Njiapanda: Mzee anataka turudi kijijini wakati mama anataka tubaki mjini

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,731
3,372
Mzee alistaafu miaka michache iliyopita.

Amejenga mjini hapo familia ilipo sasa hivi

Kajenga pia kijijini kwake na ana vimiradi vyake huko kijijini.

Sasa kumetokea tafrani hapa kati yao maana Mzee anataka aihamishie familia kijijini sasa kimbembe mke wake yani maza anataka familia iendelee kubaki mjini.

Hii imekuwa shida sana kwa watoto kuamua wasimame upande upi. Watoto wamegawanyika nao. Wapo walio simama upande wa mzee na wengine wanaomsapoti maza.

Mpasuko ni mkubwa. Hali ni tete kwakweli.
 
Mzee alistaafu miaka michache iliyopita.

Amejenga mjini hapo familia ilipo saivi...
Mshua yupo sahihi bora arudi kijijini maana kula atakuwa busy na miradi ya ufugaji na ukulima huku anakuwa anakula vitu natural na huku anakuwa kama anafanya mazoezi kuliko kubakia mjini na kushinda kutwa nzima kwenye vijiwe vya kahawa huku akicheza bao hadi giza linazama.

Anarudi home kwenda kula na kulala ndo maana wazee wengi wastaafu mjini wamekuwa wambea kama wanawake maana muda mwingi wanashinda vijiwe vya kahawa nakuanza kuwachambua kila msichana anaye pita.

Muache aende kijijini akapige kazi au unataka hadi afie town ndo muingie garama mara mbili kumpeleka kijijini mwache aende mwenyewe akiwa hai
 
Mnataka kubaki mjini je kuna namna gani ya kuendesha maisha maana umesema miradi iko kijijini na mzee amestaafu? Pesa ya kuhudumia familia mnategemea itoke wapi?

Au wazee watakuwa wanajishughulisha na nini iwapo mnabaki mjini au mtalima lami...joke!

Uendeshaji wa miradi ukoje huko kijijini? Maana kuna miradi mmiliki ukiwa mbali uzalishaji wake unakuwa hauna tija. Mzee yuko sahihi rudini kijijini akasimamie miradi yake aendeshe familia!

Nje ya mada umri wa watoto una range kuanzia miaka mingapi mkubwa hadi mingapi kwa mtoto mdogo?
 
Mzee alistaafu miaka michache iliyopita.

Amejenga mjini hapo familia ilipo saivi

Kajenga pia kijijini kwake na ana vimiradi vyake huko kijijini...
kuna shida gani mkiishi mjini lakini pia mkaishi kijijini? mathalan kipindi cha kilimo na mavuno, anaishi kijijini wakati ulibaki anakua anaishi town..

kwan nn mbaya...
 
Back
Top Bottom