Tuseme Ukweli: Masikitiko Yangu Vifo Vya Watanzania

Tuseme Ukweli: Masikitiko Yangu Vifo Vya Watanzania

Kwa jambo hili, nakubaliana kabisa na mawazo yako FaizaFoxy.

Kwa uzembe huu, kuna watu wanapaswa kuwajibika.
 
Bi Faiza na Chama chako cha mapinduzi usiyejua kilipindua nini nikuunge mkono pia hujui ni kwanini pia ulikipenda ilipotokea kukipenda na bado unaendelea tu! Nina shaka kama unajua majukumu ya idara zote ulizozitaja kwenye uwajibikaji kutokana na sakata la ajali iliyopoteza watanzania wengi jana bila kujali itikadi yao ya vyama wala imani!

Kwa kuwa unataka bodi ya usajili ya wakandarasi (CRB) iwajibike kutokana na ajali ya Mafinga (kwa kuwa ndio wenye dhamana ya kusajili makandarasi) basi nenda mbali zaidi kwa kumwajibisha Mkunga aliyekuwepo zamu wakati madereva wa magari yaliyohusika katika ajali hii awajibike,na wazazi wa madereva tajwa wawajibike pia kwa kuwazaa!

Ishauri serikali ya chama chako iiwajibishe mamlaka ya utoaji zabuni (PPRA) kwa kuwa ndio wana dhamana ya kusimamia zabuni na kupitia usimamizi huo ndipo mkandarasi wa barabara iliyotokea ajali alipatikana! Wajibisheni pia viongozi wa serikali za mitaa na wananchi wa eneo la changarawe kwa kuwa eneo lao ndiko ajali ilitukia!

Hapo umekosea, sana tena.

Nnajuwa kwanini nilikipenda na nnajuwa kwanini nnakipenda hadi leo hii. Kumbuka hilo.

Chama cha CCM, kama wewe unakijuwa tu kuwa ni CCM, mimi nnakijuwa kilikoanzia, kabla ya kuwa CCM na nna historia nacho kutoka uhai wa wazee wangu. Jengo la CCM la Mkoa wa Dar, ubavu kwa ubavu na nyumbani kwetu nilipozaliwa na nilipokulia (kwa sasa kuna ghorofa), nyumba ilipozaliwa TANU na kabla ya hapo ilikuwa ya TAA ni nyumba ambayo toka nnazaliwa nnaiona, nyumba ya pili kutoka nilipozaliwa.

Nyerere, wewe unamsikia tu, mimi nnamjuwa toka utotoni na nimeshamuuzia sigara karata, kwa mkono wangu, kwetu tulikuwa na duka enzi hizo.

Nyerere mpaka kabla ya kung'atuka akija CCM basi siku ambazo anaweza kuwa na dakika tano za ziada akija kwetu kusalimia. Kumbuka hilo.

Usijaribu kutia maneno yako kinywani mwangu.

Nnalia, nnalia, nnalia.
 
Tatizo si CCM wala CHADEMA, hebu tuseme ukweli.

Tatizo ni misingi mibovu iliyounda hii nchi inayoongozwa na katiba mbovu iliyoundwa na a/walioweka misingi mibovu.

Ukweli ubaki kuwa ukweli. Tusioneane haya katika ukweli.
Kumbukua kuna waliosema hatuhitaji katiba mpya kwani iliyopa inafaa na hata hii mpya imepuuza mengi ya msingi.

Utawala wa chama kimoja kwa miaka mingi baada ya uhuru ndio umetufikisha hapa tulipo leo.

Nyerere baada ya kutoka madarakani aligundua kosa lake na kuona mfumo wa vyama vingi ungesaidia kukosoa serikali iliyopo madarakani.
 
Hapo umekosea, sana tena.

Nnajuwa kwanini nilikipenda na nnajuwa kwanini nnakipenda hadi leo hii. Kumbuka hilo.

Chama cha CCM, kama wewe unakijuwa tu kuwa ni CCM, mimi nnakijuwa kilikoanzia, kabla ya kuwa CCM na nna historia nacho kutoka uhai wa wazee wangu. Jengo la CCM la Mkoa wa Dar, ubavu kwa ubavu na nyumbani kwetu nilipozaliwa na nilipokulia (kwa sasa kuna ghorofa), nyumba ilipozaliwa TANU na kabla ya hapo ilikuwa ya TAA ni nyumba ambayo toka nnazaliwa nnaiona, nyumba ya pili kutoka nilipozaliwa.

