Tusiopenda kufanya mazoezi tuna hoja, sababu na visingizio vya msingi sana; Tuvumiliane Tafadhali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,340
2,000
Harakati zangu za mazoezi zilianza tangu Enzi za ujana huko chuo hadi sasa mtu mzima, Lakini hazijawahi kudumu japo kwa wiki mbili.

Nakumbuka enzi hizo; Niliwahi andaa Jogging kuanzia mliman chuo, kupitia Ubungo > Magomeni > Morocco > Mwenge

Tuliondoka vizuri tu lakini nilipofika Manzese Nilichemsha kwakweli, ikabidi Nipande zangu daladala hadi Mwenge!

Sikurudia tena kufanya kwanza nikaanza kujifariji; Sina hela ya kula vizuri mazoezi ya nini, nikaachana na mazoezi uchwara!

Nilivyomaliza chuo; Mzuka wa mazoezi ukaanza tena; nikawa siku za weekend naenda kunduchi beach, lakini napo sikudumu sana kwasababu ya visingizio vya kukosa nguo za mazoezi,

Mungu si Athumani, nikanunua raba na pensi ya michezo, nikarudi ulingoni! Kulekule Kunduchi Beach, siku za weekend, siku ya kwanza nikakaza fresh, siku ya pili pia nikakomaa, Siku ya tatu nikawaza: Ya nini kufanya mazoezi alfajili mwisho nikabwe bure? NIKAACHA!

Maisha yakaendelea miaka na miaka, nikawaza huenda mazoezi mazuri ni yale ya GYM, wacha nikajiandikishe.

Nililipia GYM mwezi mmoja, katika mahudhurio yangu pale GYM nakumbuka nilifika siku tatu tu nikaghairi; kwanza nikawaza, mazoezi gani sina hata gari aaah? ...Nikaachana na GYM
Miaka ikasonga! Niliponunua gari, nikarudi tena GYM kujiandikisha, nikahudhuria siku mbili nikaopoa mrembo mmoja; sikurudi tena mazoezini, na mazoezi nikaacha tena. Kwanza nikawaza napoteza pesa na mafuta bure.

Nikajisemea wacha nikija jenga nyumba yangu nitaweka chumba cha mazoezi.

Miaka ikasonga, nilipojenga, nikaweka chumba cha mazoezi, lakini nakumbuka nilifanya wiki moja tu, nikawaza tena labda wacha ninunue mashine kabisa za mazoezi zitanisaidia!
Mwaka jana nilifanikiwa kuzinunua lakini nimezitumia siku chache tu nikaona miyeyusho! NIKAACHA

Hadi leo chumba cha mazoezi nimekigeuza STOO!

Mazoezi yana wenyewe! Tuwaachie mazoezi yao EBOOOH!!
 

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,159
2,000
Kipindi nasoma O level ile miaka minne yote niliitumia kucheza Mpira na mazoezi ya karate.

Lakini baada ya kumaliza tu mitihani nilivyorudi home nikabaki nafanya mazoezi ya mpira Mara chache sana.

Baada ya miaka 20 kupita na kuwa na tumbo kama nimeweka mitambala niliaanza kujinyima kula ili kushape vizuri tumbo nikawa napungua mwili tumbo lipo vile vile nikashauriwa nipige push up daily.

Hivyo nimeanza sasa hivi Nina week ya tatu naona matokeo si mabaya sana.

Leo Juma pili hii mpaka sasa hivi nipo kitandani naperuzi JF sijapiga push up hata moja.
 

Jeceel

JF-Expert Member
Feb 6, 2018
1,082
2,000
Mazoezi maana yake ni mazoea ungejitahidi angalau umalize mwezi kwa kufanya mazoezi hakika usingeacha tena kutokana na faida ungezipata kwa wakati huo , na pia inawezekana ulianza kwa speed sana ndio sababu uliishia njiani
 

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,340
2,000
Mazoezi maana yake ni mazoea ungejitahidi angalau umalize mwezi kwa kufanya mazoezi hakika usingeacha tena kutokana na faida ungezipata kwa wakati huo , na pia inawezekana ulianza kwa speed sana ndio sababu uliishia njiani
nitafanyia kazi wazo lako
 

carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,827
2,000
Fat level itakapokua kubwa na moyo unaenda 1000miles per second ndio utajua zoezi ndio mama na baba yako.....
Acha kumtisha mwenzako.... duniani hapa hakuna atakayetoka hai uwe mnene au sixpack.... sasa wewe endelea kukimbia kimbia bila kukimbizwa ukihisi utaishi milele...
Wenzako tunaishi tunavyotaka BTW life expectancy yenyewe miaka 63
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
8,810
2,000
Acha kumtisha mwenzako.... duniani hapa hakuna atakayetoka hai uwe mnene au sixpack.... sasa wewe endelea kukimbia kimbia bila kukimbizwa ukihisi utaishi milele...
Wenzako tunaishi tunavyotaka BTW life expectancy yenyewe miaka 63
Jipe matumaini ya uongo mamaeee!

Hapo kwenyewe unapumulia mashine kwa upumuaji ulivyo wa hovyo!

Kanyanyue vyuma acha umama!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom