Tusiache kuombea wagonjwa, maskini, yatima wajane na wenye shida mbali mbali

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
ndugu mpendwa ukiwa mmoja waliobahatika kuiona siku ya leo
embu nenda kaombe kwa wajili ya wagonjwa

muuliz mungu umemfanyia nini auko muhimbili,..wale wa muhimbili wamefanya kosa gani..waombee mungu akawaponye kabisa..hospital sehemu ya kuzaa unaondokasi kufika na kuweka makao.....jiulize kwa nini umeona kwenye hiace ya ajali ya kongowe umempa nini mungu..hao waliokufa wamekosa nini...

ombea wajane
wapo wajane engi sana wana shida mbali mbali hasa wimbi la kuchukua mali zao wakati wako na watoto,..na wamechimba na waume zao..kataa hii hali dhambi kubwa,...

ombea YATIMA
awa awakupenda kutokuwa na baba wala mama shida na matatizo ama kwa bahati mbaya kumewakumba hayp..chukua jukumu la kuwaombe na kuwasaidia

MASKNI
Hawa nao awakupenda kuwa na shida kama hizo..waombee mungu akawatoe kwenye changa la macho la umskini wakapenye na wao siku moja mkapungiane kwenye setimila...

ukifanya hayo umekamilisha usemi dini ilio bora ni!!

MUNGU AKUBARIKI
 
I always pray for orphans na nikiwa na uwezo huwa nawachangia. Big Up Diddy kwa thread hii
 
Kweli ni vizuri kufanya hivyo, lakini hiyo tu haitoshi inatakiwa wakati mwingine kuwasaidia kwa chochote ulichonacho, pesa,mavazi, chakula,masomo.nk
 
Sio kuwaombea tu,hata kwenda kuwaona na kuwapa misaada mbalimbali kama pesa,madawa,vyakula,nguo,n.k
 
Lakini wasipelekewe nguo ambazo zimeshavaliwa

kwa nini?Dah,siamini great thinker unasema hili.Kuna nguo nyingine watu washazivaa ba ni wabongo lakini ni bado mpya kabisaaaaa.Tena watu wana masanduku hata kumi hadi washazisahau hizo nguo au zinawabana.Sasa kama mtu huna nguo na umepewa suti kali ukatae? Utakuwa huna shukurani/.Tatizo ni pale penye kutoa nguo zilizochoka au zisizochanika
 
Charity vyovyote vile lakini mimi si-sapoti kutoa kwa yatima nguo ambazo tumeshazivaa, kama kweli unataka kuwazawadia wazawadie kile ambacho siyo umeshakichoka
 
Charity vyovyote vile lakini mimi si-sapoti kutoa kwa yatima nguo ambazo tumeshazivaa, kama kweli unataka kuwazawadia wazawadie kile ambacho siyo umeshakichoka
Hata kama umeshakichoka,lakini kama bado kinalipa je? mbona nguo za mitumba zimechokwa na wazungu na tunazivaa na sisi si watoto yatima?
Dah hapa tutabishana mpka kesho,kwa hili bado sana kukubaliana na wewe.eniwei ngoja tuishie hapa................
 
Wala hatubishani Charity, lakini tuishie hapa na kila mmoja abaki na msimamo wake lakini point ya msingi ibaki pale pale kuwasaidia watoto yatima
 
Wala hatubishani Charity, lakini tuishie hapa na kila mmoja abaki na msimamo wake lakini point ya msingi ibaki pale pale kuwasaidia watoto yatima

Ni kweli Dk ICU.Nakutakia majonzi mema hapo kesho na sherehe njema ya ufufuo hapo mapema siku ya kwanza ya juma.Uwe na furaha na amani pamoja na familia yako yote.
Cha msingi zaidi naomba Yesu afe na wewe na atakapofufuka ufufuke nae.
Neno maalumu la sikukuu hii kwako ni katika;
Yak 1:27.
 
Asante sana Charity kwa neno maalum. Na mimi naomba nikupe neno kutoka katika Wathesalonike 4:9
 
Back
Top Bottom