Kuwashwa mwili ni tatizo jipya Dar es Salaam?

DALALI MKUU

JF-Expert Member
May 7, 2022
1,487
2,739
Salaam wakuu.

Siku za hivi karibuni nimeona na kushuhudia wakazi wengi hapa Dar es salaam wametokwa na vipele na kuwashwa mwili.

Hasa watoto nimeona wengi pia wanawashwa na vipele mwili mzima. Hivyo nauliza, huu ni ugonjwa wa kawaida au Kuna tatizo lipo?

Nauliza na nini cha kufanya ikiwa utapata shida Kama hiyo?
 
Salaam wakuu.
Siku za hivi karibun nimeona na kushuhudia wakazi wengi hapa dar es salaam wametokwa na vipele na kuwashwa mwili.

Hasa watoto nimeona wengi pia wanawashwa na vipele mwili mzima.
Hivyo nauliza je huu ni ugonjwa wa kawaida au Kuna tatizo lipo.?
Nauliza na Nini Cha kufanya ikiwa utapata shida Kama hiyo.
Hili tatizo linaenea kwa kasi nchini japo mamlaka za magonjwa hazijui na hazina taarifa kuwepo kwa tatizo hilo. Mwili huwasha na kutoka vipele, hivo vipele vikikauka ngozi hubanduka tabaka la juu kama nyoka ajivuaye gamba. Haijulikani ni ugonjwa gani na unasababishwa na nini
 
Mna uhakika maji ya bomba mnayokunywa ni salama?

Wengi wenu ni vipofu nyie, mtaanza kusema kuna VIRUS yuko angani anawabutua watoto na kuwatumbua mapele. 🤣

Angalieni maji ya bomba hayo kama hayajatiwa madawa fulani. Au chakula wanachokula.

Hakuna cha jotro wala nini. Jotro lipo miaka yote.
 
Unajidanganya.

Labda madaktari tu ndo hawajui, maana wale pia ni vipofu wanaosubiri MAAGIZO ya SEREKALE.

Lakini akina SAMIA wanajua. Muulizeni, ana taarifa zote mezani, nothing goes UNCHECKED.
sasa kama mamlaka za kutangaza magonjwa zina taarifa ya kuwepo kwa vipele hivyo kwa nini wasitangaze kama wafanyavyo kwenye red eye, maana wengine tumeingiwa mfadhaiko tukidhani tayari tumeambukizwa magonjwa makubwa ya kutisha japo hatujapima tujue afya zetu. Vipele vinawasha balaa, vikipasuka hufanya ngozi kupauka
 
hili tatizo linaenea kwa kasi nchini japo mamlaka za magonjwa hazijui na hazina taarifa kuwepo kwa tatizo hilo. Mwili huwasha na kutoka vipele, hivo vipele vikikauka ngozi hubanduka tabaka la juu kama nyoka ajivuaye gamba. Haijulikani ni ugonjwa gani na unasababishwa na nini
Hii ni hatar Sana
 
Mna uhakika maji ya bomba mnayokunywa ni salama?

Wengi wenu ni vipofu nyie, mtaanza kusema kuna VIRUS yuko angani anawabutua watoto na kuwatumbua mapele. 🤣

Angalieni maji ya bomba hayo kama hayajatiwa madawa fulani. Au chakula wanachokula.

Hakuna cha jotro wala nini. Jotro lipo miaka yote.
Maji haya haya au
 
Joto Kali na ukosefu wa maji ni janga kwa Dar es salaam kama huyu bibi akigombea 2025 na akashinda tuna miaka mitano Tena ya kutaabika kwa kuwashwa miili
Siyo sababu mi naona anga tu limechafuka....huku mbeya ndiyo wameharibika mno....wanaambia ni allergy
 
Back
Top Bottom