Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Mawazo yako yanaweza kuonekana finyu kwa mtu ambaye ameshaingia kwenye biashara na kufanikiwa pakubwa.

Ni ngumu sana kumshawishi mtoto wa Bhakressa ambaye amekulia kwenye mazingira ya biashara na kuona hizi 500M-1B figures kama mauzo ya kila siku kwamba ajira ya kumlipa million 25 kwa mwezi ni bora kuliko biashara!

Ila ukija kwa mtu ambaye baba yake anaendesha duka ambalo faida zake ni kati ya 9000-12,000 kwa siku ni ngumu sana kumshawishi kuwa biashara ni bora kuliko kulipwa 2.5 millions per each month!

Ajira inategemea unaingalia in which dimensions! Kwa maisha ya sasa na uchumi wetu ulivyodorora mtu anayepata ajira ya kumlipa 3.5-5m ana unafuu mkubwa kuliko wafanyabiashara wengi wadogo wadogo wenye mitaji chini ya million 3!
Usipovuta bangi huwa una madini hatari jirani
 
Kuna Dogo mmoja alitoka kijijin kwao huko msoma kaja mjin kaanzisha biashara ya mpesa ,tgopesa Mambo ya uwakala kwa ujumla.
Kakomaa biashara ikawa vizuri akavuta mke ohhh msala uka anzia apo biashara anafanya ila matumizi Ni mengi mpka akawa anajikuta anagusa mtaji..! kule kijjn alikua kaachiwa ng'ombe kadhaa za urithi ..Mchezo ukawa Ni Mambo yakiyumba kidogo anapiga sim wanauza Ng'ombe ana boost mtaji.
Mpka Sasa Zizi kalimaliza na mda si mrefu tunamtafutia kirikuu arudi kwao kijijin Mimi nimemshauri kirikuu sio nzuri atafute hata pick up au guta kwa usafiri wa uhakika.
 
Hiyo ya kuponda ajira ni sizitaki mbichi hizi tu yaani ni kwa vile bongo ajira hazipo ila zingekuwepo hata hao waliojiajiri wangezikimbilia! Kuna watu wengi tu wana miaka 30 wameajiriwa wanakunja salary zaidi ya 3M monthly jiulize je ni vijana wangapi wa huo umri waliojiajiri wanakunja profit zaidi ya 3M monthly?
 
cc: jokate, nikiwapili

Jiulize kwanini hata wazazi wengi wanaofanya biashara wanapeleka watoto kusoma na kuwaambia wasome ili wapate ajira?? kwanini wasiwaambie wasome ili wafanye biashara ?? hapa sizungumzii wafanya biashara wakubwa kama kina bakhresa, nazungumzia wafanya biashara kwa mfano wenye maduka ambayo faida kwa siku unakuta ni chini ya elf 20, hapo anampigania mwanae aje kupata ajira ili aweze kupata mshahara wake wa milion au zaidi na asiteseke kuuza duka kila siku .

Biashara ni nzuri ikiwa na mikakati ya kuipanua, Mfano kwa watu kama wakinga tunajionea kwa macho yetu ni next level, , pale mtu unaona live bila chenga jinsi biashara ilivyo tamu kuzidi ajira , Lakini kama huna mikakati ya kupanua biashara yako, hapo ni sawa na kukamua chungwa kavu yani unalikamua sana lakini juisi ni ndogo sana (the squeeze aint worth the juice)

Natoa mfano kwa Marekani, Siku hizi wanaijeria ndio kundi linaoongoza kwa kuelimika kwa watu weusi, kwa sasa wanaajiriwa sana kwenye makampuni, serikalini, vyeo vizito, n.k Wale wamarekani weusi ambao walikuwa wanaona ajira ni utumwa ndio leo hii wanapiga kelele sana kwamba wanaibiwa ajira na hii yote ni sababu wanavyoona wanaijeria wanapiga mishahara safi, wana madaraka kwenye system, n.k.

Tatizo wengi wanapofikiria kujiajiri mawazo yao yanaenda moja kwa moja kwa wafanya biashara matajiri na kujiwekea bench ark hapo.

Kiukweli kujiajiri hapa Tanzania hakuna nafuu endapo utakuwa unapata kipato chini ya au kinacholingana na mtu alieajiriwa.

Tunaanza na swala la mahudhurio, Mtu alieajiriwa, anaweza akawa haendi kazi jumamosi na jumapili, hizo ni siku 104 kwa mwaka, tukiongezea na likizo ya mwezi hapo ni siku 134, tukiongezea na zile public holidays hapo ni siku kama 150. Kwa upande wa Mtu aliejiajieri hapo inakuwa taabu, wengi hasa wenye maduka hufungua kila siku, ama kwa mbali watapumzika jumapili tu, hakunapublic holidays wala kujipa likizo, N bampa to bampa.

Ajira ni kipato cha uhakika na kadri miaka inavyoenda kuna mishahara kupanda, promotions, n.k mtu anaweza kuingia kwenye ajira akiwa na 25, hapo atapata kipato chake cha uhakika mpaka akiwa na 60 nila misuko suko, Kimbembe kinakuja kwa aliejiajiri hapo, Yaani akiibiwa mzigo, akipata kesi, akifungwa, n.k hapo kupata mtaji upya inakuwa ni shughuli na inaweza kubadili maisha yake kabisa.

Kazni ni kuzea kazi tu, kazi nyingi hazina ugumu, ndio maana hata waliofoji vyeti wanapiga kazi fresh tu, Njoo kwene biashara sasa uone kam unaweza kufoji

Kiufupi Biashara ni nzuri lakini kama kipato ni chini kuliko alieajiriwa au kipo sawa, yule mwenye biashara atahangaika sana.

ntaendelea.....
hii inahusu na wale waoajriwa kiwandani amabapo unalipwa elfu nane kwa siku halafu unalipwa kwa wiki au unazungumzia wa maofisini na kompyuta na kiyoyozi???
 
Tatizo la ajira unakuwa mtumwa wa mwajiri wako haijarishi mshahara ni mkubwa kiasi gani

Ukijiajiri unakuwa huru, waajiriwa wenye maono wanawekeza wakiwa kwenye ajira na hawasubiri kustaafu wanaacha kazi.

Sent from my itel A16 using JamiiForums mobile app
Mbona hata ukiwa mfanyabiashara unakuwa mtumwa kwa wateja wako au utumwa ni kwa boss tu? Siku hizi kila sector ina utumwa hata ndoa nayo ina utumwa ila watu wanaingia kila siku!
 
Omba Mungu usipate majanga, biashara ni bora kuliko kuajiriwa. Mtu wa kawaida muuza chips, kama ana nidhamu ya pesa anamzidi mwajiriwa anaelipwa 1000000 kwa mwezi.
Ukitaka kujua Mambo kwa ground Ni tofauti huyo muuza chips Mpe Option mbili
1 - Mwambie Kuna kazi ya kulipwa mil moja kwa mwezi je Yuko tyari au
2 - aedelee kuuza chips

Uone atachagua kwenda wapi
....mind you ukilipwa mshahara wa mil moja kwa mwezi uwe unajua Apo Kati Kati Kuna hela nyingine ya sintofaham utaifaid Sana tu
 
Ukitaka kujua Mambo kwa ground Ni tofauti huyo muuza chips Mpe Option mbili
1 - Mwambie Kuna kazi ya kulipwa mil moja kwa mwezi je Yuko tyari au
2 - aedelee kuuza chips

Uone atachagua kwenda wapi
....mind you ukilipwa mshahara wa mil moja kwa mwezi uwe unajua Apo Kati Kati Kuna hela nyingine ya sintofaham utaifaid Sana tu
Inategemea na ajira, usiwekee uhalali pesa zaido ya mshahara, nilishafanya ajira ambayo hamna hata senti tano nje na mshahara
 
