Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Vizuri lakini kama jambo lingetokea baya nani angelaumiwa? Unafikiri polisi wetu hawa wakiacha kufanya majukumu yao mitaani kila mtu atakuwa na amani?

Acha upotoshaji wewe nimekuambia ni mmoja kati ya watu wanaoneza chuki kwenye jamii, aidha kwa makusudi ama kwa bahati mbaya. Hakuna anayepinga polisi kutekeleza wajibu wao, bali watu wanapinga polisi kufanya kazi kwa upendeleo wa wazi. Mifano nimekupa kwenye ile post yangu tofauti ya utendaji wa polisi kwenye ule mkutano wa ccm na huu wa juzi wa cuf.
 
Ikiwa kampeni ambazo ndio chanzo kikuu cha kukamata madaraka ya nchi na dola zilipita salama iweje uwe na hofu na maandamano ambayo hayahusiani na chochote kile cha kukimbilia Ikulu. Matokeo yalitangazwa na watu wakatulia kama vile hakukuwa na uchaguzi. nanukuu: "Huu ndio uongozi wa ovyo kabisa tangu nchi hii ipate uhuru"

Musiwalazimishe Raia muliokuwa mumewazoea wawe tofauti, Musiwalazimishe viongozi wa siasa waliokua tofauti nanyi wakatafuta haki kwa njia ambazo si nzuri, Mumekaa madarakani muna amani ya kutosha, munaimba, munacheza, kwa nini na wenzenu wasiimbe? kwanini na wenzenu wasicheze? Siasa nchi hii iko juu na ni nyinyi wenyewe ndio mlioipandisha kama mnakusudia kuishusha au kuifuta kabisa fuateni sheria na badilisheni vipengele vya katiba na sio kutumia nguvu kubwa kwa wananchi wasio na hatia.
 
You guy, hutahalalisha batili kuwa halali. Zuio la mikutano ni kimyume cha sheria na katiba. Ndug wa Mwangosi unadhani watakuelewa hayo uliyoandika hapo? Hujafikwa ndio maana unajisemea tu!
Na ndugu wa hawa waliokufa jana wao watakuelewa
 
Huyu mwanakijiji dk za mwisho huku ndo anazid kupoteza kila hoja yake lazm ibume tu haelewek maish
yanaend kas kuliko kawaid
 
Kauli za Msigwa na Mtatiro zote zina ujumbe wa rambirambi kwa polisi waliopoteza maisha na familia zao huku zikiambatana na maoni yao kuhusu wapi kama taifa tunaelekea ikiwa baadhi ya Watanzania wanafurahia mauaji ya polisi na rai kwa serikali kutumia intelijensia yao kupambana na uhalifu halisi badala ya kuminya demokrasia. Sijaona tatizo hapa. Labda tatizo linaweza kuwa wewe Mwanakijiji kujaribu kutumia tafsiri yako potofu kupindisha ukweli.
 
Ila hakuna mtawala aliyekufa wamekufa polisi wakiwa kazini.
Mkuu mimi pia nimelaani tukio la askari wetu kuuawa lakini wanasiasa wengi wa upinzani wakatoa angalizo kwa polisi wajitathimini upya. Inakuwaje watu wanashangilia vifo vya wenzao? Lazima kuna tatizo hapo. Sasa huyu mnafiki anaokoteza maneno kutaka kuchafua wapimzani waliotoa maoni yao kuhusu tukio hilo. Ndio maana nimemshambulia yeye na si hoja zake kwasababu namjua huyo ni mnafiki tu.
 
Kweli Mzee Mwanakijiji umepuuzwa sasa!

Sizioni Comment za wale wote mlioanza nao Safari moja toka JF inaanzishwa.
 
Huku ni kutokwa na akili mwana kijiji ameongea mambo ya msingi hebu tuwe wakweli.
Hili tukio linahusikaje na mambo ya kisiasa unataka kuniambia kuwa hao majambazi wametumwa na Chadema ili kuwaogopesha polisi wasiendelee kutii amri inayotolewa na viongozi wao?

Hebu turudi nyuma kidogo pamoja na mifano aliyotoa mwanakijiji lakini tunayo mifano hai ambayo imepata kutokea hapa kwetu.
Wakati hawa majambazi walipovamia vituo vya Mkuranga, Sitaki shari, Ikwiriri, Gaeita na kuua asikari wasio na hatia, na hata kuchinja wananchi wasio kuwa na hatia huko Tanga kulikuwa na zuio gani la polisi kwa vyama vya kisiasa?

Hii nchi ni nchi tuyoishi sote usifikiri kuwa unaishi nchi nyingine tofauti kwamba kukitokea vurugu kwamba wewe utasalimika.
Kumbuka kuwa vita havina macho na wala havichagui angalia hali ilivyo leo Iraqi, Libya, Syria,Soamlia na sehemu nyingine nyingi zilizokumbwa na vurugu hizi za vita ambazo chanzo chake kimeanzia katika hii mitandao.

Mimi nasema mauaji haya yana inshara za kigaidi maana ninavyoamini mimi binafsi ni kuwa jambazi lengo lake kubwa ni kwama akiua basi ni pamoja na kupora pesa au vitu vyenye thamani lakini leo tunaona wanaua na kupora silaha.
Hawa lazima watakuwa na malengo mengine tofauti na haya tunayoyafikiria kila mtu anao uhuru wa kutoa mawazo yake lakini mawazo yawe katika misingi ya kibinadamu.
Hivi leo hii Lema au Msigwa ametokewa na bahati mbaya yeyote ambayo inahitaji msaada wa kipolisi unadhani hao polisi watashughulikia tatizo katika hali gani?

Kiongozi uliyechaguliwa na watu na kuwakilisha watu unatakiwa kuwa na hekima na busara za hali juu ili hao unaowawakilisha uwejengee imani ya kukuamini bila kujali itikadi ya chama chako.
Natumai utakuwa ulimsikiliza kamishina Marijani jana.
 
Nilikuwepo Mbezi Tenkibovu kituo cha OilCom tangu saa 4.50 hadi saa 6.38. Kilichonivutia ni Polisi wanne waliokuwepo pale . Kwa Muda usiozidi masaa mawili, hawa Polisi walisimamisha magari 87, na karibia wote wamepigwa faini Kwa kuandikiwa risiti.

Magari yaliyokuwa yanapanda mlima tena yenye spidi ya kawaida said a, yalikuwa yanasimamishwa hovyo hovyo ambao hawakuwa na spidi walilazimishiwa makosa mengine na kuandikiwa makosa, alikuwa na kila kitu, ila a kaambiwa kioo cha nyuma kimepasuka. Kama nchi , uonevu kama Itafika sehemu haitavumilika, maana siyo kila anayeendesha Gari Ana hela za kulipia faini. Makosa yawe ya kweli siyo ya kulazimisha. Nimesikitishwa sana, maana nilisogea Kwa muuza mahindi na kujionea Kwa ukaribu uonevu wa hawa watu.

Kuna mama Kalia akisema Kwa nini uonevu kama huu? Na kweli huyu mama alikuwa anaendesha IST Kwa mwendo wa kawaida tu
20170305_121511.jpg
 
Makosa ya barabarani ni moja ya chanzo cha mapato cha serikali hii ya mwendo kasi,makusanyo yameyumba na ndiyo maana zile mbwembwe za kutangaza makusanyo ya serikali zimesimama kwa takribani miezi miwili sasa.Tupo hatua za mwisho za kuhitimu "darasa la kusoma namba"kwa kiswahili,siku chache zijazo tutaanza muhula mpya wa kusoma namba kwa kisukuma.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Nilikuwepo Mbezi Tenkibovu kituo cha OilCom tangu saa 4.50 hadi saa 6.38. Kilichonivutia ni Polisi wanne waliokuwepo pale . Kwa Muda usiozidi masaa mawili, hawa Polisi walisimamisha magari 87, na karibia wote wamepigwa faini Kwa kuandikiwa risiti.

Magari yaliyokuwa yanapanda mlima tena yenye spidi ya kawaida said a, yalikuwa yanasimamishwa hovyo hovyo ambao hawakuwa na spidi walilazimishiwa makosa mengine na kuandikiwa makosa, alikuwa na kila kitu, ila a kaambiwa kioo cha nyuma kimepasuka. Kama nchi , uonevu kama Itafika sehemu haitavumilika, maana siyo kila anayeendesha Gari Ana hela za kulipia faini. Makosa yawe ya kweli siyo ya kulazimisha. Nimesikitishwa sana, maana nilisogea Kwa muuza mahindi na kujionea Kwa ukaribu uonevu wa hawa watu.

Kuna mama Kalia akisema Kwa nini uonevu kama huu? Na kweli huyu mama alikuwa anaendesha IST Kwa mwendo wa kawaida tuView attachment 476989
Watanganyika hata wakafanywa nini wataridhiya tu
 
Makosa ya barabarani ni moja ya chanzo cha mapato cha serikali hii ya mwendo kasi,makusanyo yameyumba na ndiyo maana zile mbwembwe za kutangaza makusanyo ya serikali zimesimama kwa takribani miezi miwili sasa.Tupo hatua za mwisho za kuhitimu "darasa la kusoma namba"kwa kiswahili,siku chache zijazo tutaanza muhula mpya wa kusoma namba kwa kisukuma.

Naona na yeye ameanza kujisomesha number
 
hao police ni wajanja tu sio kwamba hiyo hera inaenda selikalini. hile machine ukiingiza number ya gari inatoa details kama hiyo gari inadaiwa. hile karatasi sio reciti. anaanza kukuomba rushwa kwakusingizia gari lako kudaiwa sana. wanao kuona wanafikiri Katoza faini kumbe hamna ni hongo kama kawaida tu hamna kitu
 
ukute umeandika ili kutafuta huruma ya hadhira, hayo magari 87 yote yamesimamishwa kwa kuonewa? tatizo umefikia hitimisho lako haraka mno na kuulaum upande, ingefaa kama ungetaja makosa yao na kuyajadili kulingana na sheria za "traffic and road safety regulations'
 
Nikiangalia mijadala mingi ndani ya JF (na hoja zangu zikiwemo) napata hofu sana kama kunajengwa dhana kwamba ni halali kupambana na jeshi la Polisi ama pia ni halali kuamrisha jeshi la Polisi kupambana na wananchi hata kama wakati mwingine ni wananchi wasio na hatia.

Kunajengwa chuki kubwa sana kwa wananchi dhidi ya jeshi la Polisi kwa jinsi linavyotumika. Kwa watu wa vyama vya upinzani wanajenga taswira kwamba Jeshi la Polisi linatumiwa na CCM dhidi yao. Na CCM nao wanaona ni halali Jeshi la Polisi "kuwashughulikia" wapinzani wao wasiotaka kutii "mamlaka halali".

CCM na wapinzani wao kisiasa ni wananchi wa Tanzania wanaoishi kwenye jamii yetu. Kama wapinzani wanapouawa Polisi wanaona ni afadhali na wao "kimewapata" na CCM nao wakiona ni "halali" kutumia Jeshi la Polisi dhidi ya wapinzani wao. Basi si CCM wala wapinzani wao watakaochukiwa na Polisi bali ni Polisi watakaochukiwa na Makundi hayo mawili ingawa itakuwa kwa wakati tofauti.

Siku CCM wakiona wapinzani wao wanaandamana na kufanya mikutano bila ya kuzuiwa na Polisi, lazima wataona Polisi limekuwa Jeshi legelege na watawachukia. Na siku wapinzani nao wakizuiwa kufanya mikutano na maandamano, wataona Jeshi la Polisi linatumika kisiasa.

Ili tusijenge chuki dhidi ya Jeshi la Polisi ni lazima tuliache Jeshi letu la Polisi lifanye kazi zake kwa weledi kwa kuzingatia sheria iliyounda jeshi hilo na taratibu zilizopo!
 
Back
Top Bottom