Tuseme Ukweli: Masikitiko Yangu Vifo Vya Watanzania

Tuseme Ukweli: Masikitiko Yangu Vifo Vya Watanzania

Inauma sana....jamani hata kukarabati kijipande tu cha barabara amabcho ni korofi halafu waandike bajeti ya ukarabati wa barabara nzima,wale mpunga unaosalia wanashindwa?????Acha niishie hapo...RIP marehemu na poleni majeruhi
 
Ndio leo unagundua kuwa ajali za barabarani zinaua nyuma ya Malaria! Barabara za bongo ni machinjio na ni ubishi wa wanasihasa ndio unasababisha hivyo. Hao wanasiasa waache wahandisi na makandarasi wafanye kazi! Na wahandisi waache sihasa.
 
Umezunguka sana, wa kuwajibika ni mmoja tu na vyeo vya kupeana kindugu. Kwa mfano, waziri kivuli awajibike kwa lipi? Awajibike tu mmoja, asiishie kutuma salamu za rambi rambi, maana nakuambia pale kishamaliza kazi, salaamu za rambi rambi.
Huu uzembe haiwezekani rais aishie kutuma salaam za rambi rambi.
 
Kwa heshima na taadhima naomba ku "declare interest"; Mimi ni mwanachama hai wa CCM toka siku TANU na Afro Shirazi Party zilipounganishwa na kuwa chama kimoja cha kisiasa, kwa jina CCM.

Baada ya ku "declare interest"" naomba kwa heshima na taadhima Nawaomba Watanzania muelewe kuwa Nimeumia na nimeumizwa zaidi baada ya kusikia "ajali" iliyouwa Watanzania 50 na kujeruhi wengine walionusurika kifo imetokana na mashimo ya barabarani!

Kwa hili, ikibidi hata kipenzi cha roho yangu Rais Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete kuwajibika basi uwajibike.

Hakuna ajali hapo, kuna uzembe wa hali ya juu!

Naomba kuwasilisha.

Na nnalia kwa vifo vya Watanzania wenzangu na wale wote wanaowalilia na nnasikitishwa zaidi kila nnapowafikiria wale waliokatizwa ndoto zao kwa kuondokewa na walio karibu nao.

Kama hayo hayajatekelezwa sitokusamehe Kikwete, na Mwenyeezi Mungu hatokusamehe na Watanzania hawatokusamahe.

Eeeh Allah nnakuomba nisameh kama nimekosea lakini nnalia, nnalia, nnalia.
Huyu sasa ndiye yule FF tuliyemkuta jf sisi wengine tulipo join, sijui alikwenda wapi,lakini sasa amerudi.

Mkuu FF, pole!, ulipotea sana na kipindi haupo, kuna impostor fulani aliitumia jina lako, huyu alikuwa na akili robo yako, afadhali sasa mwenyewe umerudi.

Karibu tena na pole kwa kuumia!.

Pasco
 
....vilivyounganishwa vikaja na jina CCM, Chama Cha Mapinduzi, sijui walipindua nini au jina hilo lilitokana na nini ...
Baada ya hapo sijaona kilichopinduliwa na "Chama Cha Mapinduzi" kwa miaka kadhaa mpaka ujio wa Jakaya (Jee, mnajuwa maana ya "Jakaya"?).

Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete ndiye Rais wa pekee Tanzania hii kutokea CCM aliyedhihirisha na kunikinaisha kuwa "mapinduzi" yapo na yanawezekana. Hususan miaka takriban tisa (9) baada ya kushika hatamu ya utawala nilimsikia, kupitia TV, wakati akiongea na "wazee wa Dar" alipoongelea "sakata la Escrow", akisema kuwa, siasa ya "kutaifishana" (kwa uchache) tuliachana nayo. Hapo ndipo nilipohisi kuwa mapinduzi ndiyo hayo! na aliyediriki ni Kikwete.

I like this .. ila, isije ikawa juzi alikuoverlook kwenye uDC?
 
FaizaFoxy kwani nyie watu wa CCM mnakufaga ?? Nyie si mtatawala milele ?

Wanaokufa ni sisi walalahoi wala usiwe na hofu.
Nyie mnapaa tu na mindege hewani kishomo kitokee wapi huko hewani?

Nyie ni wa milele, hamfi
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy kwani nyie watu wa CCM mnakufaga ?? Nyie si mtatawala milele ?

Wanaokufa ni sisi walalahoi wala usiwe na hofu.
Nyie mnapaa tu na mindege hewani kishomo kitokee wapi huko hewani?

Nyie ni wa milele, hamfi

= mnakufa

bibiyo na babuyo wako wapi?
 
Una haki na mawazo yako, lakini kumbuka kuwa sikujitambulisha kama utakavyo wewe ieleweke, kwani hakuna mwana JF asiyejuwa kuwa FaizaFoxy ni CCM, ni Muislam, na asiyekubaliana hata moja na muasisi wa CCM, Nyerere. Naomba kumbuka hayo.

Mimi nime "declare interest". Sijuwi kama unaelewa maana yake?

Nnalia, nnalia, nnalia.


Unaikubali bakwata ambayo imeanzishwa na mwalimu
 
Haijalishi hata leo hii usipoamini kwamba nimeshazaliwa tayari, kuna wengi wetu pia ni mashabiki wa iliyokuwa Tabora Rangers, Lipuli ya Iringa kwa kuwa tu zilikuwa timu zilizopendwa na wazi wetu na kupenda timu nyingine ni kumkosea Baba!

Hapo ndipo unapoleta hoja dhaifu kutokana na kutaka ubishani usio na maana.

Mimi CCM na ntabaki kuwa CCM kwa sababu moja kuu, nnaamini katika maboresho "within", na CCM kama ilivyo chama kingine chochote, ina nafasi kubwa sana ya kuboreshwa na hilo linafanyika kila kukicha.
 
Kumbukua kuna waliosema hatuhitaji katiba mpya kwani iliyopa inafaa na hata hii mpya imepuuza mengi ya msingi.

Utawala wa chama kimoja kwa miaka mingi baada ya uhuru ndio umetufikisha hapa tulipo leo.

Nyerere baada ya kutoka madarakani aligundua kosa lake na kuona mfumo wa vyama vingi ungesaidia kukosoa serikali iliyopo madarakani.

Nyerere hakuleta vyama vingi. Ni shinikizo la nchi za Magharibi ili kutukwamua katika umasikini wa hali ya juu aliotuwachia nao Nyerere ndiyo ulipelekea vianzishwe vyama vingi, shinikizo hilo lilifanya hata pale wananchi walio wengi walipotoa maoni yao kuwa tunataka tubaki na chama kimoja, Mwinyi akaona hawa ulikuwa ni uoga wa udikteta ndiyo uliwafikisha kuamua hivyo, hakuwasikiliza na akaanzisha mfumo wa vyama vingi kama alivyotakiwa na "wakubwa" ili misaada ya kiuchumi ianze kumiminika "kutuokoa" or was it kutuopoa?.
 
Hapo ndipo unapoleta hoja dhaifu kutokana na kutaka ubishani usio na maana.

Mimi CCM na ntabaki kuwa CCM kwa sababu moja kuu, nnaamini katika maboresho "within", na CCM kama ilivyo chama kingine chochote, ina nafasi kubwa sana ya kuboreshwa na hilo linafanyika kila kukicha.

Siku CCM itakapokufa natural death kwa uzee na uchakavu wa sera zake unakaribishwa kwenye chama kitakachoshika hatamu...wewe njoo tu na ideology zako za CCM thereinafter utapigwa shule ujitambue na utakuwa raia mwema!
 
Siku CCM itakapokufa natural death kwa uzee na uchakavu wa sera zake unakaribishwa kwenye chama kitakachoshika hatamu...wewe njoo tu na ideology zako za CCM thereinafter utapigwa shule ujitambue na utakuwa raia mwema!

Haya, endelea kusubiri. Uko huru.
 
Haya, endelea kusubiri. Uko huru.

Mwenyezi Mungu akupe kheri uishi maisha marefu ili ushuhudie mabadiliko na wakati yatakapotukia uwe balozi mwema wa kueleza kizazi kijacho kwamba hapo zamani za kale palikuwepo CCM, ikakua, ikazeeka na kufa na kwamba ilipokaribia kufa mliokuwa minazi ya chama ilikupeni wakati mgumu sana na hamkujua kwamba maisha yangaliweza kusonga mbele bila CCM!
 
Hili tatizo linasababishwa na serikali ya CCM very shame. CCM is idiot political party. Hiyo barabara ni mbovu lakini hawaoni mimi napita mara kwa mara, barabara imejaa mashimo hivyo madereva wengi huhama site kukwepa mashimo. CCM unaua watu ona ulivyo mchafu kwa madhambi, umejaa viongozi mashetani msio na huruma Mungu awalaani nyie wana kulaaniwa. Watanzania 50 wanakufa on the spot kwa uzembe wenu. Mnaiba pesa mnaacha kutengeneza miundo mbinu ona sasa mnaua watu. Say no to ccm.
 
Nadhani kwa uzembe huu wanaohusika wote wanyongwe

adhabu yavkunyongwa ndo suluhisho kama wafanyabyo nvhi zingine kama korea.. China n.k
 
Umeongea. Leo aanze Jakaya na Waziri mkuu kuwajibika. Jakaya amekunywa damu za Watanzania wengi kila pande wa nchi ni vilio. Ajali zimetawala. Jakaya amemaliza hata albino. Jakaya watoto wametekwa eti wanasomeshwa dini. Je hiyo njia wamepitia watoto wangapi? Wameishia wapi?


Jakaya sasa imetosha. Waachie jeshi hii nchi kwa huu muda wa mpito.

Jakaya imetosha.
 
Back
Top Bottom