Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,229
Kwa kumbukumbu tu,Polisi waluwahi kuacha kulinda mikutano ya CHADEMA na shughuli ikafanyika kwa amani.
Mkuu tangia lini Police wa Tanzania wameacha kuwa wanasiasa? RPC na OCD ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kwa wilaya na mikoa yao. Wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa/wilaya ni Mkuu wa mkoa na Mkuu wa Wilaya reapectively. Inajulikana wazi sifa ya kwanza ya kuwa mkuu wa mkoa wilaya(na labda DED/RAS???) ni uwe kada na mwanachama mtiifu wa CCM. Sasa kama RPC/OCD ni wajumbe wa vikao vinavyosimamiwa na makada wa CCM its obvius kuwa nao ni wanasiasa tu kama hao makada wenzao wa CCM.Na. M. M. Mwanakijiji![]()
Mara nyingi napenda kusoma hoja na kuziacha tu hata kama naona zimejengwa vibaya. Hata hivyo kuna wakati inabidi nijirushe ndani kwani hatari ya kuacha hoja hizo zisimame kama zilivyo ni kwamba zinapata uhalali wa kuaminika hasa kwa watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawawezi kuona ulaghai wa hoja (fallacy) uliofichika ndani yake.
Yametokea mauaji ya polisi jana usiku ambapo polisi wanne wameuawa, kuporwa silaha na wananchi wengine kujeruhiwa. Mwitikio wa wa baadhi yetu ni kushtushwa na kukasirishwa na kitendo hicho na kukilaani bila kukihusisha na siasa za nchi yetu – iwe upinzani au chama tawala. Tumechukulia tukio hilo kama kitendo cha uhalifu ambao hakina namna yoyote ya kuonekana “kinaeleweka”.
Hata hivyo wapo baadhi ya ndugu zetu – na ninaamini wanaamini wanafanya kwa nia njema kabisa – ambao kwa kutumia ujanja wa maneno wakijificha katika kutoa rambirambi na pole wakijaribu kuhusisha tukio hilo na siasa zinazoendelea nchini. Baadhi yao wanajaribu kuonesha kuwa tukio hilo limetokea kwa sababu ya Polisi kujihusisha na kulinda amani au kuonekana wanatekeleza maagizo ya kisiasa ambayo yanakandamiza au kubana siasa za upinzani.
Julius Mtatiro – akiandika katika ukurasa wake wa Facebook anasema “Baada ya majambazi kuwaua POLISI (RIP), sehemu kubwa ya raia kwenye mitandao ya kijamii wanashangilia. Nimeshtuka sana. Hii ni dalili kuwa jamii yetu imeanza kugawanyika. Kwa nini Raia wanaanza kufurahia unyama wanaotendewa ndugu zao? Hii chuki imeanza lini? Kaileta nani? Serikali ijitathmini upya, kuna tatizo kubwa na litaanza kukua. Mungu awasitiri wafiwa wote”
Kwa ufupi yeye anasema kuwa wapo watu wanafurahia mauaji ya polisi kwa sababu Serikali ndio imewafanya watu wafurahia mauaji ya ndugu zao; kwamba, serikali ikiacha kufanya mambo fulani basi watu hawatofurahia mauaji ya polisi! Hii ni miongoni mwa hoja muflisi kabisa ambazo nimewahi kuzisoma. Hivi ni serikali gani ambayo itaacha kufanya mambo ambayo inaamini kuwa ni ya usalama kwa taifa au ni ya muhimu ati kwa sababu watu wachukia polisi?
Anaposema “Serikali ijitathmini upya” ana maana gani? Serikali ijitathmini katika mambo gani? Na anapozungumzia “chuki” anaitambua vipi? Siyo kweli kwamba mahali pengi duniani watu wanaochukia polisi mara nyingi ama ni wahalifu wao wenyewe au wanufaika wakubwa wa uhalifu? Raia anayetegemea usalama wake na amani kwenye mtaa na nyumba yake nan chi yake anaweza vipi kufurahia polisi wakiuawa? Kwamba, raia mwenye chuki na chama fulani cha kisiasa au kiongozi fulani wa kisiasa – sema Rais kwa mfano – anapata uhalali gani kufurahia mauaji ya polisi ambaye siyo mwanasiasa na siyo kiongozi wa kisiasa bali mtu aliyekubali kupewa jukumu la kulinda nchi na usalama wa raia? Siyo kwamba, mtu anayehamishia chuki za kisiasa kwa polisi anaongozwa siyo na chuki bali ujinga uliopilitiliza; yaani hajui polisi wanatekeleza majukumu yao vipi.