Nyerere, wewe unamsikia tu, mimi nnamjuwa toka utotoni na nimeshamuuzia sigara karata, kwa kono wangu, kwetu tulikuwa na duka enzi hizo.

Nyerere mpaka kabla ya kung'atuka akija CCM basi siku ambazo anaweza kuwa na dakika tano za ziada akija kwetu kusalimia. Kumbuka hilo.

Usijaribu kutia maneno yako kinywani mwangu.

Nnalia, nnalia, nnalia.


Haijalishi hata leo hii usipoamini kwamba nimeshazaliwa tayari, kuna wengi wetu pia ni mashabiki wa iliyokuwa Tabora Rangers, Lipuli ya Iringa kwa kuwa tu zilikuwa timu zilizopendwa na wazi wetu na kupenda timu nyingine ni kumkosea Baba!
 
Inasikitisha sana na kwa alie tazama ajali ile tutakubaliana kwamba kweli ..inakufanya mtu ukate tamaa ya kuishi. Na ukifuatilia yale majina utaona kuna watu wa familia moja!!! ..ili ni pigo kwa Tanzania na familia zilizo adhirika.

Kwa swala la kuwajibika ilo kwa Tanzania ni ndoto, ata kama mtoa tamko ulikuwepo kipindi icho cha uhuru sidhani, labda kama mwenzetu wewe ndo mama salma au mama nyerere / bibi wa taifa.

Namuomba Mungu awaponye wagonjwa wote wa ajali ile, walio tangulia wapumzike kwa amani na familia zilizo patwa na janga ilo azipe nguvu. Amen

= athirika

Hapana mimi si "mama salma au mama nyerere / bibi wa taifa.".

Nnakuelewa unaposema "kuwajibika ilo kwa Tanzania ni ndoto", lakini nnauhakika ni wajibu wetu pia kkuoneshwa kukerwa kwetu. Au wewe unafikiri ni "mama salma au mama nyerere / bibi wa taifa." tu ndiyo wenye kuwa na uchungu zaidi ya Watanzania wengine? Fikiri.
 
Kule Mbeya, kuna mama alisafirisha ndugu zake 5. Inatajwa kuwa wote watano wametangulia mbele za haki. Ni simanzi kubwa.
Tukija kwenye kuwajibika sioni ni kwa namna gani CRB wanaingia hapo! Kazi yao kubwa ni usajili wa Wakandarasi. Eneo husika hakukuwa na ujenzi wowote angalau tungesema yeye anahusika. Wa kulaumiwa labda ni Tanroads mkoa, ingawa napo siyo sana, pengine hawakuwa na fungu. Kumbuka Tanroads hao hao kwa kushirikiana na Mhandisi mshauri wamejenga barabara ambayo ni super hapa Tanzania. Inaanzia Ruaha Mbuyuni hadi Mafinga, umbali wa kilometa kama 200. Pale walipoishia ukitoka kidogo barabara ndo mbovu na ndo hapo hapo janga lilipotokea. Hivyo siyo vema kuwalaumu Tanroads sana, kwani eneo walilojenga ni umbali mrefu na ambao naamini ni gharama kubwa, labda eneo lingine ambalo kimsingi kwa sasa liko Njombe na Mbeya barbara ni mbovu sana, traffic polisi walimtaarifu dereva awe makini mashimo ni mengi,na ni kwa eneo kubwa la barabara ambalo ni pesa hasa!
 
Sio kila usilolijua wewe ni ujinga kuna wakati unatakiwa kujua pengine unayoyajua ni ujinga kwa wengine!

Nisilolijuwa ni "usiku wa kiza" na siyo ujinga. Ujinga ni kutolielewa unalolijuwa, kama ulivyo wewe.

Nnalia, nnalia, nnalia.
 
Toka nikufahamu at least umeongea pwoynti. Sii bure roho mtakatifu kakutembelea.Bwana ametoa, Bwana ametoa jina la Bwana lihimidiwe.
 
Kumbukua kuna waliosema hatuhitaji katiba mpya kwani iliyopa inafaa na hata hii mpya imepuuza mengi ya msingi.

Utawala wa chama kimoja kwa miaka mingi baada ya uhuru ndio umetufikisha hapa tulipo leo.

Nyerere baada ya kutoka madarakani aligundua kosa lake na kuona mfumo wa vyama vingi ungesaidia kukosoa serikali iliyopo madarakani.


Nasikitika sana kwa umri wangu nilionao jua langu litakuchwa pasi kuona mabadiliko hasi toka kwa niliyotegemea wajitambue...

