambuka na binadamu anahisia zipi juu ya maisha yake!.

Hilo sijasoma mahali wala mada hii sijasoma mahali bali ni fikra zangu!,na moja ya kumfaulu mwanadamu ni kupitia matamanio yake iwe kihisia au kimwili.(fikiri)
Hayo ni mambo yanayoweza hata kupindisha fikra sahihi na kuleta fikra potofu pandikizi isiyosahihi!.

Sijaona sababu haswa inayowafanya watu wakubaliane kuwa kuna maisha baada ya kifo!!!! Labda ni upofu wangu na ujinga nilionao!

Kwangu kifo na uhai ni kama hali mbili zinazokinzana na Wala sio mabadiliko ya daraja la kutoka uhai huu na kuingia uhai mwengine!. Kama uhai unasifa za kuwa na utendaji kwa maana ya kupumua,kula,kunywa, kutembea n.k Basi kifo ni kinyume chake ambapo kuwa kinyume kunamaana ya kinyume haswa! Kilichokufa hakina fikra,hakili,hakitendi n.k

Kufa ni sawa na kuwa kabla haujazaliwa!.. kabla haujazaliwa hukuwa na fikra,hukuwa chochote hukua wewe unaejihisi hivi sasa,wewe na utambuzi huo ulionao. Baada ya kuzaliwa (kuwa hai) basi umekuwa wewe na kuwa na fikra na utambuzi huo ulionao na wewe kujihisi hivyo unavyojihisi!.. kifo ni hali inayokuja kuharibu hali hiyo,itakuwa hainamaana ya kifo Kama kinachokufa Kama bado kutakuwa na sifa za uhai Kama kufikiri,kutenda n.k

Ulimwengu tuliopo unasifa ya kuharibu na kutengeneza,tupo katika sifa ya vinavyoharibika na pia tupo ktk ulimwengu wa sifa ya vinavyojiripea ktk uharibikaji huo!.. namaanisha ipo namna ya uhai wetu umejitengenezea namna ya kusurvive ktk ulimwengu huu wa kuharibika! Na namna hiyo ni "kuzaliana" hii ndio dhana pekee nayoilewa kama uendelezaji wa uhai ktk ulimwengu!. Nafasi iliyopo ya sisi kuendelea kuishi ni ktk kuzaliana. Kifo ni kama gari la taka linalokuja kukusanya taka zilizopoteza sifa ya kuwa hai!.. ukifa ndio mwisho wa kila kitu kuhusu wewe Ila kuzaa ndio muendelezo wa uhai uliokuwanao wewe.

Niwape hongera kwa wanaojua kucheza na akili ya mwanadamu ili kufanikisha malengo yao ya kuishi vizuri na kuongoza!.

Kila kitu ambacho kinakuja kwenye maisha yako kitakuathiri kutokana na vile unavyokichukulia!. Kila hisia iliyopo mwilini mwako inakazi yake lkn akili ndio inakazi ya kuongoza hisia hizo, so nishauri lako uchague uongozwe na mitikisiko ya hisia au utumie hiyo mitikisiko ya hisia Kama njia ya kubiidisha ubongo wako ufikiri zaidi!.. it's your choice.

mkuu soma hiyo hapo, japo ni ndefu​

Je tunapokufa tunaenda wapi?​

Ukweli wa Biblia
Wengi wanafundisha kwamba, mtu akifa kama ana dhambi roho yake inaenda jehanamu kuteswa, au kama hana dhambi roho yake inaenda mahali peponi (mbinguni), mawazo haya yanaendana pia na fundisho la “Toharani” la Romani Katoliki, ambalo hufundisha kwamba mtu akiwa na dhambi kidogo akifa huenda “toharani” mahali pa mateso ambapo atasafishwa ili aweze kwenda mbinguni.
Uongo huu umewaongoza wengi kufanya ibaada ya wafu, na kuwaombea ndugu zao waliokufa. Je kuna haja ya kumuombea mtu aliyekufa? Je mtu akifa huwa anaenda wapi? Kupata jibu la maswali haya hatupaswi kutegemea mawazo ya mtu, ni lazima tuyaache Maandiko yajibu menyewe kwa maana hayo ni Neno la Mungu Mwenyewe.

Zaburi 6:5 inasema, “Maana mautini hapana kumbukumbu lako: Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?”

Mtu anapokufa hawezi kukumbuka wala kushukuru au kufanya kitu chochote.

Zaburi 88:10-12 “Wafu je! Utawanyia miujiza? Au waliofariki watasimama na kukuhimidi? Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? Miujiza yako itajulikana gizani? Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?”
Hivyo katika kaburi ni sehemu ya “usahaulifu”, “uharibifu” na “gizani”. Mtu aliyekufa hawezi hata kumsifu Bwana.

Zaburi 115:17 “Sio wafu wamsifuo BWANA, Wala wo wote washukao kwenye kimya;”

Sasa kama wafu hawawezi kumsifu Bwana na katika Ufunuo 7:10 tunaona watu waliookolewa “wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Hii inathibitisha kuwa hakuna mtu ye yeyote aliyekufa harafu akaenda mbinguni; maana wafu hawawezi kusifu wala kuongea. Na zaburi 115:17 imeweka wazi kwamba kaburini ni sehemu ya kimya. Na kama mtu akiendelea kufundisha kwamba mtu akifa papo hapo huenda mbinguni au jehanamu, naomba anijibu swali hili Je huko mbinguni, au toharani, au jehanamu anaenda kukaa kimya?
Zaburi 146:4 “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea”
Sasa kama anaurudia udongo na mawazo yake yanapotea, Je tunapaswa kufikiri kuwa mtu aliyekufa anaenda mbinguni au jehanamu au toharani eh?
Muhubiri 9:5,6 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu yao, husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.”
Wazi eh au siyo? Ikiwa wafu hawawezi hata kushiriki au kujua kitu chochote kinchofanyika chini ya jua (duniani), Je kwanini huwa tunasikia baadhi ya wafu akiwemo na bikira Maria wametokea eneo flani? Utakuja kujua huko mbele.
Isaya 38:10,12 “Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu[kabrini]…Nalisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.”
Umeshika hapo? Hapa mfalme Hezekia anasema wazi kwamba atakapokufa hatamwona “BWANA” wala “mwanadamu.” Kwa sababu kanisa lako linakufundisha kwamba ukifa tu, papo hapo unaenda mbinguni au jehanamu, Je hii inamaanisha kwamba mbinguni hautamwona MUNGU? Je haijaandikwa katika Mathayo 5:8 kwamba “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.”? Hivyo mtu akifa haendi mbinguni; kwa maana wafu hawawezi kumuona Mungu. Na pia mtu akifa hawezi kumwona “mwanadamu” hii inamaanisha kwamba mizuka yote inayotokea ya bikira Maria, na wengineo ni uongo; maana wafu hawawezi kuwaona wanadamu.
Isaya 38:18 “Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.”
Ayubu 14:10,12,21 “Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi?…Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa uzingizini…Wanawe hufikilia heshima, wala yeye(maiti) hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao.”
Muhubiri 9:10 “Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu(kabrini) uendako wewe”
Kama tulivyoona, mtu akifa hawezi kusikia, kuona, kuhisi, kufanya kazi, kutembea, wala kufanya kitu cho chote kile. Sasa kama ni hivyo, Je unadhani kwamba mtu mfu ambaye hawezi kuongea, kuona, wala kufanya kitu cho chote awezaje kuwa mbinguni, au toharani, au jehanamu? Je mbinguni, toharani, na jehanamu ni sehemu ambazo watu hawawezi hata kuongea? Kwa hakika HAPANA! Sasa Je mtu akifa kiukweli huenda wapi?
Zaburi 13:3 inasema, “Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.”
Kifo katika Biblia kinafananishwa na “usingizi” mtu akifa ni kama amesinzia kwa sababu zifuatazo; kwanza hajijui, hawezi kuinuka wala hawezi kufanya kitu chochote; pili ipo siku atakayoamuka kutoka usingizini(kifoni) wakati Yesu atakapowafufua wote waovu kwa wema na kuwahukumu kadri ya kila mtu na matendo yake. Kwa hakika, Yesu alithibitisha kuwa kifo ni “usingizi” kwa sababu mtu aliyekufa siku moja ataamuka tena.
Yohana 11:11-14 “Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.”
Hapa Yesu anakiita kifo kuwa ni usingizi, ni kwa sababu Yesu anajua kabisa kuwa wote waliokufa siku moja wataamuka jinsi ile ile kama wewe na mimi tunavyoamuka asubuhi kutoka usingizini. Sababu nyingine ambayo Yesu anakifananisha kifo na usingizi ni kwamba, mtu akifa hajifahamu wala hawezi kufanya kitu chochote kile. Lakini ipo siku ambayo wote waliokufa wataamka kwa ajili ya hukumu, wengine uzima wa milele, na wengine kuharibiwa milele.
Yohana 5:28-29 “Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”
Wale wote waliokufa wamo makaburini wamelala, hawako mbinguni, wala jehanamu, wala toharani. Bali wamelala kaburini wakisubiri hadi Yesu atakapowafufua siku ya mwisho.
Yohana 11:23,24 “Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”
Kwa sababu wengi wanafundisha kwamba mtu akifa papo hapo anaenda mbinguni au toharani, na Yesu alipokuja alifufua wafu wengi, Je hii inamaani Yesu aliwaodoa wale wafu kutoka toharani, jehanamu au mbinguni ambako walienda mara tu walipokufa? Je inawezekanaje mtu ambaye tayari yuko jehanamu au mbinguni afufuliwe tena? Hakuna kitu kama hicho.
Ayubu 14:12 inasema, “Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwawako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.”
Waliokufa wamelala na hawataamka hata Yesu atakapowafufua siku ya mwisho.
1Korintho 15:20-23 “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.”
1Thesalonike 4:14 “Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.”
Wengi wanashindwa kukubaliana na ukweli huu kwamba waliokufa wamelala tu, na kwamba watafufuliwa siku ya mwisho, badala yake wanashikilia mafungu machache ambayo yametafsiriwa vibaya ili kuonyesha kwamba mtu akifa mara moja huenda toharani, au jehanamu, au mbinguni. Ngoja tuangalie mafungu ambayo wameyatafsiri vibaya ili kuthibisha fundisho lao la uongo la toharani.

Je mfano wa Lazaro na tajiri unamaanisha mtu akifa papo hapo anaenda mbinguni, au jehanamu ya moto?​

Luka 16:19-31 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.”
Hapo Yesu alikuwa anaongelea mfano, mfano siku zote hauchukuliwi kwa uhalisia. Mfano hutumika kuashiria kitu kingine tofauti na kitu kinachotamkwa. Marko 4:34 inasema, “wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.” Kama mifano aliyotoa Yesu inapaswa kuchukuliwa kama ilivyo, kwanini Yesu aliwaeleza wanafunzi wake maana ya mifano hizo kwa siri? Hii inaonesha wazi kuwa mifano ni viwakilishi tu vinavyotumika kuwakilisha kitu kingine, na ndio maana ilimbidi Yesu awaeleze wanafunzi wake kwa siri maana ya mifano hiyo.
Kama mtu atauchukulia mfano wa tajiri na Lazaro jinsi kama ulivyo, ili athibitishe kuwa mtu akifa papo hapo anaenda motoni au mbinguni, anatakiwa pia aichukue mifano mingine yote jinsi kama ilivyo. Na hili litakuwa jambo lisilo na maana kwa sababu hata mitume hawakuichukua mifano jinsi kama ilivyo, bali walimuuliza Yesu awaelezee maana yake.
Kwa wale ambao wanauchukulia mfano wa tajiri na Lazalo jinsi kama ulivyo, hebu tulinganishe mifano mingine katika Biblia, kisha tutaona kosa lao li wapi. Kwa mfano unauchukuliaje mfano wa Waamuzi 9:8-15? Ambapo miti ilienda kuutia mti mafuta uwe mfalme juu yao. Je ni nani ambaye alishaona miti ikiongea na kutembea kwenda kuuchagua mti uwe mfalme? Huo ni mfano tu ambao kama ukisoma Waamuzi 9:16-24 utaona ile miti ilikuwa inawakilisha watu halisi. Pia angalia mfano wa magugu na ngano katika Mathayo 13:24-32, Je unauchukulia kiuhalisi mfano huu? Hapana! Yesu aliuelezea mfano huu na ulimaanisha vitu vingine tofauti na magugu na ngano. Hivyo mfano wo wote ule sio wa kuchukulia kama ulivyo, mfano huwakilisha kitu kingine tofauti na kile kilichotamkwa.
Tukirudi katika mfano wetu wa tajiri na Lazaro. Luka 16:12 inasema “Lazaro alipokufa alichukuliwa mpaka kwenye kifua cha Ibrahimu.” Ukweli ni kwamba kwenye kifua cha Ibrahimu siyo sehemu watakayoenda watakatifu, hivyo Yesu alitumia “kifua cha Ibrahimu” kuwakilisha tu “mbinguni”. Pia Luka 16:22-23 inasema, “yule tajiri alikufa akazikwa, na kule kuzimu akainua macho yake akamuona Ibrahimu na Lazaro.” Neno “kuzimu” la kigiriki lililotumika hapo ni “hades”, na la kiebrania ni “sheol” ambayo yote yanamaanisha “kaburi”, hivyo Yesu alitumia neno “kuzimu/kaburi” kuwakilisha jehanamu ya moto. Kifua cha Ibrahimu na kuzimu vyote ni mifano tu ya mbinguni na motoni, na hayapaswi kuchukuliwa kwa uhalisi.