Naye Peter Msigwa – Mbunge wa Iringa Mjini – na yeye anaenda mbali kidogo katika hili lakini akitumia ‘fallacy’ ile ile. Yeye anasema – kwenye mtandao huo huo wa Facebook – “Nichukue nafasi hii kutoa pole sana kwa familia za Askari wetu waliouwa kikatili na Majambazi , hii haikubaliki kabisa . Nashauri jeshi la polisi liimarishe kitengo cha intelejensia kukabiliana na uhalifu wa aina hii badala ya kitengo hicho kuwa cha KISIASA kuKABILIANA NA UPINZANI na kuilinda CCM”
Na yeye pia anafanya (commit) kosa lile lile la Mtatiro. Yeye anaona kuwa mauaji haya ya polisi yasingefanyika kama Polisi wasingekabiliana na upinzani au “kuilinda CCM”. Hata tukichukulia kwa ajili ya hoja hii kuwa kweli Polisi wanatumika kukabiliana na upinzani au wanailinda CCM ni kwa vipi hili linaelezea au kuhalalisha kwa namna yoyote mauaji ya vijana wetu ambao walikuwa wanaenda kupokea lindo kulinda Benki ya CRDB?
Vinginevyo tunaweza vipi kuhusisha kwake tukio la mauaji ya polisi na suala la siasa za upinzani?
Hivi ni kuwa kama kungekuwa hakuna huu mgongano hewa kati ya upinzani na serikali hawa polisi wasingeuawa? Hivi wahalifu (wawe majambazi au vinginevyo) wanaamua kushambulia polisi na kuwaua kwa sababu polisi wanatekeleza maagizo yao ambayo yana athari kwa vyama vya siasa maagizo ambayo wao hawana namna ya kuyakataa? Hivi ni kweli kama polisi wakiamua kukaa pembeni na kuacha wapinzani wafanye mambo yao, wanaandamane popote na kwa namna yoyote bila ulinzi wa polisi hivi kweli likiharibika jambo hawa viongozi wa upinzani watasema “polisi” ndio wakulaumiwa?
Bila ya shaka wengi mnakumbuka lile tukio lililotokea wiki si nyingi zilizopita huko Dallas, Texas ambapo waandamanaji wenye kutetea haki za weusi katika mwamko wa Black Lives Matter walikuwa wanaandamana kupinga vitendo vya kikatili ambavyo wameona vikifanyika kwa weusi na baadhi ya polisi weupe. Katika kuandamana kwao kule kupinga polisi bado walihitaji ulinzi wa polisi! Na Polisi wale wakiwa wanawalinda waandamanaji wakajikuta wanashambuliwa na polisi watano wakauawa siku ile!
![]()
(Pichani msafara ya mazishi Afisa Liu huko Marekani, aliuawa kwa kushtukizwa akiwa ndani ya gari na askari mwenzie. Chini msafara mwingine wa polisi wa New Jersey aliyeuawa Melvin Santiago).
![]()
Na baadaye kulikuwa na tetesi za baadhi ya makundi ya vijana walikuwa wakishangilia mauaji ya polisi wale; lakini wakati huo huo baadhi ya waandamanaji wale wale wakati milio ya bundi inashambuliwa wakaenda kujificha nyuma ya polisi wale wale ambao walikuwa wanawaona wabaya! Baadhi ya watu wakagundua kuwa maneno makali dhidi ya Polisi na kuwapaka rangi ile ile polisi wote ni kutowatendea haki na kuhatarisha usalama wa jamii yenyewe.
Sasa, kama itatokea – na nadhani inaweza ikawa hivi – CHADEMA na vyama vya upinzani vikaruhusiwa kuandamana au wakalazimisha kuandamana na polisi wakaamua kuwaacha waandamane bila ulinzi wowote hivi ikitokea watu miongoni mwao wakaanzisha vurugu siyo kwamba viongozi hao hao wa CHADEMA watakuwa wa kwanza kulalamika kwanini “Polisi” wale wale wabaya hawakutoa ulinzi? Na kama polisi wataamua kutoa ulinzi halafu watu wakawashambilia Polisi kwa sababu wameaminishwa kuwa ni wabaya wao kwa vile wamekuwa ni “kitengo cha CCM” hawa viongozi wa upinzani watakubali kuwajibika au wataendelea kuona kuwa wao hawahusiki katika kupandikiza hii chuki dhidi ya polisi nchini?
Maneno makali – ambayo wengine labda wanayaona ni rahisi kuyatoa – dhidi ya Polisi wetu hayajengi upinzani wala kuimarisha uhusiano bali yanazidisha chuki na kwa namna fulani yanajibu swali lao la “nani ameleta chuki hii”. Ingawa wanaweza kudhani kuwa kile kinachoonekana chuki dhidi ya polisi kinatokana na Serikali au CCM wakati umefika kwa viongozi wa upinzani wenyewe nao kujiangalia kama kauli zao na maneno yao dhidi ya Polisi hayachangii katika kuongeza chuki dhidi ya polisi.
