Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Kwa yanayofanyika huko kibiti, sidhani kama wananchi tutaweza kusogeleana na jeshi la polisi tena. Uhakika kuwa polisi ni walinzi wa raia na Mali zetu umetoweka na sasa wanakibiti wanakimbiakimbia tu kama kuku walioona mwewe. Lkn ipo siku tutafika tuendako.
 
Sidhani kama hawa nyumbu wanaelewa!
We jamaa unajidai sana.Sijui unaringia nini hasa,unapata faida gani kuwaita binadamu wenako Nyumbu? Unajivunia UCCMM wako wakati hadi inakera.Uzi umeletwa,ume balance ila wewe unayejiona "malaika" unaona huu ni ujumbe wa hao Nyumbu!. Exposure kidogo zinawafanya mjione miungu na majiniazi kuliko hata akina Plato,Newton n.k
 
Nikiangalia mijadala mingi ndani ya JF (na hoja zangu zikiwemo) napata hofu sana kama kunajengwa dhana kwamba ni halali kupambana na jeshi la Polisi ama pia ni halali kuamrisha jeshi la Polisi kupambana na wananchi hata kama wakati mwingine na wananchi wasio na hatia.

Kunajengwa chuki kubwa sana kwa wananchi dhidi ya jeshi la Polisi kwa jinsi linavyotumika. Kwa watu wa vyama vya upinzani wanajenga taswira kwamba Jeshi la Polisi linatumiwa na CCM dhidi yao. Na CCM nao wanaona ni halali Jeshi la Polisi "kuwashughulikia" wapinzani wao wasiotaka kutii "mamlaka halali".

CCM na wapinzani wao kisiasa ni wananchi wa Tanzania wanaoishi kwenye jamii yetu. Kama wapinzani wanapoua Polisi wanaona ni afadhali na wao "kimewapata" na CCM nao wakiona ni "halali" kutumia Jeshi la Polisi dhidi ya wapinzani wao. Basi si CCM wala wapinzani wao watakaochukiwa na Polisi bali ni Polisi watakaochukiwa na Makundi hayo mawili ingawa itakuwa kwa wakati tofauti.

Siku CCM wakiona wapinzani wao wanaandamana na kufanya mikutano bila ya kuzuiwa na Polisi, lazima wataona Polisi limekuwa Jeshi legelege na watawachukia. Na siku wapinzani nao wakizuiwa kufanya mikutano na maandamano, wataona Jeshi la Polisi linatumika kisiasa.

Ili tusijenge chuki dhidi ya Jeshi la Polisi ni lazima tuliache Jeshi letu la Polisi lifanye kazi zake kwa weledi kwa kuzingatia sheria iliyounda jeshi hilo na taratibu zilizopo!
Mbona umeandika kama upo nje ya mipaka ya taifa la Tanzania.
Kwani sheria za jeshi la polisi zinaelezaje kuhusu kukabiliana na "watuhumiwa"?
 
Umeandika "tuliache jeshi la polisi lifanye kazi yake kwa weledi", Kwani limeshikwa na nani? I mean ni nani analizuia au kulisababisha lisifanye kazi yake kwa weledi?
Kama umenisoma vizuri ni kwamba sisi ndiyo tuliache Jeshi letu lifanye kazi zake kwa weledi bila ya kuingiza ushabiki wetu usio na tija!!
 
Kwani sheria za jeshi la polisi zinaelezaje kuhusu kukabiliana na "watuhumiwa"?
Inategemeana na hali ya mambo wakati huo wa kukabiliana na "watuhumiwa". Kwa mfano kama hao watuhumiwa wamekaa chini na wamenyoosha mikono juu, kuna haja gani ya kuwashindilia virungu?
 
Polisi tanzania unaweza kuwa una infomation muhimu baada wakulinde we ndo unakua mtuhumiwa usiombe uambiwe unalisaidia jeshi ka polisi utajuta
 
We jamaa unajidai sana.Sijui unaringia nini hasa,unapata faida gani kuwaita binadamu wenako Nyumbu? Unajivunia UCCMM wako wakati hadi inakera.Uzi umeletwa,ume balance ila wewe unayejiona "malaika" unaona huu ni ujumbe wa hao Nyumbu!. Exposure kidogo zinawafanya mjione miungu na majiniazi kuliko hata akina Plato,Newton n.k
Achana na huyo fala sijui anajiita nyani ngabu huoni ana element zote za ushoga
 
Polisi tanzania unaweza kuwa una infomation muhimu baada wakulinde we ndo unakua mtuhumiwa usiombe uambiwe unalisaidia jeshi ka polisi utajuta
Kuna chanzo cha jeshi letu kuwa hivyo. Ama ni upungufu wa maadili ama ni hali duni za maisha yao na maslahi yasiyozingatia ugumu wa kazi yao wanayoifanya!!
 
  • Thanks
Reactions: 314
Matendo ya polisi yanawajengea chuki. wananchi kwa mamilioni hawawezi kuwa wrong all the time. Matendo yao, kukubali kwao kutumika kisiasa na kushindwa kuwalinda na kuwatetea wanyonge ndani ya nchi yao ndio kunawafanya wasipendwe.

Hii chuki ni self reflection kwa jeshi la polisi kujitazama na kubadilika. Upendo haulazimishwi., rapport hailazimishwi.
 
Kuna chanzo cha jeshi letu kuwa hivyo. Ama ni upungufu wa maadili ama ni hali duni za maisha yao na maslahi yasiyozingatia ugumu wa kazi yao wanayoifanya!!
Wanakosa weledi mkuu yaani polisi akivaa gwanda anakua kama ye sio raia wa tz anachijua ye ni torture tu
Siwapendi polisi kiukweli
 
Hii chuki ni self reflection kwa jeshi la polisi kujitazama na kubadilika. Upendo haulazimishwi., rapport hailazimishwi.
Unadhani Polisi ni watu wenye uelewa mdogo sana kiasi kwamba hawajui wafanye nini wapendwe na wananchi? Kuna jambo linawafanya wawe kama hivyo unavyowaona wewe!!
 
Inategemeana na hali ya mambo wakati huo wa kukabiliana na "watuhumiwa". Kwa mfano kama hao watuhumiwa wamekaa chini na wamenyoosha mikono juu, kuna haja gani ya kuwashindilia virungu?
Je binafsi unaona ni kweli jeshi la polisi linatumika?
Na hivi unafikiri chanzo cha hili tatizo la jeshi "kudhaniwa/kuonekana" linatumika limeanzia wapi na lini?
Maana umekuja na njia mbadala bila kuonesha chanzo cha tatizo kimeanzia wapi.
 
Unadhani Polisi ni watu wenye uelewa mdogo sana kiasi kwamba hawajui wafanye nini wapendwe na wananchi? Kuna jambo linawafanya wawe kama hivyo unavyowaona wewe!!

Kupendwa hakuhitaji uwe na akili au uelewa mkubwa., ni choice wamefanya. Wameamua kuwa animosity is worth less than changing their current direction.
Siku wakiona cost ya hii animosity imekuwa kubwa sana watabadilika. Ila ni jambo lililo wazi nikitazama vitengo vya jeshi la polisi chenye afadhali ni kitengo cha zimamoto tu!vitengo vilivyobaki kama trafki, FFU, etc si habari njema.
 
Back
Top Bottom