Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Tusikubali Wanasiasa Wapandikize Chuki Dhidi ya Polisi

Kuna chanzo cha jeshi letu kuwa hivyo. Ama ni upungufu wa maadili ama ni hali duni za maisha yao na maslahi yasiyozingatia ugumu wa kazi yao wanayoifanya!!
Ukweli ni kuwa CCM imelitumia Jeshi la Polisi bila kufuata maadili wala sheria kuwaumiza raia wa Tanzania kwa njia zisizo za kimaadili wala sheria ili mradi wao wakidhani raia hao ni wapinzani tu. Matokeo ni Polisi kukosa weledi na kuacha kuwaheshimu raia wanaowalipa mishahara, wao wakiamini wanalipwa na viongozi wa ccm na serikali. Haya yamejenga chuki kubwa kati ya Polisi na raia. Sasa matukio kama ya Kibiti ni kutonesha jeraha linalovuja usaha tayari.
 
IGP Mangu ameshindwa kabisa kujenga mahusiano kati ya Polisi na raia. Nadhani pengine ndio worst IGP TZ never had. Amerithi madaraka jeshi likiwa na nidhamu na weledi wa hali ya juu. Yale mambo ya kutumia nguvu na kufungisha mashati yalishapitwa na wakati sasa yanarudi. Matumizi ya nguvu bila weledi na siri kubwa za operesheni za Polisi inaakisi wazi aina ya uongozi wake na bila shaka nyuma yake kuna uvunjaji mkubwa wa sheria. Na hapo ndipo panapojenga wasiwasi wa wananchi juu ya usalama wao na mali zao. Wanataka wananchi watoe taarifa za uhalifu wakati wao wameshindwa kujihakikishia usalama wao.Vituo vya Polisi vinafungwa saa kumi na mbili jioni kwa kuwa tu Polisi haijiamini. Je wale wenye vibanda vya M-pesa na tigo pesa watafanyaje?

Na Waziri Mwigulu inabidi ajiuzulu. Zaidi ya askari wetu kumi wamepoteza maisha. Nchi imefikia kipindi ambacho usalama wetu wa ndani umekuwa mdogo kuliko kipindi chote baada ya uhuru bado mtu kanga'ang'ania cheo.
 
denoo49 chanzo ni tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi bado fikra zetu zikabaki kwenye mfumo wa chama kimoja tena kinachofuata misingi ya vyama vya kishoshalisti na kikomunisti. Mfumo huo wa siasa viongozi hulazimisha waonekane wana akili kuliko wanaowaongoza na sharti kuabudiwa na wananchi.

Kwa bahati mbaya binadamu kumwabudu binadamu mwenzake si kazi rahisi bila ya kulazimishwa., hapo ndipo jeshi la Polisi lilipoanza kupotoshwa. Na hili usidhani lipo CCM tu, kama fikra zetu hazitaendana na mfumo wa vyama vingi, basi kila chama kikiwa madarakani kitataka kutumia Polisi dhidi ya wapinzani wao.

Kimweri una hoja lakini ukweli wa mambo ni lazima mfumo wa kuendesha Jeshi letu la Polisi ni kwanza ubadilishwe. Kwa mfano kuwa OCD ama RPC si kutokana na cheo pekee bali pia ni hisani ya IGP alieko madarakani wakati husika. Sasa ni OCD ama RPC gani yupo tayari kuhamishwa na kurudishwa Makao Makuu kwa kushindwa kutii amri za mabosi wao ambao ni wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na usalama wa maeneo yao?
 
Jeshi la polisi kutumika ndio tatizo..

Kama lingekuwa linafanya kazi zake independently kusingekuwa na chuki...

Tatizo Tops wao ni wanasiasa...!

Nahisi ukishakuwa polisi huitaji kuogopa lawama na chuki tena.
 
Polisi itakuwa free siku wakifanya kazi wao kama wao...

Though ni ngumu sana..
Ni ngumu sana kwani ili wafanye kazi zao wakiwa huru dhidi ya wanasiasa inabidi wanasiasa hao hao ndiyo watunge sheria itakayokata minyororo ya wanasiasa kwa Polisi. ITAWEZEKANA?
 
Nikiangalia mijadala mingi ndani ya JF (na hoja zangu zikiwemo) napata hofu sana kama kunajengwa dhana kwamba ni halali kupambana na jeshi la Polisi ama pia ni halali kuamrisha jeshi la Polisi kupambana na wananchi hata kama wakati mwingine ni wananchi wasio na hatia.

Kunajengwa chuki kubwa sana kwa wananchi dhidi ya jeshi la Polisi kwa jinsi linavyotumika. Kwa watu wa vyama vya upinzani wanajenga taswira kwamba Jeshi la Polisi linatumiwa na CCM dhidi yao. Na CCM nao wanaona ni halali Jeshi la Polisi "kuwashughulikia" wapinzani wao wasiotaka kutii "mamlaka halali".

CCM na wapinzani wao kisiasa ni wananchi wa Tanzania wanaoishi kwenye jamii yetu. Kama wapinzani wanapouawa Polisi wanaona ni afadhali na wao "kimewapata" na CCM nao wakiona ni "halali" kutumia Jeshi la Polisi dhidi ya wapinzani wao. Basi si CCM wala wapinzani wao watakaochukiwa na Polisi bali ni Polisi watakaochukiwa na Makundi hayo mawili ingawa itakuwa kwa wakati tofauti.