Leo hii, kama viongozi hawa wa upinzani nchini mwetu nao wakipatwa na majanga na wakatafuta msaada wa polisi hivi wataelewa polisi wakiamua kuwaziria na kugoma kwenda kutoa msaada kwa vile wanachangia kupandikiza chuki dhidi ya polisi kuna mtu ataelewa?
Ukweli ni kuwa wapo watu ambao wanachukia polisi na wataendelea kuchukia polisi kwa sababu zao. Lakini kwa jamii inayojidai kutaka kujenga utawala wa kidemokrasia haiwezi hata kidogo kuvumilia au kuchekea matukio dhidi ya polisi ati kwa vile polisi wakati mwingine wanapotekeleza majukumu yao wanaweza kujikuta – kihalali au kwa makosa – wamesababisha madhara ya watu au vitu.
Mtu anayeshambulia polisi na hata kuwaua anakuwa katika uhalali gani wa kutekeleza jambo gani ambalo linaweza kumuweka sawa na askari polisi ambaye akitekeleza majukumu yake akiamini anailinda jamii akajikuta amemuua mtu au kumdhuru? Polisi anayefanya hivyo hata kwa makosa kuna taratibu za kisheria na kijeshi za kuchunguza jambo hilo (kama tulivyoona katika baadhi ya kesi); lakini Raia anapomuua Polisi ni kwa vipi tunaweza kudhani naye anatekeleza jambo fulani kiasi kwamba kuna moral equivalency kati yake na polisi?
Binafsi, nakataa na nalaani vikali kauli za kisiasa ambazo zinaonekana kuchochea baadhi ya wananchi kuchukia polisi n ahata kujaribu kufafanua ni kwanini mauaji ya polisi yanaweza kuwa yanahusiana na hali ya kisiasa nchini. Kufanya hivyo ni kutokuwa wawajibikaji na watu ambao wanajaribu kufafanua vitendo viovu ili kuhalalisha au kupata magoli fulani ya kisiasa.
Kama demokrasia hatuwezi kusimama bila kuwa na vyombo vya usalama ambavyo wananchi wake siyo tu wanavitegemea lakini wanasimama navyo.
Ni matumaini yangu askari hawa waliouawa watachukulia kama mashujaa ambao majina yao yatakumbukwa na Serikali iwazike siyo tu kwa heshima za kijeshi bali pia kwa heshima za mashujaa ambao waliuawa wakiwa kazini kuitumikia Taifa lao hata kwa damu yao. Ni matumaini yangu, misafara ya mazishi yao itaongozwa na makundi ya polisi na raia wema waliojipanga barabarani kuenzi utumishi wao na kuona fahari kwa vijana wao hawa na kuwapa moyo polisi wengine kuwa mamilioni ya Watanzania bado wako nyuma ya polisi wao na wanawategemea pamoja na changamoto zote zilizopo.
Wakati umefika tuanze kuwakatalia viongozi wa kisiasa kupandikiza chuki au kutetea chuki dhidi ya polisi kwa kisingizio au sababu yoyote ile.
Niandikie: Mwanakijiji@klhnews.com
Tatizo la Polisi kuuawa na kunyang'anywa silaha halikuanza katika tukio hili. Yamekuwepo tangia utawala uliopita na ni tatizo ambalo wananchi tuna hamu ya kujua kulikoni. Hizi kauli zinazotolewa na viongozi (wa pilosi na kisiasa) hazitupi matumaini kwa sababu hazielezi hasa kiini cha matukio haya. Kumbuka hata Rais wetu wa sasa alishalizungumzia na kuwashangaa Polisi kuvamiwa na kunyang'anywa silaha. Ni vizuri pia kabla ya kuanza kutupiana lawama na kuhimiza utii, pande zote zinatakiwa kuheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Bila hayo kufanyka kutakuwa na pande zinazoshangilia upande mwingine ukiumia. Hii ni hulka tu ya ubinadamu.Na. M. M. Mwanakijiji![]()

Huku ni kutokwa na akili mwana kijiji ameongea mambo ya msingi hebu tuwe wakweli.mtahangaika sana kutafutia maneno ya magufuli ya zuio la mikutano uhalali lakini ukweli upo pale pale yupo against na sheria,taratibu za nchi.chuki dhidi ya polisi wanasababisha polisi wenyewe kwa kutotumia utashi katika kulinda haki za raia.Tukutane September 1
Msaliti na mnafiki huwa hasikilizwi na watu wanaojitambua. Endelea kuramba miguu ya watawala.
kwa watu ambao mnaandika ili kupata comments nyingi au ili muone mnaungwa mkono na kina nani basi mara zote mtajitahidi kusema vitu vinavyovutia watu!Soma comment zote mzee mwana kijiji, angalia comments zinazo ku support na zinazo pingana na andiko lako.
Piga picha miaka mitano au kumi taka jf ianzishwe jinsi watu to alivyokuwa wapi comment kwenye post zako.
Mwisho hi jitathmini where you are heading in your political analysis.