Kwa kuamini kila zama ina kitabu chake ni vyema tukabaki na dhana hiyo kwamba Mwalimu Nyerere hakua malaikana alikuwana udhaifu wake kama tulivyo binadamu wengine,tulichokosea ni kuacha kuendelea mbele kutoka alipotuacha mwalimu na badala yake tumebaki walalamishi tu, wa kulalamikia historia!

Siamini katika saiasa naamini katika utendaji/uwajibikaji na uadilifu...bila kuwa muadilifu hata ungeingia kwenye mfumo usio wa kichama bado hatututasogea popote ila tutarudi nyuma kuliko zama za kina Mangungo,Isike, Machemba na Kinjekitile!
 
Khaaa!!! Waziri mkuu unamwita "kikaragosi" Mbona leo umekuwa mkali hivi! Ndio maana hajakupendekeza uwe mkuu wa wilaya, kumbe unamdharau!!

Kumbuka kuwa kuna nchi kutokana na muundo wao, Rais anakuwa "kikaragosi" mfano India na au Ujerumani, wao huongozwa na Waziri Mkuu.

Hapa kwetu Waziri Mkuu ni "kikaragosi" tu, hawezi kumwajibisha hata waziri wake akikosa, au katibu mkuu wa wizara ambazo yeye ni "Waziri Mkuu"?. Sidhani kama Waziri Mkuu wa Tanzania anaweza kumwajibisha hata karani wa wizara yoyote ile. Kumbuka hilo.
 
Mkuu umeongea kwa uchungu sana lkn hakuna la kufanya ni kumshukuru Mungu tu kwani unafikiri hao uliowataja hawajui au huwa hawaoni hizi barabara zetu.Ni jambo la ajabu kuona ajali inasababishwa na mashimo kama kwamba ni jambo la ghafla. RIP marehemu wote na waliojeruhiwa Mungu awaponye
 
Kule Mbeya, kuna mama alisafirisha ndugu zake 5. Inatajwa kuwa wote watano wametangulia mbele za haki. Ni simanzi kubwa.
Tukija kwenye kuwajibika sioni ni kwa namna gani CRB wanaingia hapo! Kazi yao kubwa ni usajili wa Wakandarasi. Eneo husika hakukuwa na ujenzi wowote angalau tungesema yeye anahusika. Wa kulaumiwa labda ni Tanroads mkoa, ingawa napo siyo sana, pengine hawakuwa na fungu. Kumbuka Tanroads hao hao kwa kushirikiana na Mhandisi mshauri wamejenga barabara ambayo ni super hapa Tanzania. Inaanzia Ruaha Mbuyuni hadi Mafinga, umbali wa kilometa kama 200. Pale walipoishia ukitoka kidogo barabara ndo mbovu na ndo hapo hapo janga lilipotokea. Hivyo siyo vema kuwalaumu Tanroads sana, kwani eneo walilojenga ni umbali mrefu na ambao naamini ni gharama kubwa, labda eneo lingine ambalo kimsingi kwa sasa liko Njombe na Mbeya barbara ni mbovu sana, traffic polisi walimtaarifu dereva awe makini mashimo ni mengi,na ni kwa eneo kubwa la barabara ambalo ni pesa hasa!

Wana faida gani kama ni wataalam na wanashindwa kuishauri Serikali na waliopo madarakani kwenye kitu kama hicho cha kuwa na mashimo kwenye njia kuu ya Kimataifa? Fikiri.
 
Fikiria hii kila mtu anajua barabara ya Bagamoyo imezinduliwa na Rais
na waziri husika anasifika kuwa mchapakazi na wengine wanataka awe Rais
huku wote tunajua hiyi barabara haina taa hata moja
kuanzia mwenge hadi tegeta ni giza nene kiasi kwamba madereva wote wanaweka full ili kuona barabara
na kila mtu anajua hatari ya ajali ya giza na kuweka full barabarani....

ajabu zaidi hakuna hata mtu mmoja wa kuongelea hilo
TB fanya uongelee hilo hata wewe. Sio lazima umsubiri mwingine mkuu.
 
Hhahahahahaa hii I'd imekuwa hacked I swear FaizaFoxy kama ni wewe kuna kitu kimekupata
 
FaizaFoxy u made my day "kwa hili ilibidi hata tezi dume kuwajibika awajibike"
 
Last edited by a moderator:
ok
umeonge vizuri lkn why ujivunie U-ccm????
umezaliwa na ccm kwani..
we unafikiria kuwa unaijua sana ccm faiza??

nakushauri jivunie ww mwenyewe coz you can account for yourself even in front of God
 
Back
Top Bottom