Siku CCM wakiona wapinzani wao wanaandamana na kufanya mikutano bila ya kuzuiwa na Polisi, lazima wataona Polisi limekuwa Jeshi legelege na watawachukia. Na siku wapinzani nao wakizuiwa kufanya mikutano na maandamano, wataona Jeshi la Polisi linatumika kisiasa.

Ili tusijenge chuki dhidi ya Jeshi la Polisi ni lazima tuliache Jeshi letu la Polisi lifanye kazi zake kwa weledi kwa kuzingatia sheria iliyounda jeshi hilo na taratibu zilizopo!

!
!
sina sababu ya kuwapenda polisi
 
Mbona umeandika kama upo nje ya mipaka ya taifa la Tanzania.
Kwani sheria za jeshi la polisi zinaelezaje kuhusu kukabiliana na "watuhumiwa"?
Umesema watuhumiwa kwa maana hiyo wana kibiti wote ni watuhumiwa?je hao wanawake wanaofanyiwa uchafu na hao jamaa zako nao ni watuhumiwa?tumia akili sio kufikilia kupitia eneo lako jengine.
 
We jamaa unajidai sana.Sijui unaringia nini hasa,unapata faida gani kuwaita binadamu wenako Nyumbu? Unajivunia UCCMM wako wakati hadi inakera.Uzi umeletwa,ume balance ila wewe unayejiona "malaika" unaona huu ni ujumbe wa hao Nyumbu!. Exposure kidogo zinawafanya mjione miungu na majiniazi kuliko hata akina Plato,Newton n.k
Mjumbe huyu ni wa kumpuuza maana ni mpuuzi.. Ukimjibu ndio anazidisha upumbavu na upuuzi wake. Jina lenyewe linaonyesha jinsi alivyo mpuuzi jamaa linajiita Nyani.
 
Umesema watuhumiwa kwa maana hiyo wana kibiti wote ni watuhumiwa?je hao wanawake wanaofanyiwa uchafu na hao jamaa zako nao ni watuhumiwa?tumia akili sio kufikilia kupitia eneo lako jengine.
Hakika umekufa umebakia kuoza tu na kunuka. Kabla ya ku quote post ya mtu, jitahidi uwe unatanguliza ufahamu wako kabla ya kiwiliwili chako.

Umejiuliza ni kwanini au nini kimepelekea nimemuuliza mleta uzi maswali hayo? Na unaposema ni jamaa zangu, unaweza kunionesha post yangu hata moja tu yenye kutetea hao Polisi.

OK, umesema kuna "wanawake wamefanyiwa uchafu huo", unaweza pia kutuwekea ushahidi hapa ili hao Polisi tuweze kuwaumbua kwa uchafu huo?
 
Nikiangalia mijadala mingi ndani ya JF (na hoja zangu zikiwemo) napata hofu sana kama kunajengwa dhana kwamba ni halali kupambana na jeshi la Polisi ama pia ni halali kuamrisha jeshi la Polisi kupambana na wananchi hata kama wakati mwingine ni wananchi wasio na hatia.

Kunajengwa chuki kubwa sana kwa wananchi dhidi ya jeshi la Polisi kwa jinsi linavyotumika. Kwa watu wa vyama vya upinzani wanajenga taswira kwamba Jeshi la Polisi linatumiwa na CCM dhidi yao. Na CCM nao wanaona ni halali Jeshi la Polisi "kuwashughulikia" wapinzani wao wasiotaka kutii "mamlaka halali".

CCM na wapinzani wao kisiasa ni wananchi wa Tanzania wanaoishi kwenye jamii yetu. Kama wapinzani wanapouawa Polisi wanaona ni afadhali na wao "kimewapata" na CCM nao wakiona ni "halali" kutumia Jeshi la Polisi dhidi ya wapinzani wao. Basi si CCM wala wapinzani wao watakaochukiwa na Polisi bali ni Polisi watakaochukiwa na Makundi hayo mawili ingawa itakuwa kwa wakati tofauti.

Siku CCM wakiona wapinzani wao wanaandamana na kufanya mikutano bila ya kuzuiwa na Polisi, lazima wataona Polisi limekuwa Jeshi legelege na watawachukia. Na siku wapinzani nao wakizuiwa kufanya mikutano na maandamano, wataona Jeshi la Polisi linatumika kisiasa.

Ili tusijenge chuki dhidi ya Jeshi la Polisi ni lazima tuliache Jeshi letu la Polisi lifanye kazi zake kwa weledi kwa kuzingatia sheria iliyounda jeshi hilo na taratibu zilizopo!
Binafsi nalichukia geshi la polis
 
Sidhani kama hawa nyumbu wanaelewa!
Nyani Ngabu,kuna siku mke wangu alikuwa anacheka sana,nikamuuliza kulikoni,akaniambia yupo JF Jukwaa la Hoja Mchanganyiko,anacheka comment ya Nyani Ngabu,nikamwambia unajua NN ni classmate wangu Mlimani P.S.!? Kilichofuata ni mshangao wa kuamini kama Mlimani ya back then iliweza kuwa na mwanafunzi "kilaza to the extend that hatambui jinsi yake sahihi aliyoumbwa nayo ni ipi". That is my wife's view on you "fella". Na uzuri mke wangu naye ni ex- Solomon Mahlangu P. S ( sasa ni Chief A. Luthuli P. S.)
Kwa ujumla,never call anyone asiye upande wako "nyumbu" au jina lolote lile baya kwa sababu huna integrity ya kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom