Tusiende Sombetini

Tusiende Sombetini

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Kata nne kule mkoani Arusha,nilisema kikaoni na hapa JF kwamba nisingekwenda Arusha. Na ni kweli.Sijaenda. Nilisema kuwa CCM yetu haikuwa na nafasi hata ya kushinda kata moja. Nilibezwa,nilidhihakiwa,nikadharauliwa na kukosolewa. Matokeo yalionekana.Tukapigwa 4-0.

Uchaguzi mdogo mwingine umeshatangazwa na Tume ya Uchaguzi iliyo chini ya Jaji Damian Lubuva. Imesema kuwa Februari kutakuwa na Uchaguzi wa Madiwani wa Kata 27. Kati ya hizo,1 ni ya Arusha:Sombetini. Kule alikotokea Mawazo.Kule alikoacha uongozi Mawazo na kuhamia CHADEMA.Kule ambapo Mawazo na CHADEMA wana nguvu. Kule ambapo,tayari CHADEMA imemsimamisha mtu maarufu pia: Ally Bananga; M-CCM wetu wa zamani.

Kuna Kata 27.Ni heri CCM yetu ijielekeze kata 26. Ijielekeze kule ambapo tunaweza kupita bila kupingwa.Kule ambapo wananchi bado wanakitambua na kukipenda 'chama cha Nyerere' pasipo kufuatilia hasa kinachofanya na jinsi kinavyowahudumia. Kule ambapo CCM huchaguliwa kwa rangi yake;takrima yake;'mbinu zake' na 'mizengwe yake'. Lakini si Sombetini.

Twende kule ambapo idadi ya wapigakura yaweza kubadilishwa bila ya vikwazo vyovyote. Kule ambapo majina ya waliojiandikisha yaweza kuwa yoyote yale na hatuhojiwi.Twende kule ambapo mgombea wetu aweza kutangazwa mshindi 'kwa dharura na chini ya ulinzi mkali'.Kwakuwa watu wanakipenda chama chetu.Kwakuwa watu wanapenda CCM na viongozi wake.Kwakuwa daftari la kupigia kura laweza kutupa ushindi.Kwakuwa wananchi wanaweza 'kuzuiwa' kwenda kupiga kura zao. Lakini si Sombetini.

Sombetini tusiende. Hakuna haja. Twendeni kwingineko katika Kata 28. Hima chama changu,tusonge mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Waeleze ukweli mkuu,hapa hata mgombea wa maccm sombetini amewaambia hatatumia hata mia yake kwani atafilisika bure ilhali baada ya uchaguzi watamwacha akitafuta upya maisha.
 
Tupatupa umesahau na ile kata moja kule Bunda mlikokosa mwakilishi je huko mtakwenda tu kwa vile ni kwa bosi wa sera na utawala haramu au??? Tanzania ya leo sio ya Ccm na mabavu tena.RIP Ccm
 
Mzee Tupatupa asante kwa kuliona hilo, ila umesahau Bunda! Jaribu kukaa na Lizabon, na wengine wengi wa Lumumba uwashawishi. Vichwa vyao vigumu kwa kuwa bado wanaamini wana dola, wana wakurugenzi, wana wakuu wa wilaya hivyo wembe ni ule ule......

Angalia tu wasije wakadai wewe ni mamluki!
 
_wazee wa ushindi ni lazima
_ushindi wa kishindo
_lazima tuibuke washindi
___ccm ccm ccm
 
Mhh,Sombetini mbona Mheshimiwa diwani Ally Bananga anasubiri kutangazwa tu'
 
Wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Kata nne kule mkoani Arusha,nilisema kikaoni na hapa JF kwamba nisingekwenda Arusha. Na ni kweli.Sijaenda. Nilisema kuwa CCM yetu haikuwa na nafasi hata ya kushinda kata moja. Nilibezwa,nilidhihakiwa,nikadharauliwa na kukosolewa. Matokeo yalionekana.Tukapigwa 4-0.

Uchaguzi mdogo mwingine umeshatangazwa na Tume ya Uchaguzi iliyo chini ya Jaji Damian Lubuva. Imesema kuwa Februari kutakuwa na Uchaguzi wa Madiwani wa Kata 29. Kati ya hizo,1 ni ya Arusha:Sombetini. Kule alikotokea Mawazo.Kule alikoacha uongozi Mawazo na kuhamia CHADEMA.Kule ambapo Mawazo na CHADEMA wana nguvu. Kule ambapo,tayari CHADEMA imemsimamisha mtu maarufu pia: Ally Bananga; M-CCM wetu wa zamani.

Kuna Kata 29.Ni heri CCM yetu ijielekeze kata 28. Ijielekeze kule ambapo tunaweza kupita bila kupingwa.Kule ambapo wananchi bado wanakitambua na kukipenda 'chama cha Nyerere' pasipo kufuatilia hasa kinachofanya na jinsi kinavyowahudumia. Kule ambapo CCM huchaguliwa kwa rangi yake;takrima yake;'mbinu zake' na 'mizengwe yake'. Lakini si Sombetini.