Kanisa la Roma na makanisa ya waprotestanti, yote hutumia mfano wa Lazaro na tajiri kufundisha kwamba mtu akifa papo hapo roho yake inaenda mbinguni au motoni, lakini Luka 16:23 inaonesha yule tajiri akiwa na macho, na hii inaonyesha yule tajiri ana mwili na roho pia. Hata hivyo mtu akifa anazikwa kaburini na kuna ushahidi mwingi kwamba makaburi ya watu waliokufa siku nyingi yalishafunuliwa na miili yao ikaonekana bado ipo pamoja na macho yake, hivyo Je inawezekanaje watu hawa kwamba wameenda mbinguni au jehanamu bila miili yao? Wakati Yesu alionyesha kuwa yule tajiri anayeteseka motoni alikuwa na macho, na mdomo wa kuongelea? Kitu kingine cha kuthibitisha kwamba Yesu alikuwa anaonyesha mfano tu, ni kwamba Ibrahimu alikufa na akazikwa, na sasa yumo kaburini anasubiri ufufuo siku ya mwisho.
Mwanzo 25:8,9 “Irahimu akafariki, naye akafa katika uzee mwema…Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela…”
Yohana 8:52,53 “…Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa?…”
Katika Biblia hakuna mtu ye yote aliyewahi kuzikwa harafu ikasemekana ameenda mbinguni. Enoki alipaa, Musa alikufa akafufuka (Yuda 1:9); na hata hivyo Musa hakuzikwa na mtu ye yote, Eliya alipaa, Yesu alifufuka kwanza ndipo akapaa. Hakuna mtu aliyekufa akazikwa harafu akaenda mbinguni bila kufufuka kwanza. Yesu katika mfano wa tajiri na Lazalo amemtaja Ibrahimu kama mfano tu, kuwakilisha “mbinguni.” na ametaja neno kuzimu/kaburi kuwakilisha “jehanamu ya moto”. Hivyo mfano huo haupaswi kuchukuliwa kiuhalisi; kwa maana kama Yesu angelimaanisha kweli kwamba tajiri alipokufa alienda moja kwa moja motoni, na Lazalo alienda moja kwa moja mbinguni, hii ingemfanya kujichanganya katika maneno yake; kwa maana Lazalo alipokufa, Yesu mwenyewe alisema Lazalo amelala [Yohana 11:11].
Hata hivyo, wakati huo kulikuwa na makundi mawili ya Wayahudi; Mafarisayo, na Masadukayo. Masadukayo hawakuamini kama kuna kiyama (ufufuo), waliamini kuwa mtu akifa moja kwa moja anaenda kwenye kifua cha Ibrahimu au kuzimu, hivyo Yesu alitoa mfano wa Lazaro na tajiri kwa jinsi kama walivyoamini wao wenyewe ili ajaribu kuwavuta na kuwaelekeza warudishe imani yao katika ukweli wa Maandiko, akasema, “Wasipowasikia Musa(torati) na manabii(shuhuda), hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.” Luka 16:31. Yesu alitumia Musa kuashiria sheria/torati, na manabii kuashiria maandiko yote ya manabii/shuhuda. Ni kana kwamba alitaka kuwaambia Wayahudi kwamba kama wasipoweza kuamini na kutii kile kilichoandikwa katika torati ya Musa na katika maandiko ya manabii, hawataweza kuamini hata kama mtu akifufuka kutoka kwa wafu kuja kuwaambia. Ni kana kwamba Yesu alijua pia kuwa katika siku za mbele ingetokea mizuka inayodai kwamba imetoka kwa wafu; kama vile bikra maria na wengine wengi wanaotokea mara kwa mara, na akasema kuwa usipoamini walichokiandika Musa na manabii hiyo mizuka haitakusaidia lolote.
Mfano wa tajiri na Lazaro pia unatuonyesha kuwa ni jinsi gani isivyowezekana kwa mtu kutoka kwa wafu kuja huku duniani kwa walio hai; maana katika mfano Lazaro hakuruhusiwa kabisa kurudi kwa walio hai.

