Tusichotambua wengi wetu ni kwamba pesa za mkopo inazokopa Serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ni pesa zetu

Cyangungu

Member
Nov 7, 2019
45
54
Wengi wetu tumekuwa mabingwa wa kukejeli pale ambapo Serikali inapokopa pesa kwenye mabenki mbalimbali eti si pesa yetu ya ndani bali ni mkopo jambo ambalo si kweli!

Ukweli ni kwamba pesa inayokopwa na Serikali hurejeshwa kwa wale waliotukopesha kwa makusanyo yetu ya kodi kwa makubaliano ya muda waliokubaliana.

Kwa muktadha huo Serikali inapojinasibu kwamba inatekeleza miradi yake kwa pesa za ndani ni kweli na hakika wanafanya hivyo

Shime wa Tanzania tusipende kubeza kwa hata ambayo hatuna ukweli na hakika kwalo.
 
Wakati wa kukopa wanaotoa mkopo wana jina zuri la nchi rafiki au wadau wa maendeleo, wakianza tu kukumbushia madeni yao jina hubadilika gafla na kuitwa mabeberu.
 
Wakati wa kukopa wanaotoa mkopo wana jina zuri la nchi rafiki au wadau wa maendeleo, wakianza tu kukumbushia madeni yao jina hubadilika gafla na kuitwa mabeberu.
Jina la beberu huwa ni la hovyo sana sijui hilo jogoo linampanda nani sasa.

Bora hata wangeita mtamba kuliko beberu.
 
Cyangungu,
Kwa hiyo ukikopa bank ukaanza matumizi unamwambia mkeo ni pesa zako za mshahara? Acheni kulazimisha ili kuhadaa umma. Makusanyo tumeyaona na deni tunalifahamu, sasa hizo pesa za ndani ni zipi?
 
tatizo si mkopo pia ni haki kujua mkopo umetumikaje je umeenda sehemu husika je umefanya kile kilichokusudiwa maendeleo hayahusiani na siasa ila wabongo tunaingiza siasa hadi kwenye mambo ya msingi
 
Wengi wetu tumekuwa mabingwa wa kukejeli pale ambapo Serikali inapokopa pesa kwenye mabenki mbalimbali eti si pesa yetu ya ndani bali ni mkopo jambo ambalo si kweli!

Ukweli ni kwamba pesa inayokopwa na Serikali hurejeshwa kwa wale waliotukopesha kwa makusanyo yetu ya kodi kwa makubaliano ya muda waliokubaliana.

Kwa muktadha huo Serikali inapojinasibu kwamba inatekeleza miradi yake kwa pesa za ndani ni kweli na hakika wanafanya hivyo

Shime wa Tanzania tusipende kubeza kwa hata ambayo hatuna ukweli na hakika kwalo.

Internal funds = internally generated funds from own sources/normal operating activities. Loans by definition are external repayable funds.
Mtatunga hadi definitions zenu lakini zitabaki kuwa ni za kwenu peke yenu.
 
Back
Top Bottom