Twende kule ambapo idadi ya wapigakura yaweza kubadilishwa bila ya vikwazo vyovyote. Kule ambapo majina ya waliojiandikisha yaweza kuwa yoyote yale na hatuhojiwi.Twende kule ambapo mgombea wetu aweza kutangazwa mshindi 'kwa dharura na chini ya ulinzi mkali'.Kwakuwa watu wanakipenda chama chetu.Kwakuwa watu wanapenda CCM na viongozi wake.Kwakuwa daftari la kupigia kura laweza kutupa ushindi.Kwakuwa wananchi wanaweza 'kuzuiwa' kwenda kupiga kura zao. Lakini si Sombetini.

Sombetini tusiende. Hakuna haja. Twendeni kwingineko katika Kata 28. Hima chama changu,tusonge mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Nimekupa like kwa upevu wa mawazo na uchanganuzi mzuri lakini nahisi wewe ni "Deep cover CDM operative"??!! nimekushtukia Bro! you sound too good to be genuine!
 
ingekuwa vizur sana watanzania bila kujali chama tukawa wakweli kama wewe.
 
Huyu gambw anaona mbali sn, ni wachache wenyekuona mbali km huyu gamba
 
Tupa Tupa umekidhalilisha chama. utasemaje maneno ya kimafumbo lakini yenye ukweli namna hii?
 
Mzee tupatupa ni vizuri kuwashauri wenzio ila umesahau Bunda kata ya nyasura.kule nasikia meneja kampeni ni yule kiboko wa chenkapa alafu anahamia kule na timu yake nzima ya cdm msoma mjini.moto wa pale uspime bora wa sombetini.
 
wasivyo na aibu watakuibukia na matusi mengi maana hawapendi kuambiwa ukweli
 
Acheni kuimba wembe ni ulele........Shauri yenu utawakata.JK
 
ccm wana KAZI Kubwa sombetii, labda wapeleke baraza lote la mawaziri na rais akiwemo...
 
Kumbe bado lumumba inayo hazina ya vijana wenye upeo wa kuona mbali kama wako mkuu tupatupa
 
Wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Kata nne kule mkoani Arusha,nilisema kikaoni na hapa JF kwamba nisingekwenda Arusha. Na ni kweli.Sijaenda. Nilisema kuwa CCM yetu haikuwa na nafasi hata ya kushinda kata moja. Nilibezwa,nilidhihakiwa,nikadharauliwa na kukosolewa. Matokeo yalionekana.Tukapigwa 4-0.

Uchaguzi mdogo mwingine umeshatangazwa na Tume ya Uchaguzi iliyo chini ya Jaji Damian Lubuva. Imesema kuwa Februari kutakuwa na Uchaguzi wa Madiwani wa Kata 29. Kati ya hizo,1 ni ya Arusha:Sombetini. Kule alikotokea Mawazo.Kule alikoacha uongozi Mawazo na kuhamia CHADEMA.Kule ambapo Mawazo na CHADEMA wana nguvu. Kule ambapo,tayari CHADEMA imemsimamisha mtu maarufu pia: Ally Bananga; M-CCM wetu wa zamani.

Kuna Kata 29.Ni heri CCM yetu ijielekeze kata 28. Ijielekeze kule ambapo tunaweza kupita bila kupingwa.Kule ambapo wananchi bado wanakitambua na kukipenda 'chama cha Nyerere' pasipo kufuatilia hasa kinachofanya na jinsi kinavyowahudumia. Kule ambapo CCM huchaguliwa kwa rangi yake;takrima yake;'mbinu zake' na 'mizengwe yake'. Lakini si Sombetini.

Twende kule ambapo idadi ya wapigakura yaweza kubadilishwa bila ya vikwazo vyovyote. Kule ambapo majina ya waliojiandikisha yaweza kuwa yoyote yale na hatuhojiwi.Twende kule ambapo mgombea wetu aweza kutangazwa mshindi 'kwa dharura na chini ya ulinzi mkali'.Kwakuwa watu wanakipenda chama chetu.Kwakuwa watu wanapenda CCM na viongozi wake.Kwakuwa daftari la kupigia kura laweza kutupa ushindi.Kwakuwa wananchi wanaweza 'kuzuiwa' kwenda kupiga kura zao. Lakini si Sombetini.

Sombetini tusiende. Hakuna haja. Twendeni kwingineko katika Kata 28. Hima chama changu,tusonge mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

tumewakamata kila idara kama viwavi. there's no safe heaven, na hasa kama mmefikia hatua ya kutegemea 'hila', badala ya sera, hamfiki popote.
 
Back
Top Bottom