Daah wabarbaig bwana... Yani tangu kuzaliwa kwako Hadi miaka 60..unategemea kupata million 90 au 100 Kama kiinua mgongo...Yani inakua ndoto za maisha yako Ni kuwa na millioni 90 au 100 kutoka kuzaliwa Hadi kuzeeka...biashara ngumu lakini utatoka damu miaka 5-10..lakini growth yake iko sexy

mna mahesabu makali sana,ila field pana waprove wrong sana.
 
Inategemea na ajira, usiwekee uhalali pesa zaido ya mshahara, nilishafanya ajira ambayo hamna hata senti tano nje na mshahara
Kazi gani hyo mkuu Kama ulikua unalipwa laki Tisa kushuka chini Apo Ni sawa .
Mshahara wa Kuanzia mil moja Mara nyingi Kuna neema katkat.
 
Ukitaka kujua Mambo kwa ground Ni tofauti huyo muuza chips Mpe Option mbili
1 - Mwambie Kuna kazi ya kulipwa mil moja kwa mwezi je Yuko tyari au
2 - aedelee kuuza chips

Uone atachagua kwenda wapi
....mind you ukilipwa mshahara wa mil moja kwa mwezi uwe unajua Apo Kati Kati Kuna hela nyingine ya sintofaham utaifaid Sana tu
Muuza Chips anaweza kubali, ila haimaniishi kuajiriwa ndio kitu bora zaid.

Ila tufanye hivi, tutakutana uzeeni, sio ndio final huko.

Wenye pension, wanapata pension inaisha ndani ya miaka miwili, depression anakufa au huyu mzee anamzunguko wake wa investments zake ametulia hme
 
Muuza Chips anaweza kubali, ila haimaniishi kuajiriwa ndio kitu bora zaid.

Ila tufanye hivi, tutakutana uzeeni, sio ndio final huko.

Wenye pension, wanapata pension inaisha ndani ya miaka miwili, depression anakufa au huyu mzee anamzunguko wake wa investments zake ametulia hme
Mzee kufa Ni halali yake mda wake unakua umeisha.
Ndo maana kifo kipo Ni kwa ajili yetu mkuu.
 
fanya biashara kijana,usipumbazwe na mshahara wa kuajiliwa, business ndo kila kitu kiongozi.fikilia ukistaafu wanao hawatarithi kazi yako,hawana Cha kuendeleza kutoka kwako,lakini mfanya biashara akizeeka au akifa ,wanae watarithi biashara ya mzee wao na kuendeleza pale alipoishia. Muajiliwa akifa au akistaafu kazi, mfano alikuwa na Masters au PhD watt hawato rithi hiyo masters au PhD yake.biashara huwafanya watu waishi maisha marefu,trust me!!
 
Acha nipate ilmu
kama hamna cha kuandika muwe mnasoma na kupita bila kukomenti, mnaudhi sana kwa vijijino vifupi visivyo na maana ya kujifunza na mnaziba nafasi kwa kuongeza idadi ya komenti zisizo na maana
 
Hapo umeongea yani! Biashara zikiwa zaidi ya moja utamudu vyema sana na hakika zitafikia maturity! Ama uwe na backup ya kazi.

Ila biashara ikiwa yenyewe tu ikiyumba unayumba nayo kama pipa la mbege mpaka mnaanguka wote pwaah!!! Biashara inataka booster za mara kwa mara pale ambapo inakuwa bado haijastawi na kuwa na wateja wengi wa kudumu..

Sasa imagine una 10M umelipa pango na mtaji wa kuanzia. Biashara inaenda inayumba inataka boost ya 3M ikae sawa. Huna hata mia hapo kinachofata lazma ulie tu na kuonekana huna akili
Kwani kazini huwezi kufukuzwa
 
Back
Top Bottom