Tusimuachie Rais Samia jukumu la kuinua uchumi wa nchi, tushirikiane..

Jun 1, 2021
99
104
Wadau wa Biashara na Uchumi,

Nchi yetu inapitia kwenye hatua za makusudi za kuinua uchumi ulioathiriwa vibaya na corona. Tunatoa wito kwa kila mdau wa sekta yoyote, asimuachie jukumu hili kiongozi wa nchi pekee.

Sisi tumeamua kuangalia upande wa sekta yetu ya usafirishaji. Tumeona namna ambavyo taasisi hasa za biashara na wajasiriamali wakipata hasara kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo pale wanapoagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Na hii ndio sababu iliyopelekea tukutane na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 3 Septemba mwaka huu (juzi) na kueleza njia mbadala za kusaidia kubusti biashara na harakati za wajasiriamali ili basi uchumi wetu uendelee kuzunguka na shughuli za uzalishaji ziende vizuri.

Habari ifuatayo kutoka magazeti na vyombo mbalimbali vya habari inaeleza zaidi:

1.jpeg
----​

Na Selemani Msuya (Raia Mwema/Mwanahalisi)

KAMPUNI ya Usafirishaji ya World Logistics (WLC), imeanzisha huduma mpya ya kuagiza na kufikishia bidhaa kwa mteja (Corgo Pickup & Delivery Services), ili kukabiliana na changamoto za Uviko-19 kwa wafanyabisahara, wajasiriamali na kampuni wanaofuata bidhaa nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa WLC, Agnes Daniel wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Ofisa Masoko huyo alisema wamekuja na huduma hiyo hasa katika kipindi hiki cha Janga la Uviko-19 ambalo limekuwa na athari kwa waagizaji na wafanyabiashara nchini.

Daniel alisema tangu kutokea janga la Uviko-19 biashara ya uagizaji mizigo au bidhaa mbalimbali ikishuka hivyo wanaamini njia hiyo mpya itaweza kusaidia waagizaji na wafanyabiashara kutoka kwenye janga la kuyumba kibiashara.

“Wakati dunia bado inahangaka na janga la Uviko-19, tumeamua kushiriki kwa kurahisisha kwa kulinda afya za Watanzania ambao wanaagiza au kufuata bidhaa nje kwa kuwaletea huduma hii ya Cargo Pickup & Delivery Service,” alisema.

Alisema kupitia huduma hiyo WLC watafuata mzigo au bidhaa ya mteja kiwandani, watafunga na kusafirisha hadi kwa muagizaji bila yeye kusumbuka.

Ofisa Masko Mkuu huyo alisema kupitia huduma hiyo muagizaji ataondokana na gharama za kusafiri, hoteli na michakato mingine ambayo inagharimu muda na fedha huku akibaki salama dhidi ya maambukizi ya Uviko-19.

Daniel alitoa wito kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na Watanzania kwa ujumla ambao wanahitaji kuagiza bidhaa kutoka nje watumie WLC ambayo ni kampuni ya kizalendo.

Naye Ofisa Masoko, Apaisaria Godvice alisema kupitia huduma hiyo wanaamini mzunguko wa biashara utakuwa kwa kasi hivyo kusaidia lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kufanikiwa.

Godvice alisema wameeamua kuenda na teknolojia ili kuhakikisha ajira ambazo zipo zinakuwa endelevu hivyo ni imani yao wateja wao wataitumia huduma hiyo katika kufanya kuagiza bidhaa nje ya nchi.

“Sisi tunaagiza mizigo kutoka China, Uingereza, Japan, Afrika Kusini, Falme za Kiarabu, India, Malaysia na kwingineko. Lakini pia tunasafirisha mizigo kwenda duniani kote,” alisema.

Alisema katika kipindi cha miaka 15 ya WLC kutoa huduma wameweza kufikia wajasiriamali, wafanyabishara, makampuni na watu binafsi wengi hivyo lengo ni kuendelea kusaidia makundi hayo ili kukuza uchumi wa Tanzania.

Ofisa huyo alisisitiza kuwa pamoja na kuagiza mizigo na bidhaa kwa njia ya meli pia wanatumia usafiri wa ndege na barabara kuagizza na kusafirisha mizigo.

---

Tazama video za mkutano na wanahabari.


 

Attachments

  • Raia Mwema.pdf
    397.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom