Samia Cup Kuinua Vipaji Same

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mkuu wa Wilaya ya Same Kaslida Mgeni amewashauri Vijana kuhakikisha wanawekeza nguvu zao kwenye michezo ili kukuza vipaji vyao badala ya kujihusisha kwenye vitendo vya uhalifu ikiwemo kilimo cha bangi na mirungi.

DC amesema hayo kwenye uzinduzi wa mashindano ya Michezo ya Dkt.Samia Cup, yaliyoandaliwa na Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango ambapo amesema uamuzi huo wa Mbunge kuanzisha mashindano utasaidia kuibua vipaji hasa kwa Vijana, pia kuimarisha afya kama inavyosisitizwa na Serikali.

Akifungua michezo hiyo Naibu Katibu Mkuu UVCCM - Bara, Mussa Mwakatinya amesema Dkt Samia Cup imeanzishwa ili kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa iliyofanyika kwenye Jimbo la Same Mashariki ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa madarasa, uboreshwaji wa huduma za afya, n.k.

View: https://www.instagram.com/p/CzQbLjOCtlw/
 
Wakuu ,tunaombeni SAMIA CUP ifanyike nchi nzima na kila mkoa uchague vijana wenye vipaji ambao watashindanishwa na kupata bingwa wa mkoa na mshindi akabidhiwe kombe siku maalumu kama siku ya uhuru au muungano .Tunashauri watakaochaguliwa kwa kila mkoa wasiwe wameshiri mashindano ya ligi daraja la kwanza ama ligi kuu ili kufikia malengo ya haya mashindano yaani kuibua vipaji vipya na vichanga kabisa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom