Tusipodhibiti haya, nchi haitakuwa salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusipodhibiti haya, nchi haitakuwa salama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ground Zero, Jan 4, 2012.

 1. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IMG_20120104_065404.jpg IMG_20120104_065342.jpg
  Mniwie radhi kwa kuweka picha ambazo hazipendezi hapa. Hawa ni vijana watatu waliopatwa na mauti kwa kuchomwa moto ( kama wanavyoonekana kwenye gari) na mwingine akiwa amepigwa mawe pale chini ( alikuwa hai bado wakati picha zinachukuliwa leo asubuhi). Tukio hilo lilitokea leo asubuhi eneo la makuburi ambapo watu wenye hasira wamewachoma hawa vijana kwa tuhuma za ujambazi.

  kutokana na uzoefu wangu, tabia ya kujichukulia sheria mikononi imegharimu maisha ya watu wengi wasio na hatia na kuwasababishia vilema vya maisha kwa dhana tu. Siku hizi hata mwendawazimu akipiga kelele za mwizi ukiwa unapita hata kama unafanya mazoezi ya kwenda kwenye michezo ya olympic watu bila kujiuliza wanaweza kukuvamia na maisha yakakutoka. Tabia hii isipodhibitiwa kwa adhabu kaliiiiii, nchi hi haitakuwa salama kwa yeyote!
   
 2. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unayosema ni kweli mtupu. Binafsi nadhani pale ambapo mfumo wa sheria umekufa, matokeo ni watu kujichukulia hatua mkononi. Ni vema badala ya kuwaambia watu wasijichukulie sheria mkononi, serikali (hasa mahakama na polisi) wakajua kutoa haki na kuachana na rushwa. Kuwa ushahidi usio-rekodiwa unaoonesha maeneo mengi yenye vibaka polisi wanahusika kuwalea! Sasa kama polisi jukumu lao ni nini? Mimi binafsi ni victim wa ulegelege wa polisi! Nimeibiwa kwenye daladala. Bahati nzuri nikashtuka mara baada ya kushuka. Konda anaondoa gari nikamg'ang'ania kuwa nimeibiwa. Kituo cha polisi kipo karibu, nilikomaa kumlazimisha dereva kupeleka gari kituoni. Tumefika kituoni, nikaambiwa niwa-oneshe watu niliodhani wamenibiwa. Nikachagua watu watano walikuwa wamekaa karibu nami. Ameanza kupekuliwa mmoja mmoja, hadi mtu wa nne ndo akakutwa anahela yangu! See what happened. Polisi akamwambia umeona leo umegunduliwa, kila mara tunakuachia. Kilichofuata, nikarudishiwa hela yangu, polisi akamwachia yule jamaa akapeta! Nikamwuliza akanijibu mbona umerudishiwa chako? Kwa mtindo huu unadhani haya yatadumu hadi lini?

  Jambo la msingi ni vema kujiuliza kwanini watu wanajichukualia sheria mkononi? Je inamaana utu umetuishia? Je tukiambiwa wasijichuklulie sheria hapo tutakuwa tumemaliza tatizo? Bila shaka kuna root cause! NI vema kuwahamasisha polisi kuonesha uaminifu ili watu warudishe imani kwa jeshi letu la polisi pamoja na mahakama. Hii ni pamoja na kutoa haki kwa wakati muafaka.
   
 3. Ground Zero

  Ground Zero JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulichosema ndicho kinachoangamiza jamii yetu kwa sasa;kukosa imani kwenye vyombo vya dola hasa polisi. Lazima haki itendeke kwa kufuata sheria la sivyo nchi yetu itafikia kwenye hali ya anarcgy siku moja.
   
 4. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  wewe ni mchochezi, ngoja KOVA aje nakusemelea
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nachukia sana watu wanaoua wenzao kama wanyama.
  Shame on them.
   
 6. r

  rehema nyuda Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwli dada lizzy unachosema, inapofikia hapo mimi huwa nakosa maana au nini majukumu ya hivyo vyombo vya dola kwakua hawafanyi yale majukumu yao wanao takiwa kufanya hali hiyo ndiyo ina pelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi matokeo yake ndio haya ya watu kuuwawa kama wanya wakati sheria zipo.
   
 7. m

  moshingi JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachangiaji wengi wameelekeza lawama kwa Polisi, nadhani JF kama home of Great Thinkers tungeenda mbali zaidi ya hapo.
  Ili kuweza kutibu ugonjwa lazima ujue Chanzo na wala siyo kukimbilia kutibu dalili. Chunguzeni Elimu walizonazo askari wetu,
  utaratibu wa ajira zao, je wanapatiwa vitendea kazi kama vile magari na mafuta ya kutosha?,Maslahi yao yakoje?
  Vivyo hivyo Upande wa mahakama inatupasa kuchunguza, ni kwanini karibia kila kesi ya mtu mwenye uwezo kifedha Jamhuri hushindwa?
  Kisha tujiulize mbona hao wananchi wenye hasira hawajawahi kuwashambulia wezi wakubwa wanaoiba mamilioni ya watu binafsi
  na ya uma? Badala yake huko mitaani utasikia wakiwasifia wezi hao kuwa ni wajanja, Mashefa, mabedejee n.k, Wanamuziki wetu huwatungia nyimbo za kuwasifu, au kutaja majina yao kwenye nyimbo zao kama vile wamefanya mazuri sana kwenye jamii.
  Ninachotaka kusema Lawama siyo za Polisi peke yao, hili ni jambo pana sana linalohitaji utafiti wa kina.
   
 8. M

  Mathias sichilima New Member

  #8
  Jan 16, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jeshi la polisi kwa nafasi kubwa linabeba lawama na pia ikifuatiwa na mahakama. Elimu sio kuwa sababu ya jeshi la polisi kutotena haki kwa raia mbona Mawakili na Mahakimu wanaelimu kubwa na bado niyaleyale kuwa jamuhuri imeshindwa kesi. Bado sheria ya utumishi wa umma inamapungufu mengi kwa kuendelea kuwalinda mapolisi na mahakimu.
  Ingawa kwa nafasi ya pekee lawama zinabaki kwa serikali. Kama mtuhumiwa kabaka mwanao alafu anashinda kesi na mtaani anadunda. Mwanao anamimba masomo kushnei. Hapa kwa dhati nasema serikali imeoza.
   
Loading...