mkuu imani ni kitu cha ajabu sana , unaweza ukaamini ikawa na unaweza ukaamini na isiwe , mfano wa hizi imani ni ushirikina . kuna bwana mmoja alikuwa ana shamba na kila kukicha anaibiwa vitu vyake shambani , siku moja aliambiwa dawa la hilo tatizo ni kumleta mganga azindike shamba aliyeaminika kwa ulozi kweli kweli , jamaa akampa mganga hela ndefu akiwa na imani ya kuzindikiwa shamba na kweli kazi ilifanyika kwa kuweka tunguri kila pembe ya shamba zikining'inia .kesho yake wazee wa kazi walikuja na manati wanatungua tunguri(kibuyu) ,kimoja baada ya kingine na kukomba kila kitu shambani kuliko hata kipindi cha nyuma . jamaa alichanganyikiwa na kumfata mganga ampe hela zake . kwa hiyo basi ninalotaka kusema imani ni vitu ambavyo vinaweza vikakusaidia au vikakumaliza kabisa , iwe ya kidini ya kishetani au ya kienyeji(mf. kweny mpira goli la upande fulani huwa halilali njaa yaani kufungwa)