Je fundisho la Toharani ni la kibiblia?​

Kanisa Katoliki hufundisha kuwa mtu akifa katika dhambi anaenda motoni, na mtu akifa katika neema anaenda mbinguni, na mtu akifa na dhambi kidogo anaenda Toharani mahali ambapo anapata mateso kidogo ili kusafishwa aweze kufaa kwenda mbinguni.
Biblia inasema, wote waliokufa wamo makaburini wamelala (Yohana 11:11), na kwamba hawawezi kutoka humo mpaka mwisho wa dunia utakapofika (Ayubu 14:12), na kwamba siku moja Yesu atakuja kuwafufua kwa ajili ya hukumu; waliotenda mema uzima wa milele, na waliotenda maovu mauti ya milele (Yohana 5:28-29). Hivyo hakuna mtu ambaye yuko toharani, na hakuna fungu hata moja katika Biblia linalothibitisha fundisho hilo. Ikiwa hutaweza kuamini kile inachofundisha Biblia tu, kwamba waliokufa wote wamo makaburini wamelala wanasubiri ufufuo, hakuna njia nyingine ya kukufanya uamini ukweli. Yesu alisema usipoamini walichoandika Musa na manabii hautaamini hata kama mtu akitoka kwa wafu kuja kukuelezea (Luka 16:31), na utajikuta umeangukia katika kuamini uongo wa fundisho la toharani ambalo Musa wala manabii hawajawahi hata kulitamka.

Je Luka 23:43 inasema tunapokufa tu tunaenda mbinguni?​

Luka 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.”
Hapo Yesu akiwa karibu kukata roho alimwambia yule mwizi aliyegongelewa msalabani upande wake mmoja kwamba leo hivi(ijumaa) utakuwa nami peponi, lakini siku tatu baadaye akamwambia Maria Magidalene kwamba, “…Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba…” Yohana 20:17. Sasa kwanini Yesu alimwambia yule mwizi kwamba siku hiyo Ijumaa wangeenda mbinguni, lakini siku tatu baadaye(jumapili) anamuambia Maginarene kwamba hajaenda kabisa mbinguni? Baadhi husema Biblia inajichanganya kwa sababu hiyo, lakini hapa Biblia ilithibitisha kwamba mtu akifa haendi popote pale ila anakuwa yumo kabrini tu amelala wala hajitambui; kama Yesu alivyoonesha mfano, alikufa ijumaa lakini jumpili akasema hajaenda mbinguni bado, hii iliweka wazi kabisa kuwa mtu akifa haendi popote ila anakuwa yumo kaburini tu amelala anasubiri ufufuo. Sasa kwanini Yesu alimwambia yule mwizi kwamba “leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”?
Yesu aliposema “leo hivi utakuwa nami peponi” hakumaanisha kwamba “leo kabisa kabisa”, bali alimthibitishia tu yule mwizi kwamba kwa kuwa amemkubali Yesu kama Mwokozi, basi siku ya mwisho atahukumiwa kwa haki kama alivyostahili; kwa mfano Yesu katika Yohana 8:51 alisema, “Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.” Je hapa Yesu alimaanisha kwamba kama mtu akilishika neno lake hatakufa kabisa maisha yake yote milele? Hapana! Ila alimaanisha kuwa kama kama mtu akilishika neno lake ajapokufa bado yu hai; hii ndiyo maana Yesu anakifananisha kifo kama usingizi tu.
Pia 2Kor 6.2 inasema, “…siku ya wokovu ni sasa.” Je hii inamaanisha kwamba sasa watu wameokolewa kabisa? Hapana! Ila inamaanisha sasa ndio wakati wa kumjia Yesu kwa ajili ya wokovu. Hivyo “leo hivi utakuwa nami peponi” haimaanishi “leo kabisa”, bali siku ya mwisho itakapofika.​

