Tupia imani ya kale uliyowahi kusikia

Ukishona (kurudishia uzi au kifungo) nguo huku umeivaa utakuwa masikini.
 
mtoto aking'oka jino, ni sharti litupwe uvunguni mwa kitanda; kinyume chake, jino halitaota tena.
 
Ukipiga miluzi usiku unaolewa na mwanaume mchawi na kama we ni mwanaume basi unaoa mwanamke mchawi
 
ukimuona albino unatemea mate kifuani mama yako asije kumzaa albino!
du!!! hii ilinitesa sana nilivyokuwa mdogo , mpaka nalia na washikaji wanakukomalia kwamba ni kweli , mzazi ndiyo anakutuliza kwamba si kweli basi siku nzima unashinda ndani , utoto ni kipindi kizuri sana ni maisha ya hapo hapo ulipo hakuna kuwaza
 
mkuu imani ni kitu cha ajabu sana , unaweza ukaamini ikawa na unaweza ukaamini na isiwe , mfano wa hizi imani ni ushirikina . kuna bwana mmoja alikuwa ana shamba na kila kukicha anaibiwa vitu vyake shambani , siku moja aliambiwa dawa la hilo tatizo ni kumleta mganga azindike shamba aliyeaminika kwa ulozi kweli kweli , jamaa akampa mganga hela ndefu akiwa na imani ya kuzindikiwa shamba na kweli kazi ilifanyika kwa kuweka tunguri kila pembe ya shamba zikining'inia .kesho yake wazee wa kazi walikuja na manati wanatungua tunguri(kibuyu) ,kimoja baada ya kingine na kukomba kila kitu shambani kuliko hata kipindi cha nyuma . jamaa alichanganyikiwa na kumfata mganga ampe hela zake . kwa hiyo basi ninalotaka kusema imani ni vitu ambavyo vinaweza vikakusaidia au vikakumaliza kabisa , iwe ya kidini ya kishetani au ya kienyeji(mf. kweny mpira goli la upande fulani huwa halilali njaa yaani kufungwa)
 
Kuna imani za kale zilizoaminiwa na jamii ktk makabila na tamaduni mbalimbali mfano
1.UKIPALIWA KUNA MTU ANAKUSEMA
2.JOGOO AKIWIKA USIKU UJUE KUNA MTU ATAKUFA
3.MKONO WA KULIA UKIWASHA UTAPATA PESA
tupia na wewe imani uliyowahi kusikia

Ukijiangalia kwenye kioo usiku utakuwa mweusi
 
ukidindisha gafla bila wazo la ngono basi ujue kuna msichana anakuwaza tena kashikilia `k' yake
 
Ebwana mkuu umenikumbusha mbali sana..
Unajua nlikua nafatilia hiz iman ambazo tunaziita za zaman kwa muda kidogo na nikagundua wazee wetu wa zaman walikua na uwezo mkubwa wa kufkiri na walikua watu siasa nzur kwa kias chake ukiangalia misemo hii ming ina maana ya kumkataza kijana ktu flan ambacho kingeweza kumdhuru kirahisi au kuharbu maadili kirahisi na kwa kuwa waafrika tulikua watu wa kuamin iman za aina hz ikawa rahisi hii misemo kushikwa na kuenezwa...
Misemo na maana yake nionavyo mimi (km nimekosea mtanirekebisha)..
Usikalie majifya utaota majipu- majifya ni kwa kupikia chakula soo si vzr kukalia sehem ya kupikia hailet picha nzur.
Usishone nguo usiku ni mwiko- wanakuepusha usije kujichom coz enz hzo taa zlikua hazna mwanga wa kutosha km ss.

Usikojoe alipokojoa mwenzio mamako atavmba manyonyo- kuna hatar ya kupata maradhi ya njia ya mkojo..
Na misemo mingne mingi jarbun kuichunguza
 
Kuna imani za kale zilizoaminiwa na jamii ktk makabila na tamaduni mbalimbali mfano
1.UKIPALIWA KUNA MTU ANAKUSEMA
2.JOGOO AKIWIKA USIKU UJUE KUNA MTU ATAKUFA
3.MKONO WA KULIA UKIWASHA UTAPATA PESA
tupia na wewe imani uliyowahi kusikia

1. Mvua ikinyesha mchana ujue simba anazaa. 2. Marufuku kuloweka sufuria lililopikiwa ugali pamoja na mwiko wake maana ni matusi kwamba watu wa jinsia tofauti wamemaliza kufanya mapenzi wakasahau kujisafisha/ kuoga. 3. Marufuku kuacha mchi wa kutwangia ndani ya kinu maana ni matusi kwamba inaashiria watu wawili wanafanya mapenzi hadharani. 4. Mkiwa mnaongea mara pakatokea kimya cha ghafla ujue shetani anapita. 5. Ukivimbiwa chukua mwiko gusisha kwenye tumbo lako fanya kama vile unapakua chakula kutoka kwenye chungu/sufuria. 6.Mtoto akiumwa ugonjwa wa DEGEDEGE mning'inize kichwa chini miguu juu kwenye shimo la choo. Kwa leo inatosha, wengine watupie zao.
 
Ndugu, Mimi si mtaalaam wa lugha adhimu ya Kiswahili,
Lakini, naomba nikujuze,:
Kunako Kiswahili sanifu, abadan hatuna BAHATI NZURI. WALA BAHATI MBAYA.
*Unaweza ukawa na BAHATI ama MKOSI. Hivyo tu.
--(Walisema waungwana kurekebishana)--
Ahsante.


jicho la kulia likiwasha ujue: Bahati,
Jicho la kushoto liwasha: Bahati mbaya,
 
Ukibanwa na Mkojo Njiani na Ukikojoa unatemea mate mkojo hapo chini na unasema maneno haya... Baba na Mama Wapite lakini Shetani asipite...
 
Ukitaka usiote vitu vya kutisha usiku chini ya kitanda usawa wa Kichwa unaweka Kiatu kimoja...

Usiku usifagie

Usiku wanaofua nguo ni Wachawi pekee...

Usiku Usiseme Chumvi ni Nuksi Mjomba wako anaweza akafa sema Dawa ya Mboga tu
 
Back
Top Bottom