Tupia imani ya kale uliyowahi kusikia

Kuna imani za kale zilizoaminiwa na jamii ktk makabila na tamaduni mbalimbali mfano
1.UKIPALIWA KUNA MTU ANAKUSEMA
2.JOGOO AKIWIKA USIKU UJUE KUNA MTU ATAKUFA
3.MKONO WA KULIA UKIWASHA UTAPATA PESA
tupia na wewe imani uliyowahi kusikia

That on Judgment Day, the dead bodies would arise just as portrayed in Michael Jackson Thriller Video!
 
Ukivaa kiatu kimoja mama yako atakatika ziwa moja

Ukigeuza kiatu juu chini unamtukana Mungu

Mtoto akitia ufunguo mdomoni haoti meno

Mtoto akinyonyeshwa titi na mwanamke ambae hatoi maziwa atakuwa bubu

Mjamzito akikalia kinu atazaa mtoto miguu itatangulia

Mama mwenye uchungu akiwa kafunga kilemba cha juchwa (scarf) hawezi kuzaa ng'oo mana anakuwa kama kajiwekea kitanzi

Usiite mtu usiku kwani shetani atalijua jina lake then atakuja na yeye kumwita na akimchukua harudi tena

Mtoto mchanga kuwekewa ndimu, kisu na kaa la kupikia ili iwe kinga


Ukizika kitovu cha mtoto chini ya mnazi atakua mrefu

Mtoto akicheka wakati amelala anakua anaambiwa na malaika kuwa baba yake atakufa so anafurahia urithi.
Na akilia anaambiwa na malaika mama yake atakufa, so analia atakosa Nyoyo.
 
Mtoto mdogo chini ya miaka mitano akifagia ujue kuna wageni.
Wakati unakula ukijiuma ulimi ujue kuna mtu anakusema.
Wanawake haruhusiwi kula kichwa cha samaki.
Wanaume hawatakiwi kunawa au kulia ndani ya sufuria lenye ukoko wa ugali.
 
1. kama wenzio wamekaa we ukasimama unawanyonya Damu
2. Kajibu kwenye jicho umemchungulia mamkwe
 
Ikiwa umefanya kosa kubwa, chukua unywele wako weka chini ya kizingiti cha mlango, mdingi au mother aki step juu yake basi ujue atasahau kukuchapa.
 
Jicho likikucheza kuna mgeni anakuja cku hyo, ukijing'ata kuna mtu anakusema, ukijikwaa safari unayoenda si salama. Ila imani hizi hazina mashiko yoyote!
 
Back
Top Bottom