Je Muhubiri 12:7 inathibitisha kuwa mtu akifa roho yake inaendelea kuishi?​

Muhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.”
Neno la kiebrania lililotumika hapo kwenye neno “roho” ni “ruach”(“ר֫וּחַ” [roo’-akh]) linalomaanisha “pumzi” au “upepo”. Hivyo Muhubiri 12:7 inasema mtu akifa mwili wake unarudi mavumbini, lakini pumuzi ya uhai inamrudia Mungu aliyeiweka ndani yake tangu mwanzo. Ayubu 27:3 inathibitisha kwa kusema, “(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, Na roho ya Mungu i katika pua yangu😉” Hapa anaonyesha uhai na roho kuwa kitu kimoja katika pua ya mtu. Kuthibitisha ukweli huu zaidi katika Mwanzo 7:22 inasema, “kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.”
Pumzi ya roho ya uhai, hii inamaanisha ni ule uhai alionao mtu ambao ukiondolewa mtu anakufa Yakobo 2:26 inasema, “Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.” Hapa analinganisha kati ya mwili na imani, na roho na matendo, kama mwili bila roho[pumzi ya Mungu] umekufa, vivyo hivyo imani bila mtendo imekufa. Mwanzo 2:7 inaweka wazi ukweli huu.
Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”
Hivyo mtu anapokufa mwili wake huyarudia mavumbi na pumzi ya uhai humrudia Mungu mwenyewe.
Zaburi 146:3-4 inasema, “Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.”
Je umeshika hapo? kwamba pumuzi ya mwanadamu hutoka na kumrudia Mungu kisha mwanamu huyo anapoteza mawazo? Kama anapoteza mawazo hii inathibitisha kuwa mara tu roho imemtoka, mwanadamu anakuwa hajitambui tena kabisa. Hivyo roho inamaanisha pumuzi ambapo Zaburi 146:4 inasema baada ya pumuzi hiyo kumtoka mtu, mawazo pia yamemtoka na hawezi kujitambua tena.​

Je roho iliyomtokea Sauli haithibitishi kuwa mtu akifa roho yake bado inaendelea kuishi?​

