Tusiende Sombetini

Tusiende Sombetini

CCM ijielekeze kule ambapo tunaweza kupita bila kupingwa.Kule ambapo wananchi bado wanakitambua na kukipenda 'chama cha Nyerere' pasipo kufuatilia hasa kinachofanya na jinsi kinavyowahudumia. Kule ambapo CCM huchaguliwa kwa rangi yake;takrima yake;'mbinu zake' na 'mizengwe yake'. Lakini si Sombetini.

Twende kule ambapo idadi ya wapigakura yaweza kubadilishwa bila ya vikwazo vyovyote. Kule ambapo majina ya waliojiandikisha yaweza kuwa yoyote yale na hatuhojiwi.Twende kule ambapo mgombea wetu aweza kutangazwa mshindi 'kwa dharura na chini ya ulinzi mkali'.Kwakuwa watu wanakipenda chama chetu.Kwakuwa watu wanapenda CCM na viongozi wake.Kwakuwa daftari la kupigia kura laweza kutupa ushindi.Kwakuwa wananchi wanaweza 'kuzuiwa' kwenda kupiga kura zao. Lakini si Sombetini.

Sombetini tusiende. Hakuna haja. Twendeni kwingineko katika Kata 28. Hima chama changu,tusonge mbele!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ujumbe mzito sana huu. Hapa wanafiki kama kina Pasco na Manyerere Jackton hutawaona wakiweka mguu
 
Last edited by a moderator:
Waeleze ukweli mkuu,hapa hata mgombea wa maccm sombetini amewaambia hatatumia hata mia yake kwani atafilisika bure ilhali baada ya uchaguzi watamwacha akitafuta upya maisha.

Tupatupa umesahau na ile kata moja kule Bunda mlikokosa mwakilishi je huko mtakwenda tu kwa vile ni kwa bosi wa sera na utawala haramu au??? Tanzania ya leo sio ya Ccm na mabavu tena.RIP Ccm

ingekuwa vizur sana watanzania bila kujali chama tukawa wakweli kama wewe.

ccm wana KAZI Kubwa sombetii, labda wapeleke baraza lote la mawaziri na rais akiwemo...

Sombetiniiiiii

Bwanaeee tuachieni Sombetini yetu hamuiweziiii !!!!!! wajanja wako hapa etii
 
Ujumbe mzito sana huu. Hapa kina Pasco na Manyerere Jackton hutawaona wakiweka mguu
Ni kweli hapa sitii mguu, hiki ni kidole tuu, hapa sitii mguu, somo la Arumeru limenitosha.
Wito wangu kwa Chadema wasimamishe kila nafasi no matter what, kuna strong hold za CCM lakini CCM imechokwa mpaka basi, hata ukisimamisha jiwe, jiwe litapita.
Pasco
 
Pasco ni maneno yako haya au kuna mtu amekumezesha na kusema kupitia wewe siamini.
 
Ukweli lazima usemwe.Liwalo na liwe! ha ha ha ha ha ha ha

Tupatupa wa Lumumba
 
wa
Pasco ni maneno yako haya au kuna mtu amekumezesha na kusema kupitia wewe siamini.
Wageni humu wamekuwa wengi, wale wa zamani wanamfahamu Pasco wa jf, ndie yule yule juzi jana na leo.
Pasco
 
tumewakamata kila idara kama viwavi. there's no safe heaven, na hasa kama mmefikia hatua ya kutegemea 'hila', badala ya sera, hamfiki popote.

Wasije Sombetini kwetu hapa kazi tuu. Hatutegemei 'hila' hapa Sera tuu.
 
Ni kweli hapa sitii mguu, hiki ni kidole tuu, hapa sitii mguu, somo la Arumeru limenitosha.
Wito wangu kwa Chadema wasimamishe kila nafasi no matter what, kuna strong hold za CCM lakini CCM imechokwa mpaka basi, hata ukisimamisha jiwe, jiwe litapita.
Pasco

JISEMEE UKWELI WAKI MWAYA...HATA KAMA UTAWAUDHI WENZIO WA KIJANI.. tehetehe teherrr...
 
Back
Top Bottom