Tusaidiane tafadhalini hawa Paka wa Dar es Salaam ni Wanyama au Binadamu wenzetu tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,890
109,608
Tokea nizaliwe sijawahi kuona kama siyo kusikia Mnyama Paka akikohoa na kupiga chafya ila kwa muda wa Siku kama Nne hivi nimebahatika kulala maeneo tofauti tofauti hapa Jijini Dar es Salaam kama vile Mbezi ya Kimara, Mbagala, Sinza na Tegeta Masaiti na kuona maajabu.

Zamani hapa Dar es Salaam ilikuwa Paka akikuona tu lazima atoke ' Nduki / Akimbie ' lakini kwa miaka ya hivi karibuni Paka ndiye amekuwa akitutoa ' Nduki / Akitukimbiza ' Sisi Wanadamu na kuna muda anaweza akawa anakukimbiza huku anakuita kabisa na jina lako.

Nina wasiwasi mkubwa sana kama Paka wa sasa hivi wa Dar es Salaam ni Wanyama kweli kweli.

Nawasilisha.
 
IMG_20180704_234255_016.jpg
 
Hahahahahah! hiyo ndo bongo Dar es salama sisi huku koromije maajabu yetu ni kuona Harrier new Model ikipita kijijini kwetu, maisha yetu sisi usafiri kwama la ng'ombe mnyama, asubuhi kiporo cha ugali na kikombe cha maziwa mgando. Karibu kwetu
 
Dah! Nimecheka sana.
Hapa inabidi tumuite kaka Mshana Jr.
Atupe kaelimu kidogo juu ya hizo paka.
 
Dar sio paka tuu hadi mbuzi.
We mbuzi anakunywa bia huyo ni mbuzi?
Mbuzi anakunywa chai na chapati.. Mbuzi hachagui hadi mlenda anapeleka

Mkuu basi nisamehe bhana unajua Mimi nikicheka sana hadi kuvunjwa mbavu Kifua changu cha Pumu huwa kinanitesa. Nimecheka hakuna mfano! Kuna Watu mpo humu JamiiForums ni ' Comedians ' wazuri sana. Ndiyo maana naipenda JamiiForums kunakotukuka. Yaani Mkuu hii ' post ' yako kila nikiirudia Kuisoma mbavu zangu zinavunjika tu. Ahsante!
 
stardust JK hivi umefikiria nini hadi umeandika hivyo hiyo ' post ' yako # 7? Hakyanani sijawahi Kucheka kama ninavyocheka sasa. Halafu kuna Watu walikuwa wanataka JamiiForums isiwepo kabisa katika kutoa Huduma zake hivi hizi furaha na Kuchekeshwa hivi hadi ' Stress ' zetu tunazisahau kwa muda kama siyo kuzipunguza mngetupa nyie?

Ama hakika Long Live JamiiForums!!!!!!!
 
Mkuu basi nisamehe bhana unajua Mimi nikicheka sana hadi kuvunjwa mbavu Kifua changu cha Pumu huwa kinanitesa. Nimecheka hakuna mfano! Kuna Watu mpo humu JamiiForums ni ' Comedians ' wazuri sana. Ndiyo maana naipenda JamiiForums kunakotukuka. Yaani Mkuu hii ' post ' yako kila nikiirudia Kuisoma mbavu zangu zinavunjika tu. Ahsante!
Usipo cheka kwenye huu Uzi basi hucheki tena maisha.
Doh! Et mbuzi anapiga chai kwa chapati.
Paka anakukimbiza huku anakuita jina loh!!
Wakati mwingine muwe mnaonea huruma mbavu zetu wakuu.!!
 
Usipo cheka kwenye huu Uzi basi hucheki tena maisha.
Doh! Et mbuzi anapiga chai kwa chapati.
Paka anakukimbiza huku anakuita jina loh!!
Wakati mwingine muwe mnaonea huruma mbavu zetu wakuu.!!

Mimi mkicheka nyie na kuburudika ndiyo furaha yangu hasa kwani japo najua maisha ni magumu na Watu wanahangaika ila Kufurahi pia ni jambo jema na muhimu sana.
 
Paka wa Dar ndiyo wamekuwa wanaume siku hizi na vijanadume vya Dar ndiyo vimegeuka kuwa mapaka shume, kelele kibao ila hawana lolote.
 
Back
Top Bottom