1Samweli 28:7,11 “Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori…Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli.”
Wengi hudai kwamba fungu hili linathibitisha kuwa mtu akifa bado anaendelea kuishi eti kwa sababu mwanamke huyo alimpandisha Samweli kutoka kabrini. Ukweli ni kwamba huyo hakuwa Samweli ila lilikuwa ni pepo lilitokea mbele ya Sauli kwa umbo la Samweli. Kwa sababu Sauli alikuwa ameenda kutafuta ushauri kwa mchawi kinyume na amri ya Mungu.
Kumb 18:10 inasema, “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,”
Pia hakuna mchawi, wala mganga, wala shetani mwenye uwezo wa kumfufua Samweli, Biblia inasema ni Yesu pekee aliye na uwezo wa “kufufua na kutoa uhai” (Yohana 11:25). Na sio wachawi au mapepo. Hivyo lilikuwa ni pepo lililochukua sura ya Samweli kisha likatokea mbele ya Sauli, pia pepo hilo lilitoa unabii wa uongo ambao kama angekuwa ni Samweli kweli, au nabii yeyote wa kweli unabii huo ungetimia. Katika 1Samweli 28:19 pepo hilo lilisema, “…hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami;…” Kulingana na ukweli wa Biblia Samweli hakuwa wala hayuko mbinguni, na kwamba alikuwa amelala kaburini anasubiri ufufuo, tena Sauli baada ya kutoka hapo aliendelea na uovu wake dhidi ya Mungu, kama pepo hilo angekuwa ni Samweli kweli angejua kuwa Sauli hakustahili kwenda mbinguni kwa sababu tangu wakati huo aliendelea kumuuzi Mungu. Hilo lilikuwa pepo tu limechukua sura ya Samweli, na kama mtu akisema vinginevyo, nitamuuliza Je anaamini kuwa mchawi au mganga ana uwezo wa kumfufua Samweli?
2Wakorinto 11:14 inasema, “Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.”
Hii ndio sababu leo tunasikia watu waliokufa wanatokea, ni mapepo sio watu wenyewe. Biblia inasema wote waliokufa hawawezi kutoka kaburini mpaka Yesu atakaporudi kuwafufua.
Je sauti ya damu ya Abeli inathibitisha kuwa mtu akifa anaendelea kuishi?
Mwanzo 4:10 “Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”
Kutoa sauti tu hii haimaanishi kwamba Abeli yuko hai, na kama utasema hiyo inamaanisha Abeli yuko hai elezea fungu lifuatalo.
Habakuki 2:11 “Kwa maana jiwe litapiga kelele katika ukuta, nayo boriti katika miti italijibu.”
Je jiwe lilipiga kelele kweli nayo boriti ilijibu kiuhalisia? Pia elezea fungu lifuatalo.
Yakobo 5:4 “Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.”
Je ujira ulipiga kelele kwa uhalisia? Hapana! Wengi wanashindwa kutambua kuwa mbinguni ni sehemu ambayo hakuna majonzi tena. Ikiwa kulia kwa damu ya Abeli kunamaanisha abeli yuko mbinguni, jiulize hiyo ni mbingu gani ambayo watu wanalia?

Je mfalme Daudi yuko mbinguni sasa?​

Wengi hudai kuwa mfalme Daudi yuko mbinguni sasa kwa sababu Zaburi 16:10 inasema, “Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.” Lakini maelezo hayo hayamhusu Daudi, bali yanamhusu Yesu. Petro alisema…
Matendo 2:31-32 “[Daudi] yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.”
Kwa hiyo Zaburi 16:10 inamuhusu Yesu wala si Daudi. Daudi alikufa akazikwa wala hayuko mbinguni.
Matendo 2:29,34 “Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo…Maana Daudi hakupanda mbinguni;…”
Hapa Petro ameeleza wazi kwamba Daudi alikufa, akazikwa na hayuko mbinguni. Kama mtu angelikuwa akifa papo hapo anaenda mbinguni, kwanini hapa Petro anasema wazi kuwa Daudi hayuko mbinguni japokuwa alishakufa siku nyingi?
Katika Biblia hakuna mtu aliyewahi kufa akazikwa harafu ikasemekana eti yuko mbinguni, wote walioenda mbinguni ni wale waliofufuka kwanza au wale waliopaa moja kwa moja. Hayupo hata mtu mmoja aliyewahi kwenda mbinguni roho tu bila mwili.
Luka 24:36-39 “Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.”
Yesu alikuwa na mwili na mifupa wakati anapaa, Wakristo wote watakuwa na miili wakati wa kupaa na Bwana Yesu kwenda mbinguni, mara baada tu ya kuwa wamefufuliwa wakiungana na wale walio hai.
Wafilipi 3:20-21 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu…”
Hakuna mtu aliyewahi kwenda mbinguni roho yake tu bila mwili, wote ambao wako mbinguni walienda na miili yao pia, na wote watakaokolewa siku ya mwisho wataenda na miili yao pia. Hivyo ukiamini fundisho la toharani, au la kwamba mtu akifa tu papo hapo anaenda mbinguni au motoni, jua kwamba fundisho hilo ni akili za wanadamu na ni uongo​

Similar Discussions

Back
Top Bottom